WITO: Bi Sophia Simba Jiuzulu

Status
Not open for further replies.
Ndugu wanabodi,

Waziri Sofia Simba anashika wadhifa mkubwa sana kwenye serikali ya awamu ya nne, kwani wizara yake ndio kioo cha viongozi wote yaani Utawala bora. Wizara hii ndio inayongalia mienendo na maadili ya viongozi wote wa umma. Inakemea ukiukwaji wote wa haki za watumishi wa umma.

Je Sofia Simba anastahili tena kuiongoza wizara hii???????

Je kupigana hadharani na kiongozi mwenzako ni maadili ya uongozi????

Je kujichukulia sheria mkononi ni utawala boraa??????

Kutoa kauli chafu mbele ya hadhara tena kumtukana mtu aliyekuzidi umri ndio maadili ya mwanamke wa kitanzania?????????

Kutokupeleka malalamiko yako kwenye mamlaka husika kabla ya kujichukulia sheria mkononi ndio maadili ya utawala bora?????

Hayo pamoja na mengine mengi uliyoyafanya HUSTAHILI TENA KUWA KIONGOZI WA HIYO WIZARA WALA UONGOZI WOWOTE WA UMMA

Bi Sofia Simba JIUUUZULU, JUIZULU JIUZULU

SIoni sababu ya kumtaka Sofia Simba kujiuzulu. msipende kuangalia upande mmoja kwani huyo Mama Kahama ni mkorofi sana na anapenda vimaneno neno. Nia yake ni kumchafua tu mwenzake ili yeye aonekane mtu mzuri.

We kama umetumwa na mama Kahama basi pole yako.
 
HII NDIO SIASA YA TANZANIA, SASA HATA STORI HII IKO FRONT PAGE INASIKITISHA INGAWAJE INA UKWELI ,WHAT A KOINSDENSI?!!!!!!

Date::9/16/2008
Simba alining'ang'ania koromeo siamini kama niko hai





Baadhi ya wakazi wa Chanika Zingiziwa, Dar es Salaam, wakiwa na mzoga wa simba aliyeuawa baada ya kumshambulia mkazi wa kijiji hicho, Hamis Mgagara Jumapili iliyopita.
Na Martha Ndeki

HAMIS Mgagara (40) mkazi wa Chanika Zingiziwa, mkoa wa Dar es Salaam, bado hajaamini kilichotokea baada ya kuokoka kutoka katika mdomo wa simba jike ambaye tayari alikuwa amemkaba koo kwa kutumia makucha.


Kisa hicho cha kutisha kilitokea majuzi kijijini Zingiziwa, baada ya mkulima huyo kushitushwa na kelele za mbwa waliokuwa wakibweka karibuni na kichuguu katika eneo la shamba lake hapo kijiji majira ya asubuhi.


"Kama si wanangu, Saleh Hamis na Said Hamis na mpwa wangu Seifu Chamwande kuninasua mdomoni mwa simba ningekuwa nimebaki jina," alisimulia Mgagara kwa shida ambaye amelazwa Wadi ya Sewa Haji wodi 29, Hospitali ya Taifa Muhimbili,


"Niliposogea tu, simba huyo ambaye alioneka kama mwenye mimba alinirukia shingoni na kuniangusha chali, akazamisha kucha zake kwenye koromeo, nikapiga kelele kuomba msaada kwa majirani na familia yangu," anasimulia huku akiwa amefungwa bandeji kichwani na mikononi.


Anasema baada ya kelele za kuomba msaada, watoto wake wawili, Saleh na Said na baadaye mpwa wake Seifu walikuwa wa kwanza kujitokeza kutoa msaada na hapo ndipo mapambano na simba huyo mwenye hasira yakaanza.


"Mwanangu Saleh alipoona simba ameng'ang'ania koromeo langu alimkabakabali simba ili niweze kujinasua. Katika harakati hizo simba aliweza kuninyofoa kidole cha pili kutoka kidole gumba mkono wa kushoto na kuvunja mfupa wa kidole cha kati,"anasimulia huku uso wake ukionyesha maumivu makali.


