Wingi Wabunge wa Zanzibar wana umuhimu gani Bunge la Muungano

Unajua watngyika tunafuata mambo kama mazuzu,haiwezekani rasilimali zetu eti zifaidishe nchi jirani(zanzibar)tuamke sasa tukatae upuuzi huu
 
Unajua watngyika tunafuata mambo kama mazuzu,haiwezekani rasilimali zetu eti zifaidishe nchi jirani(zanzibar)tuamke sasa tukatae upuuzi huu
Kumbe issue ya muungano Tatanganyika wengi hatuiifaki nadhani inabidi JK aunde tume ikusanye maoni Tanzania nzima juu ya kuwepo au kusiwepo muungano
 
Faida za muungano kwa tanganyika;
(1) kutumia kiti cha zanzibar UN kwa jina la tanzania. Ikumbukwe kua tanganyika haija wahi kua mwanachama wa UN.

(2) kupata misaada inayokuja kwa jina la tanzania bila ya kuigawiya zanzibar ambayo ni mshiriki wa muungano wa tanzania au kuipa zenji 4% tu ya hiyo misaada. Kumbuka kua budget ya tanzania kwa 40% inategemea misaada.

(3) tra inafanya kazi kote zanzibar na tanganyika lkn zrb inafanyakazi zanzibar pekee.

(4) bahari na mwambao wote wa africa mashariki ni mali ya zanzibar lkn leo tanganyika imejimilikisha kimaguvu kwa mwenvuli eti wa muungano.

(5) kuwasambaratisha wapemba wakatawanyika ktk kila upande wa tanganyika na dunia na kwa hivyo kupoteza utamaduni wa zanzibar ambao ni uislam kwa 99% na wakati huo huo kuhamia kwa watanganyika wengi zanzibar.

Kama hamuoni faida za muungano waulizeni wakubwa zenu wanajua nyie si mnakunywa pombe tu hamjui jambo mnafuata mkumbo hata hayo madini yenu hayawafaidishi leo mnataka mafuta ya zenji?
 
Nafikiri kuna haja ya kuwepo sheria katika uundwaji wa majimbo ya uchaguzi kuwa ili kuwa jimbo lazima liwe na wapiga kura labda tuseme laki moja minimum hivyo zenji tuweza kuwa na wabunge wa muungano watatu tu.
 
Wabunge wanaotoka Zanzibar wanapata umuhimu tu pale bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linapojadili mambo yaliyo kwenye Muungano, kwa mambo yanayohusu Tanzania Bara hawana umuhimu na tena hawapaswi kuwepo!
 
swala la kujiita nchi ni kweli kabisa,mimi nimekutana na wanzanzibar wanafunzi nje ya nchi ukiwauliza wanatoka wapi wanasema Zanzibar tena hawataki kabisa kuitwa watanzania,sasa mimi huwa nashangaa sana je huu muungano ni kwa faida ya nani?
Wazenj wanafaidi kodi zetu bila tija yoyote,kwanza wanajíita nchi,tukate hii mirija watoto wetu wasome bure
 
Yaani kwa ratio ya watu milioni 1 kuwa na wabunge 70+ basi kwa watu milioni 40 tungetakiwa kuwa na wabunge 40x70 = 2800 which is very unrealistic...na kwa kule Zenji unakuta kila mtaa ni jimbo yaani kwa huku Dar, Sinza ni mkoa wenye majimbo kama Palestina, Makaburini, Mugabe, Kwa Remmy, Africa Sana n.k

Duh mkuu mimi naijua zanzibar nadhani unayosema sio kweli labda unaizungumzia zanzibar nyingine sio hii ya marashi ya karafuu.
 
Faida za muungano kwa tanganyika;
(1) kutumia kiti cha zanzibar UN kwa jina la tanzania. Ikumbukwe kua tanganyika haija wahi kua mwanachama wa UN.

(2) kupata misaada inayokuja kwa jina la tanzania bila ya kuigawiya zanzibar ambayo ni mshiriki wa muungano wa tanzania au kuipa zenji 4% tu ya hiyo misaada. Kumbuka kua budget ya tanzania kwa 40% inategemea misaada.

