ngozimbili
JF-Expert Member
- Jul 28, 2011
- 1,398
- 1,006
Hili la Mashinji limewaweka pagumu sana watesi wa Cdm,na limechangia kupunguza majanga Cdm,ukichangnya na Msigwa tumeokoa milioni kama 80 hiviWanabodi,
Hukumu ya Mahakama ya Kisutu dhidi ya viongozi wa Chadema imeibua mengi, yakiwemo mabaya miongoni mwake ni waliofyatua risasi kumuua Aquiline hawakushitakiwa, wajashitakiwa walioandamana huku wameshikana mikono kuonyesha solidarity, wakahukumiwa vifungo vya jela na hapo hapo kupewa option ya kuinunua haki ya uhuru wao kwa fedha TZS milioni 350, hivyo Tanzania ya leo, justice is for sale, ukiwa na fedha inainunua haki yako, unaununua uhuru wako, unaepuka kifungo cha jela, ukiwa ni kapuku mwenzangu na mimi, unaozea Segerea.
Hukumu ile kucheleweshwa na kusomwa jioni baada ya kuisha kwa muda wa saa za kazi ili viongozi hao, angalau waonje jela, na kufanyiwa udhalilishaji wa hali ya juu baada tuu ya kutua gereza la Segerea, wengi wa watu wanaijadili hukumu hiyo kwa ubaya na kuusahau wema.
Wengi wanailaani tuu hukumu ile bila ya kuangazia mema na mazuri ya hukumu ile, kama ilivyo enzi za Masiya, kati ya wale watumishi wake thenashara, kulikuwa na Yuda wawili. Kulikuwa na Yuda Iskariote na Yuda Tadei. Kutokana na usaliti wa Yuda Iskariote, likitajwa tuu jina la Yuda watu wanalihusisha na usaliti, hivyo mazuri yote ya Yuda Tadei, yalifunikwa na mabaya ya Yuda Eskarioti, vivyo hivyo hii kesi ya viongozi wa Chadema ilikuwa ni kesi mbaya, hukumu ile na yatokanayo pia ina mazuri yake yaliyofunikwa na mabaya, hivyo hili ni bandiko la kutoa wito kwa Chadema, wawe na shukrani kwa yote, mazuri na mabaya, kuna majanga mengine yanakuja kama majanga kumbe ni neema, blessing in disguise.
Sisi Wakristu tumefundishwa kuwa na shukrani kwa yote. Hivyo katika kesi na matokeo yake, licha ya mabaya yote yanayopaswa kulaaniniwa, pia kuna makubwa, mazuri ya kuonekanika ambayo Chadema kama ni watu wa shukrani, wanapaswa kushukuru kwa hayo, na ukiwa na shukrani kwa madogo, unabarikiwa kwa kupatiwa makubwa.
Hivyo ndungu zangu wa Chadema, rafiki zangu, jamaa zangu na machalii wangu,
Chadema, kuweni ni watu wa shukrani. Shukuruni kwa yote,
Shukuruni kwa makubwa,
Shukuruni kwa madogo,
Shukurini kwa mema,
Shukuruni kwa mabaya,
Shukuruni hata na kwa mateso mliyoyaoata gerezani kama Paulo na Sila,
Shukurini hata kwa mateso yote vyama vya upinzani wa kweli vinayoyapitia Tanzania, kwa sababu yote ni mapito tuu, maana hata Masiya, ni kwa kupigwa kwake, kwa kuteswa kwake sisi tuliponywa, hivyo inawezekana kabisa kwenu wana Chadema, ni kwa kuteswa kwenu, upinzani utaponywa. Ni kwa kuteswa kwenu Tanzania itaponywa, kuweni na shukrani kwa madogo ili mjaaliwe makubwa.
Ile kesi yenu ni kesi mbaya kwasababu ni kesi ya kubambikizwa. Risasi wafyatue wengine, kuua waue wengine, lakini kushitakiwa washitakiwe wengine, huku ni kubambikiza kesi.