Baada ya Saleh kumkaba kabali mpwa wake Seifu aliyekuwa na jembe alitumia mwanya huo kumlima simba kichwani hadi kuniachia na kumvamia Seif miguni kwa kulipiza kisasi kutokana na hasira ya kulimwa na jembe kichwani.


"Nami pia nilitumia mwanya huo kunyanyuka na kuendelea na mapambano na simba kwa kumpiga kwa jembe na panga hadi akaishiwa nguvu na kufikia hatua hiyo wanakijiji waliowahi kufika eneo la tukio waliendeleza mapambano hadi kummalizia, sisi tukiwa tayari tumechoka".


Baada ya mapambano hayo yasiyo ya kawaida, wanae walipata walipata matibabu na katika Hospitali ya Aman, Ilala, Jijini na kuruhusiwa kwenda nyumbani baada ya kuonekana kuwa hawakuwa na majereha mabaya kama aliyopata yeye, anasema.


Pamoja na majeraha ya koromea na mikono anasema anajisikia maumivu makali ya kucha za simba katika eneo la mashavu hali inayomfanya kuzungumza kwa.


Hata hivyo majeruhi huyo mwenye bahati ya kuokoka kifo anasema anawashukuru waganga pamoja na wahudumu wa Muhimbili kwani wamempokelea vizuri na kuwa amepatiwa matibabu yanayompa imani ya kupona haraka.


Afisa uhusiano wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Jezza Waziri, anasema majeruhi walifikishwa hapo katika hali mbaya kwa kuvuja damu kwa wingi kutokana na majeraha makubwa lakini hali yake ilikuwa inaendelea vizuri tofauti na juzi.
 

Hii habari mbona siielewi? Nini hasa kilichotokea? Walipigana au Sofia ndiye aliyempiga mwenzie? Tunaposema hadharani tuna maana gani? Nilidhani haya yalitokea kwenye kikao cha ndani na si kwenye public forum? Hiyo kauli chafu ilitokana na nini? Na ni nini hasa kilisemwa?

Ha ha haaaaa. Inabidi ufanye extracurricular independent study kujua kilichojiri kwenye tukio lolote Bongo.


SOPHIA SIMBA


``Kikao chetu kilikuwa cha siri, wewe habari hizo umezipata wapi? Mimi ni kiongozi makini, najua ninachokifanya, siwezi kutoa siri ya kikao, labda umfuate huyo aliyekuambia,``

``Wewe sijui leo ni mtu wa ngapi kunipigia simu, watu wengi wamenipigia eti wanauliza kulikuwa na masumbwi kati yangu na Janeth. Sasa kwa nini mnaniuliza, huyo aliyeamua kuvujisha siri za kikao basi na awamalizie kilichoendelea,``

``Kama anakwenda kushitaki anayo haki ya kufanya hivyo, akashitaki tu,``

``Namimi pia nina malalamiko kwake, mengi sana tena mazito, hata mimi nitamshitaki,``

JANETH KAHAMA, Mwenyekiti UWT, Mkoa


``Alitaka kunidhuru, nilikuwa katika wakati mgumu, maana hata wanaume na nguvu zao walipomshika asije kuniumiza, bado aliwasukumiza,``

``Katika hali hiyo huwezi kukumbuka jina wala sura ya mtu, nilichokumbuka mimi ni msalaba,`` alisema alipoulizwa kama anawakumbuka wajumbe waliomuokoa...alichokumbuka ni kukimbilia msalabani na kufanya maombi na kukemea roho ya ugomvi.

``Bi. Sofia ni kiongozi mkubwa sana na tunamheshimu, hivyo suala hili (la kudaiwa kupigwa naye) sijaenda kuliripoti polisi, bali nimeufikisha ugomvi huo katika vikao vya chama changu kwa kufuata taratibu na kanuni zilizopo... ninaamini huko kutatolewa maamuzi sahihi,``

``Nampenda sana Sophia, sina kinyongo naye,``

``Siwezi kumlaumu wala kusema barabarani kama alivyosema, mimi nitamfikisha kwenye vikao vya maadili, ndivyo taratibu zetu zinavyosema,``

``CCM hakuna jela, kwamba nikimpeleka huko atafungwa, lengo nikuhakikisha anapata nafasi ya kutoa madai yake,`` alisema. Hata hivyo, alikana kumhujumu Sophia kwa kutomwalika kwenye vikao vya UWT kama ilivyodaiwa.