(3) tra inafanya kazi kote zanzibar na tanganyika lkn zrb inafanyakazi zanzibar pekee.

(4) bahari na mwambao wote wa africa mashariki ni mali ya zanzibar lkn leo tanganyika imejimilikisha kimaguvu kwa mwenvuli eti wa muungano.

(5) kuwasambaratisha wapemba wakatawanyika ktk kila upande wa tanganyika na dunia na kwa hivyo kupoteza utamaduni wa zanzibar ambao ni uislam kwa 99% na wakati huo huo kuhamia kwa watanganyika wengi zanzibar.

Kama hamuoni faida za muungano waulizeni wakubwa zenu wanajua nyie si mnakunywa pombe tu hamjui jambo mnafuata mkumbo hata hayo madini yenu hayawafaidishi leo mnataka mafuta ya zenji?

Hayo mafuta unayoleta nayo tambwe hapa bado ni yakufikirika maana hata kuchimbwa bado. Na vivyo hivyo Pande za kwetu (Tanganyika) yapo vilevile na vitu vingine vingi vya thamani.

Halafu nakukumbusha ya kwamba kijiografia hivyo visiwa vitapotea baada ya miaka kadhaa ijayo hivyo na vitukuu vyenu vatapotea lakini tupo tayari kuwapa hifadhi jirani.
 
Faida za muungano kwa tanganyika;
(1) kutumia kiti cha zanzibar UN kwa jina la tanzania. Ikumbukwe kua tanganyika haija wahi kua mwanachama wa UN.

Kinatusaidia nini sisi hicho KITI? Muungano ufe na Kiti chenu chukueni wala hatukihitaji [kama kweli kipo na ni chenu]

(2) kupata misaada inayokuja kwa jina la tanzania bila ya kuigawiya zanzibar ambayo ni mshiriki wa muungano wa tanzania au kuipa zenji 4% tu ya hiyo misaada. Kumbuka kua budget ya tanzania kwa 40% inategemea misaada.

4% hata hivyo bado ni kubwa sana, mie nadhani kama kusingekuwa na Muungano hata hiyo 4% ingekuwa ya Tanganyika. Na kama mnaona mnapunjwa kwanini bado mnajing'ang'aniza kwenye Muungano. Walio wengi hatuutaki ati.

(3) tra inafanya kazi kote zanzibar na tanganyika lkn zrb inafanyakazi zanzibar pekee.

Pato la taifa linatoka TRA linatumia kote ZNZ na TNGK huyo mchukua kodi mwingine kodi yake yote inabaki hapo hapo, na kodi ya TRA ni kwa vile vitu vinavyohusika na Muungano

(4) bahari na mwambao wote wa africa mashariki ni mali ya zanzibar lkn leo tanganyika imejimilikisha kimaguvu kwa mwenvuli eti wa muungano.

Hata kulivyo na muungano hivi bado mipaka ya kibahari iko pale pale, hata muungano ukiwa haupo hiyo mipaka ya kibahari itabaki kama ilivyo maana ni mipaka ya nchi inayotambuliwa kimataifa

(5) kuwasambaratisha wapemba wakatawanyika ktk kila upande wa tanganyika na dunia na kwa hivyo kupoteza utamaduni wa zanzibar ambao ni uislam kwa 99% na wakati huo huo kuhamia kwa watanganyika wengi zanzibar.

Kuenzi utamaduni ni mtu mwenyewe, wewe leo hii unajitambua ni mzanzibari bila kujali uko wapi duniani, imani bado ni mtu mwenyewe, wewe umekuwa muislamu tu kwa sababu walokutangulia duniani walikuwa waislamu nao wamekuwa waislamu wa sababu tu mkoloni wa kwanza wa zanzibar alikuwa muislamu. kama Mreno angekuwa mkoloni wenu leo hii hata uarabu ungekuwa na hadithi kwenu sembuse uislamu. Waislamu wangapi wanabadili dini kwa kuhisi uislamu sio dini sahihi? vile vile wakristo wangapi wanabadili dini wakiadhani ukristo sio dini sahihi?

Utashi wa mtu hauna impact kwenye Muungano. Ama muungano uwepo au usiwepo hayo hapo juu yaweza kutokea kwa watu kama binadamu.

Kama hamuoni faida za muungano waulizeni wakubwa zenu wanajua nyie si mnakunywa pombe tu hamjui jambo mnafuata mkumbo hata hayo madini yenu hayawafaidishi leo mnataka mafuta ya zenji?

Kimsingi Muungano huu uliopo hauna tija. Pemba kutengana na Unguja bado sio tatizo kimsingi kama wanaamini kuwa wao kama wapemba wanaweza kuendesha kisiwa chao kama Nchi. Sioni Nguvu ya Muungano inayotuweza kuzuia mtengano wa unguja na pemba zaidi ya mabavu ya CCM iliyojikita kwenye maeneo yote matatu.

Faida pekee CCM wanayoipa kwenye huu Muungano ni uwezo wa kuamua nani awe mtawala wa ZNZ na nani asiwe. Mfano mzuri ni chaguzi zote nne za vyama vingi huko ZNZ

habari ndio hiyo
 
Labda nimsaidie muanzilishi wa thread hii kuwa wakati zanzibar na Tanganyika zinaungana zote zilikuwa na hadhi sawa ya nchi (Nation). Si sahihi kulinganisha jimbo la Kawe na nchi ya Zanzibar. Labda cha kulinganisha ambacho watanganyika hawakitaki ni mgao wa faida ya Benki kuu, kwani ilianzishwa kwa pesa kutoka Tanganyika na Zanzibar, na leo hii Serikali ya CCM inakataa kuipa mgao wa faida Zanzibar, ni hivi karibuni (1990+) ndio walianza kuipa kijisehemu tu cha share ya Zanzibar, tunataka share kamili. Kama hujui vipi Tanganyika inafaidika kwa zanzibar basi moja ni hilo, na tutawapigia mahesabu na riba mulipe, muone Zanzibar itakuwa wapi...Pia Watanganyika wanajua wakiwacha Zanzibar ijitawale itapiga hatua kubwa na hivyo itawaamsha maiti wao (watanganyika) kudai mabadiliko.
 
Mkuu hapa pamoja na ukweli unauma ni kweli kabisa
 
@ kimwe hayo mafuta hata kama hayajachimbwa lkn yapo na munayataka. Lkn mungalishughulikia uranium yenu na tanzanite zikawafaidisha ingekua vizuri kuliko kun'gan'gania mafuta ya zenji.

@ endeleaaa ama kweli weye kilaza unauliza kiti ktk UN kinakusaidieni vipi watanganyika? Kama hakuna muungano na nyie hamna kiti UN hiyo misaada munayowagaia wazenji 4% musingaliipata kwani musingalitambuliwa kimataifa.

@Endeleaaa wazenji wengi hawana haja ya muungano na hata ikibidi basi alau uwe wa serikali 3. Ukisema ccm ndio ving'ang'anizi wa muungano sawa lkn na watanganyika pia wanautaka maana wanaendelea kuichagua ccm kwa wingi.

Unasema mapato ya TRA yanatumika kote tanganyika na zanzibar sawa lkn ilikua yatumike kwa mambo ya muungano tu lkn kwa nini mambo ambayo si ya muungano kwa zanzibar yanategemea ZRB Lkn mambo ambayo si ya muungano kwa tanganyika yanaendeshwa kwa mapato ya TRA pia? Weye umesoma shule ya msingi kwa kodi ya wazenji, huduma za afya pia zinatumia kodi za tra lkn afya si ya muungano inakuaje hapa? Mambo ambayo si ya muungano ni mengi na munatumia kodi za wazenji kuyaendesha halafu unasema huoni faida ya muungano weye umelewa nini?

Kuhusu utamaduni lazima ujue kua unaathirika ukikumbana na utamaduni mwengine ndio maana ukawaona watanganyika wengi leo wanakwenda uchi kuiga utamaduni wa wazungu lkn kwenda uchi hasa si utamaduni wa watanganyika.

Kama vipi tushirikiane ili tuuvunje huu muungano yaishe haya malalamiko au vipi?
 
