Wito: Chadema, CCM na Wote Maslahi ya Taifa Yazingatiwe

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
12,454
2,000
Itakuwa kutojitendea haki kutokutambua kuwa taifa hili linapita katika hali iliyo tete sana. Hali kadhalika itakuwa ni kukosa uzalendo kwa kiwango cha juu kuyaona haya na kuyafumbia macho.

Pamoja na yote ni muhimu sana maslahi ya taifa yakawekwa mbele.

Ieleweke kuwa maslahi ya taifa (kama ilivyo kwa wajibu wa kuyalinda), si ya watawala, serikali, Polisi wala taasisi yoyote iwayo yote hapa nchini. Msingi mkuu wa maslahi ya taifa ni uhai na maisha ya mtu mmoja mmoja katika taifa, pasipokuwa na ubaguzi wowote.

Hayupo anayaweza kujimilikisha wajibu wa kuulinda msingi huu mkuu wa maslahi ya taifa. Wajibu wa kuyalinda maslahi ya taifa ni wetu sote. Hayupo aliye bora, mwenye uchungu au dhamana zaidi kuliko mwingine.

Yaliyo mazito zaidi kutufikisha kwenye hali tete hii tulimo, ni haya hapa:

(a) janga la Corona linaloendelea kutupukutisha kweli kweli,
(b) fukuto lililowiva la kudai katiba mpya.

1. Janga la Corona:

Tunapita katika wakati mgumu sana na gonjwa hili. Kama alivyosema kwa usahihi kabisa SSH:

"ugonjwa huu unatupukutisha vilivyo na anayebeza madhara ya ugonjwa huu ni vile atakuwa hajaguswa tu."

Tusiwape nafasi wanaobeza uwepo wa ugonjwa huu, tahadhari na jitihada za kitalaamu kwenye kupambana nao kwa sababu zao zozote zile.

2. Fukuto la katiba mpya:

Hili limekolezwa zaidi na kukamatwa kwa mheshimiwa Mbowe. Itakuwa ni kujidanganya kwingi kudhani kuwa sababu zilizotolewa za kukamatwa kwake zimekubalika au hata kuaminika.

Siyo siri kuwa kuna tashwishi za ukiukwaji mkubwa wa haki kwenye kadhia unaoonekana machoni pa wengine. Kwamba serikali au taasisi zake zinaendelea kubambikizia watu kesi kama ilivyodhihirika pasipo na shaka kwa awamu ile, basi tungali tunakoelekea si kwema.

Kwa hakika busara isipotamalaki mapema ni wazi kuwa tunakoelekea kitaumana na hatuko mbali sana kutokea huko.

#1, Chonde chonde wadau, hili lisigubikwe na harakati za #2. Hadi hapa wadau nisiache kutoa pongezi: "hongereni sana kwa kuweza kuwahimili wajumbe wenu kuwa na subira na ustahamilivu katika mazingira magumu."

Katika hali zote kuliweka #1 kuwa ni kipaumbele na hasa katika kuwapa nafasi watu wanaohitaji kupokea chanjo bila ya kutatizika, ni jambo lenye thwawabu kubwa.

Kwa hili kwa hakika hadi hapa tulipo, kongole kwenu sana wadau. Siyo siri mnatutoa kimasomaso.

#2, Chonde chonde serikali, hili lisiwe sababu ya kutufarakanisha na kuweka #1 hatarini na hata amani yetu rehani. Ni muhimu kupima faida za kumshikilia mheshimiwa Mbowe kwa sababu zisizoaminika dhidi ya kuchagua njia ya mazungumzo ambayo aghalabu ni salama zaidi na kwa manufaa yetu sote.

Kuna haja gani ya kutiana majaribuni? Au kuna haja gani kuruhusu uwezekano wa shari wakati pana njia bora zaidi zenye uwezo wa kupisha shari?

Waliosema, "majuto ni mjukuu na wengine wakasema "mzaha mzaha hutumbua usaha" walikuwa na uzoefu wa kuyaona mengi.

Eeh mola wetu ukawanyooshee vidole vyako vya maonyo mskali wote wanaonoa silaha na kupania ala zao ili kuyahatarisha maisha ya watu wako kwa ubinafsi wao.

Eeh mola wetu ukajidhihirishe kwao kuwa wewe ndiye uliye mkuu na hayupo Mungu kama wewe.

Kwako baba utupokee.

Ninawasilisha!
 

Kamanda Asiyechoka

JF-Expert Member
Sep 13, 2020
1,256
2,000
Itakuwa kutojitendea haki kutokutambua kuwa taifa hili linapita katika hali iliyo tete. Itakuwa ni kukosa uzalendo kuyaona haya na kuyafanyia macho.

Pamoja na yote ni muhimu sana maslahi ya taifa yakawekwa mbele.

Ieleweke kuwa maslahi ya taifa (kama ilivyo kwa wajibu wa kuyalinda), si ya watawala, serikali, Polisi wala taasisi yoyote iwayo yote hapa nchini. Msingi mkuu wa maslahi ya taifa ni uhai na maisha ya mtu mmoja mmoja katika taifa, pasipo na ubaguzi wowote.

Hayupo anayaweza kujimilikisha wajibu wa kuulinda msingi huu wa maslahi ya taifa. Wajibu wa kuyalinda maslahi ya taifa letu ni wetu sote. Hayupi aliye bora, uchungu au dhamana zaidi kuliko mwingine.

Yaliyo mazito zaidi kutufikisha kwenye hali tete hii tulimo yenye kuhatarisha maslahi yetu kama taifa ni:

(a) janga la Corona linaloendelea kutupukutisha kweli kweli,
(b) fukuto lililowiva la kudai katiba mpya.

1. Janga la Corona:

Tunapita katika wakati mgumu sana na ugonjwa huu. Kama alivyosema SSH, ugonjwa huu unatupukutisha vilivyo na kuwa anayebeza madhara ya ugonjwa huu ni vile hajaguswa tu.

Tusiwape nafasi wanaobeza uwepo wa ugonjwa huu, tahadhari na jitihada za kitalaamu kwenye kupambana nao kwa sababu zozote zile.

2. Fukuto la katiba mpya:

Hili limekolezwa zaidi na kukamatwa kwa mheshimiwa Mbowe. Itakuwa ni kujidanganya kwingi kudhani kuwa sababu zilizotolewa za kukamatwa kwake zimekubalika au hata kuaminika.

Siyo siri kuwa kwa tashwishi za ukiukwaji huu wa haki unaoonekana machoni pa wengine, tunakoelekea si kwema. Busara isipotamalaki ni wazi kuwa kitaumana.

#1, Chonde chonde wadau, hili lisigubikwe na harakati za #2. Hadi hapa wadau hongereni sana kwa kuwahimili wajumbe wenu.

Katika hali zote kuliwekea #1 kuwa ni kipaumbele na hasa kuwapa nafasi watu kupokea chanjo bila ya kutatizika, ni jambo lenye thwawabu kubwa.

Kwa hili hadi hapa tulipo, kongole kwenu sana tu wadau.

#2, Chonde chonde serikali, hili lisiwe sababu ya kutufarakanisha na hata kuweka #1 hatarini. Pimeni faida za kumshikilia mheshimiwa Mbowe kwa sababu zisizoaminika dhidi ya kuchagua njia ya salama ya mazungumzo.

Kuna haja gani ya kutiana majaribuni?

Mzaha mzaha hutumbua usaha.

Eeh mola wetu ukawanyooshee vidole vyako vya onyo wote wanaonoa silaha zao na kujipanga kuyahatarisha maslahi ya watu wako katika nchi yao kwa ubinafsi wao.

Ninawasilisha!
Unawasilisha pumba tupu. Kukamatwa Mbowe ndio iwe sababu?
 

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
12,454
2,000
Chonde chonde waungwana. Huku tunakokwenda isije tukaja kupiga U-turn kama Corona baadaye mno wakati madhara ni makubwa zaidi:


Wako wapi wazee wa busara? Wako wapi kina Kikwette? Wako wapi na kina Warioba? Wako wapi kina Butiku?

Ziko wapi madhehebu za dini, ziko wapi AZAKI?

Tusije sema hatukujua.

Angalizo mantashari: Kupigania haki hakujawahi kuwa in vain.

Cc: BAK
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom