Wino wa dhahabu:- Wasaidizi wa viongozi wetu wajifunze hapa

Tee Bag

JF-Expert Member
Dec 21, 2013
7,200
5,553
WINO WA DHAHABU:- WASAIDIZI WA VIONGOZI WETU WAJIFUNZE HAPA.

Na Thadei Ole Mushi.

Shida kubwa waliyonayo Viongozi wetu kwa Sasa ni kuongoza jamii yenye maarifa na Elimu kwa wingi.

Jamii aliyoongoza Nyerere si sawa na aliyoongoza Mwinyi. Jamii aliyoongoza Mwinyi si sawa na aliyoongoza Mkapa. Jamii aliyoongoza Mkapa si sawa na aliyoongoza JK na jamii aliyoongoza JK si sawa na anayoiongoza Rais Magufuli na jamii anayoiongoza Rais Magufuli itakuwa si sawa na itakayoongozwa na atakayemrithi. Huu ni ukweli na haitaji uwe na Elimu ya chuo kikuu kuuona ukweli huu.

TWENDE SAWA.

Imekuwa kawaida kabisa Sasa kiongozi anajifungia ndani anajiandaa haswa anatoka hadharani anaongea Jambo lake anaingia kwenye Gari yake kabla ya kufika nyumbani Jambo lile linachambuliwa na kuonekana kaongea kituko kabisa. Wasikasirike Bali wajifunze kuwa ni aina ya jamii waliyonayo kwa Sasa.

Kwa Sasa tuna wahitimu wengi haswa wa vyuo vikuu, na vyuo vya Kati wenye maarifa mbalimbali, Sasa hivi technolojia ya kupashana habari imekuwa, siku hizi watu wanajua haki yao ya kutoa maoni nk. Katika jamii Kama hii lazima Viongozi wetu wajiongeze na watafute maarifa mapya ya kukabiliana na jamii Kama hiyo.

Niliwahi kuwaandikia umuhimu wa hotuba za Viongozi wetu kuandaliwa kabla ya kuzisoma public. Nikiwasimulia kisa Cha Ghana na Marekani msaidizi wa Obama kwa kuandika haya nanukuu:-

"Kuna mtu anaitwa Nana Addo Dankwa Akufo-Addo huyu ni Rais wa Ghana. Ukimuuliza Leo mojawapo ya vitu ambavyo viliwahi kumkasirisha atakuambia ni January 7 mwaka 2017 siku aliyokuwa akiapishwa.

Siku hiyo mwandishi wa Hotuba zake bwana Eugene Arhin alifanya copy and paste ya hotuba ya Hotuba za marais wa Marekani Bill Clinton na Bush na kumpatia Rais ili akaisome kwa wananchi wa Ghana.

Hotuba hiyo ilisifiwa sana ila baada ya muda mfupi hata kabla ya Raisi kutoka kwenye Sherehe za kuapishwa watu walianza ukosoaji kitendo kilichomfanya Eugene Arhin kuomba msamaha kwa Rais na kwa wananchi wa Ghana. Ilikuwa aibu ya Mwaka ambayo Nana Akufo- Addo aliingia nayo Ikulu."

NATAKA KUSEMA NINI?

Nataka kusema kuwa Viongozi wetu wasaidiwe vyema katika maandalizi ya hotuba wanazokwenda kuzitoa kwenye majukwaa.

Kiongozi anaweza kukumbukwa kwa mambo makuu mawili moja speech zake au mambo aliyokuwa akiyafanya.

Ni Mara Chache sana kiongozi anaweza kuaandaa speech yake mwenyewe na kuitoa hadharani bila kupitia kwa mtu mwimgine kuihariri na kuifanyia marekebisho.

Mandela mpaka anakufa alitoa hotuba nyingi zenye msisimko lakini iliyovunja rekodi ni ile aliyoandaliwa na mhariri Nadine Gordimer akisaidiana na mwandishi Antony Sampson hotuba hii inaitwa "I am Prepared to die"

Wataalamu wa mambo wanasema hakuna speech ambayo imewahi kuvunja rekodi speech hii katika kusomwa na kutumika kama reference katika taifa la Afrika kusini.

Hapa kwetu Kuna Mama alikuwa akiitwa Joan Wicken huyu alikuwa ni raia wa uingereza ndiye alikuwa nyuma ya Speech za Baba Wa taifa Mwalimu Nyerere. Hotuba zote alizozitoa Nyerere njee ya nchi zilipitia kwa mama huyu Mwingereza aliyekuwa msaidizi wa mwalimu Nyerere.

Duniani kwa sasa Speech za Obama zinaendelea kuingiza mamilioni ya shilingi baada ya kuunganishwa kwa pamoja na kutengeneza kitabu. Piteni kwenye maduka ya kuuza vitabu mtaona

Sio Obama alikuwa akiandika hizi Speech Bali ni mtu aliyeitwa Jon Favreau ambaye Obama alianza naye pindi alipochaguliwa tu kuwa seneta na baadaye alihamia naye Ikulu. Obama alikuwa akimuita Favreau jina la utani "Mind Reader" kwa uwezo aliokuwa nao wa Kugundua nini Rais anataka kukisema na kukiweka kitaalamu ili kivutie watu na kifanye Clarification ya matatizo au Minongono ya wananchi.

January Makamba alijitutumua Kweli kuacha alama kwa Mzee Kikwete alikuwa anausoma mchezo, kwa vyama vya Siasa, Mitandaoni na kimataifa ndio anakaa anaandika speech ya Rais. Kwa kweli alijitahidi sana sintoshangaa Speech za Kikwete kuzikuta madukani, nimeshaona na kusoma kadhaa za Mzee Mkapa.

Pale Kenya Uhuru Kenyatta anao watu wawili Muhimu Sana mmoja anaitwa Eric Ng'eno na wa pili ni Denis Ithumbi. Eric Ng'eno yeye anahusika na kuandika Speech za Rais huku Denis yeye akiwa ni mzee wa media kwa ajili ya kuset Propaganda na kujibu propaganda zote zinazomhusu Rais.

Hawa ndio wanaompa Kenyatta Mvuto alionao Sasa. Kwa Nature ya wakenya ku win makabila yote Kama Kenyatta ni kazi kubwa Sana na kazi hii inafanywa na Hawa vijana wawili kwa ustadi mkubwa. Wanajua jamii inataka Nini na ipo katika Hali gani.

Viongozi wetu wafahamu kuwa wao ni zaidi ya watabibu speech zao zinaweza kutibu majeraha ya watu au kuwatonesha, au kuwagawa watu au kuwapa mfadhaiko watu. Lazima viongozi wetu kwa umuhimu wao wasaidiwe eneo hili la public speaking.

Speech zao ziache alama na zije kutumika vizazi na vizazi hadi mashuleni wanafunzi wajifunze kwa kutumia hotuba hizi. Hatuba hizi zionyeshe uwezo alionao kiongozi katika kutatua matatizo sio kusababisha matatizo.

Ukifuatilia mijadala mingi na mitafuruku mingi kwenye jamii yetu yanaibuliwa na viongozi wetu hasa kupitia hotuba zao. Tujitahidi kujenga taifa lenye umoja, haki na Ustawi bora kwa jamii yetu.

Wanaoandaa speech hizi za viongozi walenge mahitaji ya jamii na ustawi wa jamii husika. Speech hizi ziondoe Sintofahamu na mpasuko wa jamii, Speech hizi ziwaunganishe wana jamii zaidi. Speech hizi ziwe bora kiasi cha kuja kutumika na vizazi vingine.

Pichani ni Barack Obama akiwa na Msaidizi wake Ikulu ambaye ndiye humwandikia hotuba zake.

Picha ya pili ni January makamba akiwa na JK kwenye Kampeni kule Maswa hapo Ni baada ya kuwalisha Uongo na matumaini kibao wananchi wanaolima Pamba huko.

Picha ya tatu ni Uhuru Kenyatta akiwa na mashine ya Uongo na matumaini Denis Ithumbi.

Picha ya Nne ni Mwalimu Nyerere akiwa na Msaidizi wake wa Hotuba Mwanamama Joan Wicken.

CC: Polepole
CC: MATAGA

Ngoja nirudi jalalani.

Ole Mushi
071270602

FB_IMG_1584795801801.jpeg
FB_IMG_1584795809830.jpeg
FB_IMG_1584795823408.jpeg
FB_IMG_1584795831640.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bwana yule na polepole ,rejea maelekezo wahanga mafuriko wa milimani fursa kilimo wawauzie waliofurika.Corona hatufungi mipaka fursa watalii.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
hapa ndipo watu wenye akili wanapotofautiana na mabulula ila huyo wa kenya ni hatari zaidi maana alimtakatisha uhuru mpaka wakenya wakampenda na hata wakasahau kesi yake ya the hague
 
Tuna mambo ya msingi yakufanya,speech haziondoi umaskin mkuu

Hata wasipohutubia ila haki,maisha bora,utawala bora ukiwepo basi wananchi wataridhika tu..