Mtabe said:
kutumia kiti cha zanzibar UN kwa jina la tanzania. Ikumbukwe kua tanganyika haija wahi kua mwanachama wa UN.

Mtabe,

..Tanganyika ilikuwa na mwanachama wa UN kabla ya Muungano na mabalozi waliotuwakilisha walikuwa Nsilo Swai na Chief Erasto Mangenya.

..hata Zanzibar nayo ilikuwa ni mwanachama na ilikuwa na balozi wake huko UN.

..tulipoungana, kila nchi ilijivua uanachama wake, na kwa pamoja tukajiandikisha upya kama Tanzania.

..Muungano ukivunjika pande zote mbili zinaweza kujiandikisha upya na kurudia uanachama wao kama ilivyokuwa kabla ya mwaka 1964.
 
Sina habari kua nchi moja inawakilishwa na mabalozi wawili UN. Hata hivyo tuambie basi ni lini tanganyika ilianza kua mwanachama wa un? Zanzibar ilianza dec 1963 na bendera ya zanzibar un ilipachikwa siku moja na kenya. Tafuta watoto uwadanganye kwa taarifa yako mpaka leo tanganyika haijapata uhuru wake.
 
Jamani nauiliza hivi hawa wabunge wa Zanzibar 50+ wa kuchaguliwa na 20+ viti maalumu making a total of 70+ kwenye bunge la jamuhuri lenye wabunge 329 mbona wengi sana na sioni impact yao? Wanakula ruzuku za bure nadhani mbali na kupunguza idadi ya mawaziri tungefikiria kupunguza idadi ya wabunge na hasa wa Zanzibar ambayo unakuta kwa kila watu elfu wana mbunge mmoja?
mkuu uko sahihi, inasikitisha kuona wapiga kura laki tano wanapewa 30 percent wakati theyw ere suppoesed to be given less than 10% ya votes and representation

Ila kikubwa ujue hawana influence yoyote zaidi ya kupokea alawansi

sijawahi kuona impact ya mbinge wa zenji tangu nizaliwe
 
Impact yao japo wako wengi is almost negligible if not close to zero
 
Mtabe said:
Sina habari kua nchi moja inawakilishwa na mabalozi wawili UN. Hata hivyo tuambie basi ni lini tanganyika ilianza kua mwanachama wa un? Zanzibar ilianza dec 1963 na bendera ya zanzibar un ilipachikwa siku moja na kenya. Tafuta watoto uwadanganye kwa taarifa yako mpaka leo tanganyika haijapata uhuru wake.

Mtabe,

..Tanganyika ilikuwa mwanachama wa UN kabla Zanzibar haijapata "uhuru."

.. Uanachama wa Tanganyika UN ulianza 14 Dec 1961.

..Zanzibar ilipata uanachama wake kuanzia 16 Dec 1963.

..baada ya kuungana na kuunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, sote tuliachia viti vyetu na kuchukua kiti kimoja November 1, 1964.

..Muungano ukivunjika Tanganyika na Zanzibar zinaweza kurudia uanachama wao wa zamani bila matatizo yoyote yale. Muungano wa Czechoslovakia ulipofunjika jamhuri za Czech na Slovak zilikubaliwa na UN kama wanachama wapya.

NB:

..taarifa nilizoweka hapo juu nimezipata toka mtandao wa UN.
 
Wazanzibar wanachonga sana wakati sisi tumewapunguzia matatizo kwa kuwapatia ajira (bungeni, serikalini) na kwenye mashirika binafsi, pia kuna wengi ambao wamepata ardhi bara na hakuna anayelalamika.

Inabidi tubadirishe muundo wa muungano ili kuwe na equity katika uendeshaji wa serikali ya pamoja vinginevyo tunanyonywa
 
  • Ukweli Muungano ni liability kubwa sana kwa Bara!
  • Ni vema kwa bara hata kuungana na Kenya wenye watu wengi na uchumi mkubwa!
  • Faida kwa bara.. may be stability..ila sasa watu milioni 1 wanapewa viti 70 against watu milioni 42 wanopewa viti 270 hivi! Is this Fair?
 
Back
Top Bottom