WAJUMBE WALIOSHUHUDIA NA WAPAMBE WENGINE WENGINE

Anna Abdallah, Mwenyekiti UWT, Taifa
``Kwanza mimi siko Dar es Salaam, niko Dodoma, lakini pia si mjumbe wa kikao hicho. Hayo mambo yetu ya kuokoteza mitaani, msiniulize mimi,…‘Ninachojua, kesho tuna kikao cha Baraza Kuu, lakini habari ya nani na nani wamegombana, sitaki kuyajibu,``

John Guninita (Mwenyekiti wa CCM, Mkoa)
``Unajua Waziri Simba alitoa malalamiko yake kwangu wakati mkutano wetu tayari ukiwa umemalizika, hapakuwa na ugomvi mkubwa kama unavyouliza, bali Mwenyekiti wa UWT Mkoa (Kahama) alikuwa akijaribu kutoa ufafanuzi,``

Jina Limehifadhiwa na Chanzo Chetu (Mwenyekiti na Katibu wa Taifa, Chama cha Wadaku wasiojulikana!)
``Usifikiri uwaziri wako na kupata ofisi pale Ikulu vitakusaidia, huu ni uchaguzi wa Chama, heshimu taratibu za chama,`` chanzo chetu kilimnukuu Kahama.

``Wakati Waziri Simba akiendelea kusema, Mama Kahama alisimama na kuanza kusema: ‘Sijakutukana, sijakutukana, hizi nafasi ni za Mungu, kwanini tuvunjiane heshima,`` alisema huku akisimama kuelekea alipokaa Mama Sofia.

``Kuona hivyo, wajumbe tuliamua kuingilia kati kwa kuwashika, huku wengine wakimsaidia Mama Kahama, kwani alikuwa amepandisha presha,``

Inasemekana habari ndio hiyo!
 
FM ES,

Naomba uje mkuu umchambue huyu mama. Tupeni wasifu wake huyu waziri.

Mkuu Fairplayer,

Heshima mbele sana, ni kwamba wote wawili ni washikaji wangu wa karibu sana, ndio maana nimekaa pembeni, ingawa ukweli ni kwamba Mama Janeti amekuwa kwenye kampeni kwa muda mrefu sana na anakubalika na wengi kumrithi anayeondoka,

Lakini Waziri Sophia, ameamua kutumia karata ya power na ukaribu na muungwana, maana huyu ni one of the most trusted soldier wa muungwana, kwa sababu at one time alikuwa mshikaji wa karibu sana na Mama Kilango, ndiye aliyewasiaidia sana Mtandao kumzidi kete Malecela, kwenye ule uchaguzi kwani aliwapa data zote kuwa jina la Malecela likiingia ndani ya NEC, they are done, kwa hiyo wakamzunguka kwa mstaafu wa uwt aliyekuwa close sana na Malecela, na hatimaye wakamkaba koo masikini ya Mungu Mkapa, Mtandao wakapita,

Mama Janeti, anajua kuwa sasa hapo ana wakati mgumu sana kushinda, maan you bet muungwana, atamsaidia Sophia, by any means necessary, na atashinda case close!

Hapa naona Mama Janeti anajaribu kutafuta sympathy ya public maana anajua kuwa uchaguzi umeshaisha tayari na ame-lost!
 
Mkuu Fairplayer,

Heshima mbele sana, ni kwamba wote wawili ni washikaji wangu wa karibu sana, ndio maana nimekaa pembeni, ingawa ukweli ni kwamba Mama Janeti amekuwa kwenye kampeni kwa muda mrefu sana na anakubalika na wengi kumrithi anayeondoka,

Lakini Waziri Sophia, ameamua kutumia karata ya power na ukaribu na muungwana, maana huyu ni one of the most trusted soldier wa muungwana, kwa sababu at one time alikuwa mshikaji wa karibu sana na Mama Kilango, ndiye aliyewasiaidia sana Mtandao kumzidi kete Malecela, kwenye ule uchaguzi kwani aliwapa data zote kuwa jina la Malecela likiingia ndani ya NEC, they are done, kwa hiyo wakamzunguka kwa mstaafu wa uwt aliyekuwa close sana na Malecela, na hatimaye wakamkaba koo masikini ya Mungu Mkapa, Mtandao wakapita,

Mama Janeti, anajua kuwa sasa hapo ana wakati mgumu sana kushinda, maan you bet muungwana, atamsaidia Sophia, by any means necessary, na atashinda case close!