Waafrica hawaangalii speech wanaangalia matumbo yao....
 
..ingependeza kama waandishi wa hotuba za mwinyi na mkapa nao wakatambuliwa.
 
Niliwahi kuwaandikia umuhimu wa hotuba za Viongozi wetu kuandaliwa kabla ya kuzisoma public.

Viongozi wetu wafahamu kuwa wao ni zaidi ya watabibu speech zao zinaweza kutibu majeraha ya watu au kuwatonesha, au kuwagawa watu au kuwapa mfadhaiko watu. Lazma viongozi wetu kwa umuhimu wao wasaidiwe eneo hili la public speaking.
Ole Mushi
071270602
Naunga mkono hoja nami niliwahi kushauri
Je, aachwe aseme tu, By "Taking The Bitter With The Sweet", Or Atumie Busara?!.

Wasaidizi wa Rais, Please Msaidieni Rais Wetu Kwenye Public . Msimuachie Kila Kitu Peke Yake! .

Naamini Rais Magufuli ana washauri wazuri na anashauriwa vizuri tuu! , Ila...

Rais Magufuli ni Mkweli Daima!. Jee Tumuunge Mkono Rais Wetu Katika Kila Ukweli Wake, Hata Kama Uko Kinyume cha Katiba, Sera na Ilani?.

P
 
Mleta mada umeongea kitu cha msingi sana sana. Ni vigumu kwa kiongozi mkubwa ambaye anatakiwa kuongea mara kwa mara kuweza kuandaa hotuba zake mwenyewe na zikawa na mvuto na asiwe anarudia rudia vitu vile vile.

Sema sasa kuna changamoto kadhaa tunazoweza kuziona,

1. Motive ya muhusika kushika nafasi anayoamua kushika inakuwa ni nini?

2. Mhusika yuko interested kujenga ushawishi? kuvutia watu, n.k au yuko interested na mambo gani?

3. Kuna suala la kuwa na fikra zinazoendeana kati ya mwandishi na mtoa hotuba. Kama wanafalsafa zinazotofautiana sana, inaweza kuwa shida.

4. Hao waandaaji wa hotuba za namna hiyo hapa kwetu wapo kwa sasa? Suppose akiamua kupita humu jf kutafuta sample za watu watano wanaoweza kuandaa speech zenye mvuto kama "I am prepared to die" ya Mandela, au " I have a dream" ya Luther n.k, unadhani anaweza kuwapata? Kwa sababu ili uweze kuwapa kazi watu, ni lazima kwanza hao watu wawepo, wawe wanapatikana, wawe wanaaminika na muhitaji awaone, na aone ni muhimu kuwatumia, vinginevyo haitawezekana.

Tuchukulie ni wewe, uambiwe utafute watu watano wenye uwezo huo, unawapata wapi, na unawapataje?

Kuna suala na dhamira, mitizamo, uelewa kwa pamoja ndivyo huamua

Anyway, umetoa mifano yote ya marais, vipi viongozi wa upinzani? wana hotuba zenye mvuto?au pia wanakabiliwa na changamoto hii? unadhani ni kwa nini wao hawatumii hiyo njia? unafikiri wanafahamu kama hilo ni tatizo? na maswali mengine kama hayo.
 
Jamii aliyoongoza Nyerere si sawa na aliyoongoza Mwinyi. Jamii aliyoongoza Mwinyi si sawa na aliyoongoza Mkapa. Jamii aliyoongoza Mkapa si sawa na aliyoongoza JK na jamii aliyoongoza JK si sawa na anayoiongoza Rais Magufuli na jamii anayoiongoza Rais Magufuli itakuwa si sawa na itakayoongozwa na atakayemrithi. Huu ni ukweli na haitaji uwe na Elimu ya chuo kikuu kuuona ukweli huu.
Sio kweli.

Mimi ninayo elimu ya chuo kikuu lakini sikubaliani na sioni mantiki ya nadharia hii.

Sikubaliani na dhana ya elimu ya darasani kuwa ndiyo elimu pekee ya kumpa uwezo binaadam kuelewa mambo hata yale yanayoghusa maisha yake ya kila siku.

Binaadam ni wale wale, wawe wa enzi ya Mwalimu Nyerere au nyakati za Magufuli, wote mahitaji yao ni yale yale.

Kama wa enzi za Magufuli wengi wao wanajua kuspma na kuandika kuliko wale wa enzi ya Mwalimu, uwezo huo pekee hauwafanyi waone na kuamua mambo tofauti na wale wa Mwalimu.

Sijasoma huko chini, pengine ni jambo tofauti lisilohusiana na aya hii ya utangulizi uliyoweka hapa.

Baada ya ku'skim through' yaliyoandikwa chini::

Sioni uhusiano wa 'para' hiyo na yaliyoandikwa chini yake.

Hata hivyo niseme tu kwamba, 'speech' ni sehemu ndogo tu inayomtambulisha kiongozi, na hata yaliyomo kwenye 'speech' mara nyingi ni yale anayoyahisi yeye, kuyaamini yeye. Hao waandishi hata wakilemba vipi, kama aliyeandikiwa hayaamini ni kazi bure.

Huyo Igathe naona unampa sifa asizostahili kabisa... Kisha tupiliwa mbali kama huna taarifa.

Lakini naungana nawe katika kusihi viongozi wawe na uwezo wa kupima matamshi yao kwa jamii.

Mambo mengi yanayofanyika sasa ni kutafuta sifa kwa wananchi kwa njia zisizofaa, na bila kujua kwamba ni mambo yanayofarakanisha badala ya kuunganisha umoja wa taifa letu.
 
Bwana yule hata akiandikiwa lazima aje na maneno yake mengine.
Nakuuliza Kituo Cha Afya Cha Kiyegea Kitaisha Lini
Unajua Usinitibue Nikaamua Vinginevyo

Haya Ndugu Zangu Nakwenda Huko Walikoshindwa Kujenga Daraja

Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
 
WINO WA DHAHABU:- WASAIDIZI WA VIONGOZI WETU WAJIFUNZE HAPA.

Na Thadei Ole Mushi.

Shida kubwa waliyonayo Viongozi wetu kwa Sasa ni kuongoza jamii yenye maarifa na Elimu kwa wingi.

Jamii aliyoongoza Nyerere si sawa na aliyoongoza Mwinyi. Jamii aliyoongoza Mwinyi si sawa na aliyoongoza Mkapa. Jamii aliyoongoza Mkapa si sawa na aliyoongoza JK na jamii aliyoongoza JK si sawa na anayoiongoza Rais Magufuli na jamii anayoiongoza Rais Magufuli itakuwa si sawa na itakayoongozwa na atakayemrithi. Huu ni ukweli na haitaji uwe na Elimu ya chuo kikuu kuuona ukweli huu.

TWENDE SAWA.

Imekuwa kawaida kabisa Sasa kiongozi anajifungia ndani anajiandaa haswa anatoka hadharani anaongea Jambo lake anaingia kwenye Gari yake kabla ya kufika nyumbani Jambo lile linachambuliwa na kuonekana kaongea kituko kabisa. Wasikasirike Bali wajifunze kuwa ni aina ya jamii waliyonayo kwa Sasa.

Kwa Sasa tuna wahitimu wengi haswa wa vyuo vikuu, na vyuo vya Kati wenye maarifa mbalimbali, Sasa hivi technolojia ya kupashana habari imekuwa, siku hizi watu wanajua haki yao ya kutoa maoni nk. Katika jamii Kama hii lazima Viongozi wetu wajiongeze na watafute maarifa mapya ya kukabiliana na jamii Kama hiyo.

Niliwahi kuwaandikia umuhimu wa hotuba za Viongozi wetu kuandaliwa kabla ya kuzisoma public. Nikiwasimulia kisa Cha Ghana na Marekani msaidizi wa Obama kwa kuandika haya nanukuu:-

"Kuna mtu anaitwa Nana Addo Dankwa Akufo-Addo huyu ni Rais wa Ghana. Ukimuuliza Leo mojawapo ya vitu ambavyo viliwahi kumkasirisha atakuambia ni January 7 mwaka 2017 siku aliyokuwa akiapishwa.

Siku hiyo mwandishi wa Hotuba zake bwana Eugene Arhin alifanya copy and paste ya hotuba ya Hotuba za marais wa Marekani Bill Clinton na Bush na kumpatia Rais ili akaisome kwa wananchi wa Ghana.

Hotuba hiyo ilisifiwa sana ila baada ya muda mfupi hata kabla ya Raisi kutoka kwenye Sherehe za kuapishwa watu walianza ukosoaji kitendo kilichomfanya Eugene Arhin kuomba msamaha kwa Rais na kwa wananchi wa Ghana. Ilikuwa aibu ya Mwaka ambayo Nana Akufo- Addo aliingia nayo Ikulu."

NATAKA KUSEMA NINI?

Nataka kusema kuwa Viongozi wetu wasaidiwe vyema katika maandalizi ya hotuba wanazokwenda kuzitoa kwenye majukwaa.

Kiongozi anaweza kukumbukwa kwa mambo makuu mawili moja speech zake au mambo aliyokuwa akiyafanya.

Ni Mara Chache sana kiongozi anaweza kuaandaa speech yake mwenyewe na kuitoa hadharani bila kupitia kwa mtu mwimgine kuihariri na kuifanyia marekebisho.

Mandela mpaka anakufa alitoa hotuba nyingi zenye msisimko lakini iliyovunja rekodi ni ile aliyoandaliwa na mhariri Nadine Gordimer akisaidiana na mwandishi Antony Sampson hotuba hii inaitwa "I am Prepared to die"

Wataalamu wa mambo wanasema hakuna speech ambayo imewahi kuvunja rekodi speech hii katika kusomwa na kutumika kama reference katika taifa la Afrika kusini.

Hapa kwetu Kuna Mama alikuwa akiitwa Joan Wicken huyu alikuwa ni raia wa uingereza ndiye alikuwa nyuma ya Speech za Baba Wa taifa Mwalimu Nyerere. Hotuba zote alizozitoa Nyerere njee ya nchi zilipitia kwa mama huyu Mwingereza aliyekuwa msaidizi wa mwalimu Nyerere.

Duniani kwa sasa Speech za Obama zinaendelea kuingiza mamilioni ya shilingi baada ya kuunganishwa kwa pamoja na kutengeneza kitabu. Piteni kwenye maduka ya kuuza vitabu mtaona

Sio Obama alikuwa akiandika hizi Speech Bali ni mtu aliyeitwa Jon Favreau ambaye Obama alianza naye pindi alipochaguliwa tu kuwa seneta na baadaye alihamia naye Ikulu. Obama alikuwa akimuita Favreau jina la utani "Mind Reader" kwa uwezo aliokuwa nao wa Kugundua nini Rais anataka kukisema na kukiweka kitaalamu ili kivutie watu na kifanye Clarification ya matatizo au Minongono ya wananchi.

January Makamba alijitutumua Kweli kuacha alama kwa Mzee Kikwete alikuwa anausoma mchezo, kwa vyama vya Siasa, Mitandaoni na kimataifa ndio anakaa anaandika speech ya Rais. Kwa kweli alijitahidi sana sintoshangaa Speech za Kikwete kuzikuta madukani, nimeshaona na kusoma kadhaa za Mzee Mkapa.

Pale Kenya Uhuru Kenyatta anao watu wawili Muhimu Sana mmoja anaitwa Eric Ng'eno na wa pili ni Denis Ithumbi. Eric Ng'eno yeye anahusika na kuandika Speech za Rais huku Denis yeye akiwa ni mzee wa media kwa ajili ya kuset Propaganda na kujibu propaganda zote zinazomhusu Rais.

Hawa ndio wanaompa Kenyatta Mvuto alionao Sasa. Kwa Nature ya wakenya ku win makabila yote Kama Kenyatta ni kazi kubwa Sana na kazi hii inafanywa na Hawa vijana wawili kwa ustadi mkubwa. Wanajua jamii inataka Nini na ipo katika Hali gani.

Viongozi wetu wafahamu kuwa wao ni zaidi ya watabibu speech zao zinaweza kutibu majeraha ya watu au kuwatonesha, au kuwagawa watu au kuwapa mfadhaiko watu. Lazima viongozi wetu kwa umuhimu wao wasaidiwe eneo hili la public speaking.

Speech zao ziache alama na zije kutumika vizazi na vizazi hadi mashuleni wanafunzi wajifunze kwa kutumia hotuba hizi. Hatuba hizi zionyeshe uwezo alionao kiongozi katika kutatua matatizo sio kusababisha matatizo.

Ukifuatilia mijadala mingi na mitafuruku mingi kwenye jamii yetu yanaibuliwa na viongozi wetu hasa kupitia hotuba zao. Tujitahidi kujenga taifa lenye umoja, haki na Ustawi bora kwa jamii yetu.

Wanaoandaa speech hizi za viongozi walenge mahitaji ya jamii na ustawi wa jamii husika. Speech hizi ziondoe Sintofahamu na mpasuko wa jamii, Speech hizi ziwaunganishe wana jamii zaidi. Speech hizi ziwe bora kiasi cha kuja kutumika na vizazi vingine.