Kesi yoyote ya kubambikizwa lazima inakuwa na nia mbaya hivyo ile kesi ilikuwa ni kesi mbaya!, hivyo Chadema ishukuruni mahakama, mshukuruni Mashinji, ishukuruni CCM kuwasaidia kulipa baadhi ya faini, mshukuruni JPM kuwasaidia kuwalipia baadhi ya watu wenu, na mwisho washukuruni Watanzania waliosimama bega kwa bega na nyinyi tangu mwanzo wa kesi hadi mwisho na kuwaokoa kwa michango yao ya hali na mali, sala, machozi, jasho na damu, semeni asante, shukuruni kwa yote.
Kwa wale wavivu wa kusoma makala ndefu, ishieni hapa, sisi wazama deep tutaendelea, kwanini Chadema iishukuru Mahakama, Mashinji, CCM, JPM na Watanzania...
Hitimisho.
- Chadema wawashukuru Watanzania wote kwa kuungana nao, kuwachangia, hiyo pia imewasaidia kuwapa kipimo cha Chadema inakubalika vipi kwa Watanzania, hivyo what Chadema needs now is getting organised and how to utilise the approval rate they enjoy now to its advantage running up to 2020 general election. Siku zote Chadema imekuwa ikiamimi adui yao mkubwa anayewakosesha kuingia ikulu ni CCM kwa kusaidiwa na vyombo vyake vya dola kuanzia serikali, NEC, polisi, na nguvu za dola, mimi siku zote nawawaambia adui yao mkubwa anayewakosesha kuingia ikulu, sio wale wapiga kura milioni 6 wa CCM na zile kura milioni 2 za NEC, adui mkubwa wa Chadema ni wale wapiga kura milioni 20 ambao hawajajiandikisha, na wale milioni 12 waliojiandikisha lakini hawakujitokeza kupiga kura. Hivyo sasa Chadema should invest in people, mass mobilization na sio kila siku kutwa kucha kulalamika tuu inaonewa na CCM.
- Chadema iwashukuru Maalim Seif, Mbatia, Zitto na wapinzani wengine waliosimama nao na kuwaunga mkono, kesi hii na hukumu hii japo ilidhamiriwa kuleta majanga kwa Chadema, imekuwa the other way round, it's a blessing in disguise kwa kutengeneza solidarity mpya kuireplace UKAWA, Chadema ikubali kushirikiana kuunda umoja wenye nguvu, Chadema yenyewe peke yake haiwezi, they have to sort out their differences and work together agains a common enemey kwa kuutumia uzoefu wa UKAWA 2015 kutorudia makosa kwa wapinzani kupigana vita vya panzi kugombea majimbo huku kunguru amesimama pembeni mwisho wa siku walimfaidisha kunguru.
- Chadema iishukuru sana hii kesi, na hii hukumu, imeweza kuwapa picha ya nani ni nani, ndani ya Chadema, sasa angalau wanajua ndani ya msafara wao wa mamba nani ni ma kenge wanaosubiri tuu Bunge livunjwe, wakaripoti upande wapili.
- Last but not least, Chadema waushukuru huu mtandao wa Jamiiforums na mitandao mingine and never to underestimate the powers of social media, hivyo wanapaswa kutushukuru hata watu kama sisi ambao we don't spare the rod and spoil the child kwa kutembezea kichapo bila huruma, ushauri kama huuungetoka kwa consultant wangelipa fedha nyingi, Chadema isiwachukie watu kama sisi tunao ikosoa, unaweza kukuta sisi tunao ikosoa Chadema humu mitandaoni, tunaisaidia kuliko wale wanao isifu.
Chadema inapokesea usiojisikie wazito kuomba samahani, mnapokumbana na jambo lolote liwe zuri au baya, shukuruni tuu Mungu kwa yote na semeni asante kwa kila kitu. Mtu akikupiga shavu la kushoto, mgeuzie na la kuume, mtu akikunyanganya kofia yako au koti, mvulie na kanzu yako, mnayetende hayo yote ili anayewapigania msiwe ni nyinyi ndio mnaojipigania, bali myaweze yote katika YEYE.
Nawatakia Jumamosi Njema,
Kwa wale Wakiristu, kesho nendeni Kanisani mkatoe shukrani zenu kwa Mungu aliyewezesha haya yote.
Paskali