Hapa naona Mama Janeti anajaribu kutafuta sympathy ya public maana anajua kuwa uchaguzi umeshaisha tayari na ame-lost!

Mkuu FME asante kwa data ila hapa unanitisha kidogo,

Mi nilidhani uchaguzi una amuliwa na kura kumbe niukaribu tu kwa mkulu??
Kwa mwendo huu twafa.. make hapo inabidi tukatafute kazi ya ukata manyasi kwa mahekalu ya mukulu ili walau tujisogeze karibu naye atukumbuke katika ufalme wake!
 
Naye mama kahama huu ni muda wake wa kukaa na kelea wajukuu wala sio kwenda kugombana na viruka njia.
 
hahahaha siku hizi siaza Tz fitna tupu..hata wasio uwezoo wanakuwa na kiburi....kisa sababu wako karibu na mkuu wa kaya...kazi ipo...ila wa tz tumezidi ujinga,uoga,kufuata mkumbo...,aama wote wanajuaa kuwa mtu fulani hana uwezo na wanacmahgua sababu nini....yuko karibu na Mwenyekiti shame on us....tubadilikee....jamanii au tunasubiria hadi wastaafu ndio tuanze kuwanyoshea vidole?
 
Naye mama kahama huu ni muda wake wa kukaa na kelea wajukuu wala sio kwenda kugombana na viruka njia.
 
Nina wasi wasi na FIRST LADY, mbona unaelekea kuwatetea sana akina mama wa CCM, jana nimemsikia kiongozi wao eti KAMA KUNA WANAOWATISHA WAAMBIAENI WAKAWATISHE WATOTO WAO NA WAUME ZAO.....
du nilishangaa kwa kicheko kuona kiongozim mzima anatoa vijembe vya taarabu. kumbe sio tu wanaume wa CCM ni vituko hata wake zao pia.

Si mi nakwambia the whole issue imekaa kimipasho mipasho tu, i duno wots wrong with us
 
Mwl Nyerere aliwahi kusema katika moja ya speech zake kuwa "kiongozi huwezi kuishi kihuni huni tu"....Naona siku hizi hawa mawaziri wa JK adabu zero kabisa.......Namshauri hata Mama kahama akaripoti polisi kwa shambulio la aibu inaweza kuwa fundisho kwa wengine....Huyo Sophia Simba uswahili mwingi ndio tatizo.

ni kweli uswahili mwingi umemzidi kwasababu alimuinulia vidole juu mh zungu ina maana alikuwa kama vile anamsuta mh mbunge,
lkn jk mwenyewe atakuwa anamjua waziri wake nje ndani,na anajua mwenyewe alichomchagulia ,kwangu mie hafai hata udiwani
 
... ndiye aliyewasiaidia sana Mtandao kumzidi kete Malecela, kwenye ule uchaguzi kwani aliwapa data zote kuwa jina la Malecela likiingia ndani ya NEC, they are done, kwa hiyo wakamzunguka kwa mstaafu wa uwt aliyekuwa close sana na Malecela, na hatimaye wakamkaba koo masikini ya Mungu Mkapa, Mtandao wakapita,

Crock.

Eti Sofia Simba kawapa Mtandao data zote kwamba Malecela akiingia ndani ya NEC wamekwisha, halafu Mtandao wakakifanyia kazi hicho ki-data, wakashinda uchaguzi! Yani hizo data zako Mkuu unadhani watu wote ni wajinga kabisa kabisa kabisa ? Halafu watu wanakaa kusubiri - tena wanaomba - uwaletee data Mkuu. Yani Bongo masikini tuko nyuma kinoma katika mambo fulani. Duuh, inanisikitisha vibaya mno.

Naomba ujue kwamba kuna watu wanajua kwamba unayoyasema mengi ni habari za kuzalisha wewe mwenyewe.
 
Naye mama kahama huu ni muda wake wa kukaa na kelea wajukuu wala sio kwenda kugombana na viruka njia.[/QUOTE]

MAKUBWA HAYA! Nilidhani kugombea nafasi za uongozi ni haki ya kila mtanzania mwenye sifa zinazotakiwa.
Viruka njia ndo akina nani hapa?
 
hili jina UWT linapotosha!!! kwa hilo jina isingetakiwa iwe jumuiya ya CCM bali umoja wa wanawake kitaifa. chama kimoja kilileta matatizo mengi sana
 
Mkuu FME asante kwa data ila hapa unanitisha kidogo,

Mi nilidhani uchaguzi una amuliwa na kura kumbe niukaribu tu kwa mkulu??
Kwa mwendo huu twafa.. make hapo inabidi tukatafute kazi ya ukata manyasi kwa mahekalu ya mukulu ili walau tujisogeze karibu naye atukumbuke katika ufalme wake!

Rwabugiri!

Kura za siku hizi ni kutimiza wajibu tu kwa mujibu wa katiba. hata uchaguzi mkuu wa 2010 matokeo yake yapo tayari hadi asilimia wanasubiri utimiza wajibu tu wa sisi kutupotezea muda wa kupiga kura kabla hawajamtangaza mshindi wao.

lakini mwisho wao unakaribia
 
mnasahau mapema, huyu sophia simba, akiwa ni wziri wa utawala bora ndiye alisimama kwenye matanga ya ditopile mzuzuri akamsifia mkapa na kuponda magazeti yanayoandika ufisadi wa mkapa. sasa kama hawezi kuona ya mkapa , ataweza wapi kuwa na ustaarabu mnaoufikiri?
 
``Katika hali hiyo huwezi kukumbuka jina wala sura ya mtu, nilichokumbuka mimi ni msalaba,`` alisema alipoulizwa kama anawakumbuka wajumbe waliomuokoa...alichokumbuka ni kukimbilia msalabani na kufanya maombi na kukemea roho ya ugomvi.

``Bi. Sofia ni kiongozi mkubwa sana na tunamheshimu, hivyo suala hili (la kudaiwa kupigwa naye) sijaenda kuliripoti polisi, bali nimeufikisha ugomvi huo katika vikao vya chama changu kwa kufuata taratibu na kanuni zilizopo... ninaamini huko kutatolewa maamuzi sahihi,``

``Nampenda sana Sophia, sina kinyongo naye,``

Hii lugha ndiyo inazidi kunichanganya. Kumbe kwenye kikao palikuwa na msalaba! Kukemea roho ya ugomvi?

Ndiyo maana wenzetu hawatuamini!

Kwa nini wasimpelekee mwenyekiti wao na baraza lao? Naona spin doktaz wameishaingia.
 
This is not a way we should say, are we thinking something good can come out of that. Mashilingi when had that ministry aligombana na Mengi nothing happened. Philip Marimo akiwa wizara hiyo hiyo alishawahi kuliambia bunge kuwa riport ya TAKUKURU kuhusi Richamond ilikuwa safi but still now is still a minister under JKs leadership. To me wheather Mama Kahama or Sophia it doesnt matter, what I personally need is JK's ministers should get out of selfness, powermongaism, greedy and bear accountability of their deeds. I like CCM and thier laeders but I dont appreciate their doings and behavoiurs of some leaders like this of Simba. CCM should get to read signs of time. No evil will be covered under utandawazi.
 
Mama Sophia hana MORALS. Analeta ushangingi kwenye siasa. Alikuwa wapi siku zote kutolalamika kuwa hapewi taarifa za mikutano ya UWT. Ina kuwa issue kwa sababu kuna uchaguzi!
Angepeleka malalamiko yake in writing kwenye kamati husika.
Kwani ni nani aliyejiunganishia maji ya DAWASCO kule Mbezi kinyume ya utaratibu?
 
Hii lugha ndiyo inazidi kunichanganya. Kumbe kwenye kikao palikuwa na msalaba! Kukemea roho ya ugomvi?

Ndiyo maana wenzetu hawatuamini!

Kwa nini wasimpelekee mwenyekiti wao na baraza lao? Naona spin doktaz wameishaingia.

FM wenzenu kina nani wasiowaamini....
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom