Bikirembwe
JF-Expert Member
- Feb 13, 2008
- 250
- 7
Kwa nini nyinyi munaohisi kuwa Zanzibar inapendelewa katika hii ndoa ya Muungano kila wakati munatoa hoja ya idadi ya watu. Kumbukeni kuwa huu Muungano ambao ndio una matokeo mengi ( likiwemo hili la kugawa majimbo ya uchaguzi) ni makubaliano ya zilizokuwa nchi mbili Tanganyika + Zanzibar na sio wingi wa watu kama ni hivyo hamuoni kuwa hakuna haja ya watu milioni 40 kuungana na watu milioni 1. Acheni chokochoko kama unatoa hoja toa kwa kutumia vigezo kamili na ukumbuke kabla ya kufanya haya Zanzibar ilikuwa nchi na Serikali yake. Hakuna thamani ya hilo na tumekubali kuungana na kupoteza vyote hivyo. Jee wachina waombe viti vingapi? huko UN ikilinganishwa na Comoro.