"Wireless Power Cables"

Pazi na Jogoo

JF-Expert Member
Aug 12, 2016
331
494
Kuna mwama falsafa aliwahi kusema "Wazo bora ni lile unaloshindwa kulisema hadharani/wazi"

Naomba na mie niseme kwamba Technology si taaluma yangu ingawa kwa siku kadhaa nimekuwa nawaza juu ya jambo hili na sasa nataka kuliweka wazi ili wataalamu waone kama inawezekana.

Kwa kawaia tuna tumia power cable za umeme ambazo zina waya, wengine wanita Extensheni, ambazo zinachomekwa kwenye switch ukutani kisha ndipo unapata kuwasha Tv, Radio, Fridge, na vingine.

Sasa kwa kipindi hiki technology imekuwa sana, nikawaza kwamba kama saiv tuna LUKU, Dawasa nao nasikia maji unalipia kama luku unit ulizolipa zikiisha na maji hakuna pamoja na mambo mengine mbalimbal.

Sasa nikawaza kwamba wataalamu wetu kwenye vyuo vya ufundi kama DIT au Veta na shirika kama SIDO hawawezi kutengeneza au kuzalisha power cable ambazo ni wireless yaani inakuwa cable peke yake ambayo inakuwa na kitu kama Bloototh hivi ambayo hii pia inakuwa kwenye switch ukutani inamaana ukiweka inakuwa connected moja kwa moja kusafirisha umeme na tayari kwa matumizi,

Kuliko kuwana cables nyingi ambazo wakati mwingine zinapelekea kusababisha hutilafu ya umeme na kuleta madhara nyumbani.
 
Ni ngumu sana kufanya hcho kitu. Huawezi safirisha umeme kwa Bluetooth kwasabab hyo ni standard ya kusafirisha data. Kwa sasa tuna wireless chargers za simu zinazotumia induction kusafirisha umeme. Kuna kuwa na coil mbili za waya ambazo ikizisogeza karibu zinacharge simu (moja ipo kwenye charge nyingine ipo kwenye simu). Kusafirisha umeme mkubwa hvyo bila interference itakua ni shida kidogo. Ila akina Xiaomi na Motorola wanaoshughulikia technology ya long distance wireless charging ya mpaka 100cm kuendelea.

Hakuna kinachoshindikana tutafika tu huko siku moja, ila kwa technology ya sasa ya kutumia induction hicho kitu hakiwezekani bila kuhatarisha maisha ya watu. Hivi vitu ni lazima viwe vinazingatia afya za binadamu sio proof of concept tu.

Pia scientists Nikola Tesla around mwaka 1901 alikuwa idea hyo ila haikukamilika. Alikua ana idea ya kutumia vituo kusambaza umeme kutoka kituo kimoja kwenda kingine mpaka unapomfikia mtumiaji. Idea yake ilikua inalenga kuleta wireless electricity dunia nzima. Alianza na kitu kimoja cha experiment ambacho walikiiya Wardenclyffe Tower.
 
Mambo mengi yanaanza kwa wired lkn yanadevelop to wireless.
Tutafika tu. Hata maji itakuwa hakuna haja ya kuweka bomba. Just wireless
Miaka ya nyuma lazma tufuate mishahara halmashauri. Ila leo ....
 
Maji wireless?? upo sirias au unazingua? Halaf umeme wa wireless upo unatumika kwenye kuchaji baadhi ya simu ila ni mdogo na inabidi kifaa kuwa karibu sana, nguvu ya umeme wa nyumbani ni kubwa sana kuweza kusafirisha kwa wireless hata kama teknolojia itakua vp kuna vitu haviwezekani
 
Kuna mwama falsafa aliwahi kusema "Wazo bora ni lile unaloshindwa kulisema hadharani/wazi"

Naomba na mie niseme kwamba Technology si taaluma yangu ingawa kwa siku kadhaa nimekuwa nawaza juu ya jambo hili na sasa nataka kuliweka wazi ili wataalamu waone kama inawezekana.

Kwa kawaia tuna tumia power cable za umeme ambazo zina waya, wengine wanita Extensheni, ambazo zinachomekwa kwenye switch ukutani kisha ndipo unapata kuwasha Tv, Radio, Fridge, na vingine.

Sasa kwa kipindi hiki technology imekuwa sana, nikawaza kwamba kama saiv tuna LUKU, Dawasa nao nasikia maji unalipia kama luku unit ulizolipa zikiisha na maji hakuna pamoja na mambo mengine mbalimbal.

Sasa nikawaza kwamba wataalamu wetu kwenye vyuo vya ufundi kama DIT au Veta na shirika kama SIDO hawawezi kutengeneza au kuzalisha power cable ambazo ni wireless yaani inakuwa cable peke yake ambayo inakuwa na kitu kama Bloototh hivi ambayo hii pia inakuwa kwenye switch ukutani inamaana ukiweka inakuwa connected moja kwa moja kusafirisha umeme na tayari kwa matumizi,

Kuliko kuwana cables nyingi ambazo wakati mwingine zinapelekea kusababisha hutilafu ya umeme na kuleta madhara nyumbani.
Unamaanisha kusafirisha umeme upi.. yani umeme wa majumbani au?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom