Wito: CJ Prof. Ibrahim Juma, make a historia kwa Mahakama kutimiza wajibu wake kulinda haki. Tumia Suo Moto kui-check Serikali pia ruhusu Pro Bono

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,467
113,574
Wanabodi

Samahani. Naomba kuanza na kuomba msamaha kwa kutumia maneno ambayo sio ya lugha ya Kiswahili wala lugha ya Kiingereza bali ni maneno ya lugha ya Kilatini kwasababu sikijui Kiswahili chake, wala Kiingereza chake, ni maneno ambayo yanafundishwa hivyo hivyo.

Imani Kubwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma.

Japo mimi ni mwandishi tu wa habari, lakini pia nimetoa tongotongo za sheria pale UDSM, kitivo cha Sheria ya enzi zile ikiitwa Faculty of Law (FoL), sasa ni School of Law. Enzi hizo, Jaji Mkuu wa sasa Prof. Ibrahim Juma, enzi hizo akiwa ni Dr, kabla hajaukwaa uprofesa, alikuwa ni mmoja wa waalimu wangu, na pia alikuwa Dean wangu. Waalimu wengine ni Prof. Palamagamba Kabudi alikuwa supervisor wangu wa LL.B dissertation, Dr. Tulia Akson, Dr. Harrison Mwakyembe, Dr. Sifuni Mchome, Prof. Florence Luoga wengine wengi ambao walikuwa waalimu wetu pale sasa wako serikalini. Mwalimu niliyetokea kumpenda sana ni Prof. Issa Shivji, na hivyo kujikuta somo lake nikapiga A, na kuna Mwalimu sikumpenda na sijui alijua, somo lake nikapigwa F, ilivyo pelekea ku DISCO kwa technical DISCO.

Waalimu wa chuo kikuu sio malaika ni binaadamu kama binaadamu wengine hivyo nao wana madhaifu yao. Moja ya madhaifu makubwa ya wanasheria ni pamoja na kujisikia wao ndio wasomi saana, wanajisikia sana, wanaongea vingereza vigumu, bombastics kibao na maneo kibao ya Kilatini. Hivyo mwalimu somo lake nusu ya darasa wakipiga supp, ndio anafurahi heshima adabu!.

Prof. Juma was different just like Shivji, Chris Peter, Kanywani, Mgongo Fimbo na wengine, alikuwa very humble. Uadilifu wake nilikuja kuujua wakati hilo DISCO langu lilipotua mezani kwake yeye akiwa Dean. It is expected yeye as Mwalimu angesimama na Mwalimu mwenzake aliyenitundika DISCO, lakini huyu ni mtu wa haki bin haki, akanisikiliza hoja zangu, akaitisha mtihani wangu, akakuta hilo somo lenye F, nilikuwa na B+ akasimamia ikarudishwa DISCO likafutika.

Hiyo uadilifu wa Prof. Ibrahim Juma katika utendaji haki sio wa mashaka wala wa kuhadithiwa; huyu ni mtenda haki kwa mawazo, maneno na matendo.

Hivyo mtenda haki huyu, sasa ndiye Jaji wetu Mkuu, hivyo hili ni bandiko la kumuomba Prof. Ibrahim Juma, kwa vile yeye ni mtenda haki, na sasa ndiye Jaji Mkuu wa Tanzania, aweke historia mpya ya haki Tanzania, kwa Mhimili wa Mahakama ya Tanzania kutimiza wajibu wake sio tu wa kutoa haki, bali kulinda haki za Watanzania zilizotolewa na Katiba ya JMT, lakini serikali ya JMT ikazipora kwa kuibadili katiba na kunyanganya haki hizo.

Zaidi ya jukukumu la kutoa haki, pia Mahakama kama Mhimili ina jukumu la kufanya checks and balance kati ya Mhimili wa Bunge usijiinue zaidi kuliko mamlaka yake na Mhimili wa serikali usijiinue zaidi kuliko mamlaka yake hivyo kuminya haki zilizotewa na katiba ya JMT.

Kikawaida mahakama hata kama inaona jambo fulani linafanywa na serikali lakini linakwenda kinyume cha haki, haiwezi kujiamulia tuu kuingilia hadi kutokee mtu au Taasisi ifungue shauri ndipo mahakama isikilize na kulitolea maamuzi.

Kuna mambo mengi makubwa ya uvunjaji wa Katiba ya JMT unaofanywa na viongozi wa serikali ya JMT, lakini kwa vile hakuna anayelalamika, mahakama nayo inaangalia tu.

Kuna uvunjaji mkubwa wa haki za binaadam kwa kesi kuchukua muda mrefu bila kukamilika kwa uchunguzi. Mfano mzuri ni ile kesi ya yule wakili wa Arusha aliyekaa mahabusu kwa miaka 7, kwa kesi ambayo ukikutwa na hatia kifungo chake ni kisichozidi mwaka mmoja. Hapa tunapozungumza kuna watu wako mahabusu tangu Rais Magufuli ameingia madarakani hadi leo hazijasikilizwa na watuhumiwa wako mahabusu.

Sasa ufike wakati Jaji Mkuu kuitumia mamlaka yake ya Mahakama kama Mhimili wa kutoa haki, itimize wajibu wake wa kulinda haki za kikatiba kwa kutumia kanuni ya Suo Moto ambapo mahakama yeye yenyewe inapoona haki za kikatiba zimevunjwa na wakuu wa mihimili ya Bunge ya Serikali, inajifungia ndani na kutoa prerogative order hivyo kui-check serikali kwa mahakama kutimiza its role of checks and balance.

Amri za kuzuia mikutano ya siasa, kuruhusu wagombea binafsi, Tume ya Uchaguzi ambayo sio inclusive, DPP kufanya upelelezi kwa miaka na miaka, camera kuingizwa mahakama, watu kubambikiwa kesi sizizo na dhamana, fumueni sheria zote hizi kandamizi. Kesi pekee ambazo hazitakuwa na dhamana zibaki treason na 1st degree murder.

Pia kufuatia baadhi ya watendaji wa serikali haswa ma-RC na ma-DC na watu wengine vicha vichaa, media, kujiinua sana kunyanyasa raia na kutoa kauli mbofu mbofu kwa kuropokaropoka maneno ya ajabu ajabu kuchafua watu zinazokwenda kinyume cha haki za binaadam ikiwemo kutukana watu, kukiuka right to privacy za watu, kukiuka right to privacy za wagonjwa.

Kwa bahati mbaya sana, kwanza sio Watanzania wengi wana uelewa wa sheria kujua kuwa wanakashifiwa, hivyo vichaa waropokaji na wapayukaji wanajipayukia tu kwasababu wanajua hao wanaowapayukia hawawezi kwenda popote.

Pili kuna wanaokashifiwa ambao wanajua wamekashifiwa, lakini wanaamua kuacha tu kwa makusudi kwasababu wanajua kashfa hizo zina baraka za Serikali. Mfano mzuri issue ya makada wa CCM -- Kinana, Membe na Makamba -- kukashifiwa na kichaa mmoja, na baada ya kuandika barua kwenye chama kulalamikia udhalilishaji huo, wakageuziwa kibao kwa kusambazwa voice notes za sauti zao, kitu ambacho ni uliukwaji mkubwa wa rights to privacy.

Tatu kuna wanaojua wanakashifiwa, lakini kujikuta hawa uwezo wa nguvu ya kiuchumi kuajijiri wakili kuwafungulia shauri. Kila siku tunashuhudia media trials kwa washitakiwa kupigwa picha hadi wakiwa mikononi mwa polisi hadi ndani ya vyumba vya mahakama.

Kwa vile sasa Tanzania tuna mawakili wengi wa kutosha, huu ni wakati tunaomba turuhusu sheria ya Pro Bono. Mtu akikashifiwa, mwanasheria unajitolea kumtetea bure, akishinda kesi ndio anakulipa gharama zako.

Kama serikali imeruhusu plea bargain, inashindwa vipi kuruhusu Pro Bono?

Kama tungekuwa na sheria ya Pro Bono viongozi kama hawa wasingekuwa na uwezo wa kuropoka mambo kama haya.

Hitimisho:
Jaji Mkuu Prof Ibrahim Juma, baada ya tuhuma za the Legislature kuji-submit kwa the Executive, nina imani kubwa na wewe ukiamua, unaweza hivyo nakuomba CJ Prof. Ibrahim Juma, make a historia kwa mahakama zetu kutimiza wajibu wake kulinda haki za kikatiba kwa kutumia Suo Moto KuiCheck Serikali na pia its high time Tanzania turuhusu Pro Bono.

Wako wanafunzi mtiifu,

Paskali
 
angalau japo kidogo Pascal umeanza kubadilika badilika kidogo kidogo, leo haujatumia zile 'leading questions' unazo tumia siku zote unapowasiliha nondo zako humu jamvi, turudi kwenye uzi wako huyo prof wako wa sheria anawezaje kutimiza wajibu wake kwa kulinda haki za kimahakama na hali mkononi ana assignments kutoka kwa mteuzi wake ( jiwe ) ya kuwashugulikia 'wabaya' wotee wa awamu hii?
 
Tatizo ni mazingira yaliyopo yanamruhusu aliweza kutoa hukumu ya haki dhidi yako sababu mazingira ya kazi yake yanamruhusu lakini je ataweza kufanya hayo unayoshauri kwa mazingira ya sasa? jibu ni wazi hawezi lakini umezungumzia udhaifu wa mawakili wetu ambao mbali na huo unaoutaja wengi ukimbilia kesi ambazo zina mvuto kwa jamii lakini mpaka sasa wakati mahakama ya Afrika ilishatoa hukumu juu ya mgombea binafsi na serikali kwa wakati ule kusingizia kuwa limepelekwa kwenye bunge la katiba badala ya kufanya utekelezaji bado sijaona wakili yeyote pamoja na kujipachika majina ya wakili wasomi ambaye ameenda mahakamani na kushinikizwa kwa sheria hiyo itekelezwe.Kwa mtazamo wangu ni rahisi kupata katiba mpya pale tutakapoanza kwa na wagombea binafsi kwani vyama vyote vilivyopo vipo kwa ajili ya kulinda maslahi ya watu fulani.
 
Mkuu tatizo kubwa ni maamuzi ya kisiasa, ule upepo wa 2015 ulikua mkali sana, na kwa sasa Mzee baba anajaribu kuupoza labda joto likipungua Mahakama na Bunge vitarudi katika mistari yake
 
Kwanza the Court can not act suo motto in a suit which doesn't exist. That is number one.

Pili, Mahakama,- the court can not work basing on public opinion(be it weakeness or strengths ). The court has to act on its original public trust that is the court of justice .

Tatu, Kangaroo Court(s) is/are always made, it is not in a single day, the whole judicial systems in Tanzania is made, be it Court of Justice or Kangaroo Court is subjected to its very rooted process. Mahakama ya Tanzania iko hapo ilipofika sio kwa bahati mbaya na ni mfumo.

Fikiria District Magistrate wa mlele anamtaka mwananche aseme plaint yake na amedraw na je ana efd ya kudraw, akadismiss , if it need should have rejected.

We have deteriorated ourself into Kangaroo Court, who to blame then.?!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimependa hizo sifa ulizommwagia Prof. Juma, inaonesha ni jinsi gani mtu akiwa independent anavyoweza perform majukumu yake perfectly; but now, take a look at his current state, he is not independent anymore, a simple example what he did to Fatma Karume.

So, you were talking about Prof. Juma wa UDSM, but now, we have the same Prof. Juma, but who belongs to Lumumba Street, not UDSM.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaangalia Tv Remote ipo kwa jirani unaangalia channel ambayo jirani anataka uangalie akitaka ulale anabofya tu remote tv inazima.
 
Wanabodi

Samahani. Naomba kuanza na kuomba msamaha kwa kutumia maneno ambayo sio ya lugha ya Kiswahili wala lugha ya Kiingereza bali ni maneno ya lugha ya Kilatini kwasababu sikijui Kiswahili chake, wala Kiingereza chake, ni maneno ambayo yanafundishwa hivyo hivyo.

Imani Kubwa na Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma.

Japo mimi ni mwandishi tu wa habari, lakini pia nimetoa tongotongo za sheria pale UDSM, kitivo cha Sheria ya enzi zile ikiitwa Faculty of Law (FoL), sasa ni School of Law. Enzi hizo, Jaji Mkuu wa sasa Prof. Ibrahim Juma, enzi hizo akiwa ni Dr, kabla hajaukwaa uprofesa, alikuwa ni mmoja wa waalimu wangu, na pia alikuwa Dean wangu. Waalimu wengine ni Prof. Palamagamba Kabudi alikuwa supervisor wangu wa LL.B dissertation, Dr. Tulia Akson, Dr. Harrison Mwakyembe, Dr. Sifuni Mchome, Prof. Florence Luoga wengine wengi ambao walikuwa waalimu wetu pale sasa wako serikalini. Mwalimu niliyetokea kumpenda sana ni Prof. Issa Shivji, na hivyo kujikuta somo lake nikapiga A, na kuna Mwalimu sikumpenda na sijui alijua, somo lake nikapigwa F, ilivyo pelekea ku DISCO kwa technical DISCO.

Waalimu wa chuo kikuu sio malaika ni binaadamu kama binaadamu wengine hivyo nao wana madhaifu yao. Moja ya madhaifu makubwa ya wanasheria ni pamoja na kujisikia wao ndio wasomi saana, wanajisikia sana, wanaongea vingereza vigumu, bombastics kibao na maneo kibao ya Kilatini. Hivyo mwalimu somo lake nusu ya darasa wakipiga supp, ndio anafurahi heshima adabu!.

Prof. Juma was different just like Shivji, Chris Peter, Kanywani, Mgongo Fimbo na wengine, alikuwa very humble. Uadilifu wake nilikuja kuujua wakati hilo DISCO langu lilipotua mezani kwake yeye akiwa Dean. It is expected yeye as Mwalimu angesimama na Mwalimu mwenzake aliyenitundika DISCO, lakini huyu ni mtu wa haki bin haki, akanisikiliza hoja zangu, akaitisha mtihani wangu, akakuta hilo somo lenye F, nilikuwa na B+ akasimamia ikarudishwa DISCO likafutika.

Hiyo uadilifu wa Prof. Ibrahim Juma katika utendaji haki sio wa mashaka wala wa kuhadithiwa; huyu ni mtenda haki kwa mawazo, maneno na matendo.

Hivyo mtenda haki huyu, sasa ndiye Jaji wetu Mkuu, hivyo hili ni bandiko la kumuomba Prof. Ibrahim Juma, kwa vile yeye ni mtenda haki, na sasa ndiye Jaji Mkuu wa Tanzania, aweke historia mpya ya haki Tanzania, kwa Mhimili wa Mahakama ya Tanzania kutimiza wajibu wake sio tu wa kutoa haki, bali kulinda haki za Watanzania zilizotolewa na Katiba ya JMT, lakini serikali ya JMT ikazipora kwa kuibadili katiba na kunyanganya haki hizo.

Zaidi ya jukukumu la kutoa haki, pia Mahakama kama Mhimili ina jukumu la kufanya checks and balance kati ya Mhimili wa Bunge usijiinue zaidi kuliko mamlaka yake na Mhimili wa serikali usijiinue zaidi kuliko mamlaka yake hivyo kuminya haki zilizotewa na katiba ya JMT.

Kikawaida mahakama hata kama inaona jambo fulani linafanywa na serikali lakini linakwenda kinyume cha haki, haiwezi kujiamulia tuu kuingilia hadi kutokee mtu au Taasisi ifungue shauri ndipo mahakama isikilize na kulitolea maamuzi.

Kuna mambo mengi makubwa ya uvunjaji wa Katiba ya JMT unaofanywa na viongozi wa serikali ya JMT, lakini kwa vile hakuna anayelalamika, mahakama nayo inaangalia tu.

Kuna uvunjaji mkubwa wa haki za binaadam kwa kesi kuchukua muda mrefu bila kukamilika kwa uchunguzi. Mfano mzuri ni ile kesi ya yule wakili wa Arusha aliyekaa mahabusu kwa miaka 7, kwa kesi ambayo ukikutwa na hatia kifungo chake ni kisichozidi mwaka mmoja. Hapa tunapozungumza kuna watu wako mahabusu tangu Rais Magufuli ameingia madarakani hadi leo hazijasikilizwa na watuhumiwa wako mahabusu.

Sasa ufike wakati Jaji Mkuu kuitumia mamlaka yake ya Mahakama kama Mhimili wa kutoa haki, itimize wajibu wake wa kulinda haki za kikatiba kwa kutumia kanuni ya Suo Moto ambapo mahakama yeye yenyewe inapoona haki za kikatiba zimevunjwa na wakuu wa mihimili ya Bunge ya Serikali, inajifungia ndani na kutoa prerogative order hivyo kui-check serikali kwa mahakama kutimiza its role of checks and balance.

Amri za kuzuia mikutano ya siasa, kuruhusu wagombea binafsi, Tume ya Uchaguzi ambayo sio inclusive, DPP kufanya upelelezi kwa miaka na miaka, camera kuingizwa mahakama, watu kubambikiwa kesi sizizo na dhamana, fumueni sheria zote hizi kandamizi. Kesi pekee ambazo hazitakuwa na dhamana zibaki treason na 1st degree murder.

Pia kufuatia baadhi ya watendaji wa serikali haswa ma-RC na ma-DC na watu wengine vicha vichaa, media, kujiinua sana kunyanyasa raia na kutoa kauli mbofu mbofu kwa kuropokaropoka maneno ya ajabu ajabu kuchafua watu zinazokwenda kinyume cha haki za binaadam ikiwemo kutukana watu, kukiuka right to privacy za watu, kukiuka right to privacy za wagonjwa.

Kwa bahati mbaya sana, kwanza sio Watanzania wengi wana uelewa wa sheria kujua kuwa wanakashifiwa, hivyo vichaa waropokaji na wapayukaji wanajipayukia tu kwasababu wanajua hao wanaowapayukia hawawezi kwenda popote.

Pili kuna wanaokashifiwa ambao wanajua wamekashifiwa, lakini wanaamua kuacha tu kwa makusudi kwasababu wanajua kashfa hizo zina baraka za Serikali. Mfano mzuri issue ya makada wa CCM -- Kinana, Membe na Makamba -- kukashifiwa na kichaa mmoja, na baada ya kuandika barua kwenye chama kulalamikia udhalilishaji huo, wakageuziwa kibao kwa kusambazwa voice notes za sauti zao, kitu ambacho ni uliukwaji mkubwa wa rights to privacy.

Tatu kuna wanaojua wanakashifiwa, lakini kujikuta hawa uwezo wa nguvu ya kiuchumi kuajijiri wakili kuwafungulia shauri. Kila siku tunashuhudia media trials kwa washitakiwa kupigwa picha hadi wakiwa mikononi mwa polisi hadi ndani ya vyumba vya mahakama.

Kwa vile sasa Tanzania tuna mawakili wengi wa kutosha, huu ni wakati tunaomba turuhusu sheria ya Pro Bono. Mtu akikashifiwa, mwanasheria unajitolea kumtetea bure, akishinda kesi ndio anakulipa gharama zako.

Kama serikali imeruhusu plea bargain, inashindwa vipi kuruhusu Pro Bono?

Kama tungekuwa na sheria ya Pro Bono viongozi kama hawa wasingekuwa na uwezo wa kuropoka mambo kama haya.

Hitimisho:
Jaji Mkuu Prof Ibrahim Juma, baada ya tuhuma za the Legislature kuji-submit kwa the Executive, nina imani kubwa na wewe ukiamua, unaweza hivyo nakuomba CJ Prof. Ibrahim Juma, make a historia kwa mahakama zetu kutimiza wajibu wake kulinda haki za kikatiba kwa kutumia Suo Moto KuiCheck Serikali na pia its high time Tanzania turuhusu Pro Bono.

Wako wanafunzi mtiifu,

Paskali

Pro Bono - huduma ya kisheria bila tozo.
 
Back
Top Bottom