Pichani ni Barack Obama akiwa na Msaidizi wake Ikulu ambaye ndiye humwandikia hotuba zake.

Picha ya pili ni January makamba akiwa na JK kwenye Kampeni kule Maswa hapo Ni baada ya kuwalisha Uongo na matumaini kibao wananchi wanaolima Pamba huko.

Picha ya tatu ni Uhuru Kenyatta akiwa na mashine ya Uongo na matumaini Denis Ithumbi.

Picha ya Nne ni Mwalimu Nyerere akiwa na Msaidizi wake wa Hotuba Mwanamama Joan Wicken.

CC: Polepole
CC: MATAGA

Ngoja nirudi jalalani.

Ole Mushi
071270602

View attachment 1395123View attachment 1395124View attachment 1395125View attachment 1395126

Sent using Jamii Forums mobile app
Inaonesha wewe ni wa juzi tu! Kama hukumpa ombeni sifue sifa kwa Mkapa basi tu! January Makamba ni masifa tu
 
Humu
Mleta mada umeongea kitu cha msingi sana sana. Ni vigumu kwa kiongozi mkubwa ambaye anatakiwa kuongea mara kwa mara kuweza kuandaa hotuba zake mwenyewe na zikawa na mvuto na asiwe anarudia rudia vitu vile vile.

Sema sasa kuna changamoto kadhaa tunazoweza kuziona,

1. Motive ya muhusika kushika nafasi anayoamua kushika inakuwa ni nini?

2. Mhusika yuko interested kujenga ushawishi? kuvutia watu, n.k au yuko interested na mambo gani?

3. Kuna suala la kuwa na fikra zinazoendeana kati ya mwandishi na mtoa hotuba. Kama wanafalsafa zinazotofautiana sana, inaweza kuwa shida.

4. Hao waandaaji wa hotuba za namna hiyo hapa kwetu wapo kwa sasa? Suppose akiamua kupita humu jf kutafuta sample za watu watano wanaoweza kuandaa speech zenye mvuto kama "I am prepared to die" ya Mandela, au " I have a dream" ya Luther n.k, unadhani anaweza kuwapata? Kwa sababu ili uweze kuwapa kazi watu, ni lazima kwanza hao watu wawepo, wawe wanapatikana, wawe wanaaminika na muhitaji awaone, na aone ni muhimu kuwatumia, vinginevyo haitawezekana.

Tuchukulie ni wewe, uambiwe utafute watu watano wenye uwezo huo, unawapata wapi, na unawapataje?

Kuna suala na dhamira, mitizamo, uelewa kwa pamoja ndivyo huamua

Anyway, umetoa mifano yote ya marais, vipi viongozi wa upinzani? wana hotuba zenye mvuto?au pia wanakabiliwa na changamoto hii? unadhani ni kwa nini wao hawatumii hiyo njia? unafikiri wanafahamu kama hilo ni tatizo? na maswali mengine kama hayo.
Pascal Mayala anaweza.
Vyama vya siasa mbadala- Zitto kabwe anavutia kusikiliza. Kuanzia sauti, ujengaji WA hoja, Contents za hoja zenyewe na zikiwa backed up na data. Anachokera na kukosa ni kutaka kutolea ufafanuzi au kuongea Kila tukio. Mengine awe anachuna yanapita Tu.
 
Kuanzia sauti, ujengaji WA hoja, Contents za hoja zenyewe na zikiwa backed up na data. Anachokera na kukosa ni kutaka kutolea ufafanuzi au kuongea Kila tukio. Mengine awe anachuna yanapita Tu.
Ninakubaliana nawe kwa hili. Na hii ni sifa nzuri sana kwake.

Ila kasoro/udhaifu unaomharibia kwa bahati mbaya sana, ni zaidi ya hiyo uliyotaja.

Lakini inawezekana akijengewa ushauri imara kudhibiti hayo, anaweza akawa mzuri.

Sina taarifa zinazoonyesha kwamba si msikivu wa ushauri, kama huyu tuliyenaye sasa hivi.
 
Tatizo La Magufuli Hashauriki Ubishi, Ujuaji, Sifa Majigambo Na Udicteta Zote Sifa Zake.

Ila Katika Speech Baada Ya Nyerere Na Mkapa Mkapa Alikuwa Kichwa Sana Akiwa Anahutubia.
 
Back
Top Bottom