Uchaguzi 2020 Wingi wa wagombea CCM ni uthibitisho kazi nzuri ya Rais Magufuli kwa taifa letu. Je, Oktoba ni kuchagua au kuthibitisha tu taratibu?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,467
113,567
Wanabodi,

Tunapoelekea kwenye hatua ya kwanza ya uchaguzi kwa uchukuaji wa fomu za kugombea kwenye vyama vya siasa, kumejitokeza, uwingi wa mkubwa, wa wagombea kupitia CCM.

Huu ni uthibitisho wa kazi kubwa na nzuri iliyofanywa na Rais, Dr. John Pombe Joseph Magufuli na awamu yake ya 5, na inayoendelea kufanywa kwa taifa letu la Tanzania, ikiwemo kupambana na rushwa, kuongeza uwajibikaji, kupaisha maendeleo ya nchi kwa maendeleo makubwa ya kuonekanika katika baadhi ya sekta, ikiwemo kulifufua shirika la ndege la Tanzania, ATCL, kujenga SGR, Stigler, barabara za juu kwa juu, elimu bure, kujenga Tanzania ya viwanda, kuiingiza nchi yetu kuwa ni nchi ya uchumi wa kati na mengine mengi makubwa mazuri, kulikopelekea Watanzania wengi wakiwemo wapinzani kumkubali JPM na kuikubali CCM, hivyo kuunga mkono juhudi kwa kumpenda JPM, kumkubali, na kuipenda CCM na kuifanya kukubalika sana, hivyo kwenye uchaguzi wa mwaka huu, kujikuta watu wengi kujitokeza kwa mamia kugombea jimbo moja mfano jimbo la Kawe, ili tuu kumuunga mkono rais Magufuli na kujitokeza kumsaidia.

Swali ni jee uchaguzi wa October ni uchaguzi wa kuchagua kwa kushindanisha vyama au kushindanisha wagombea, au ni tunakwenda tuu kwenye uchaguzi kuithibitisha tuu ushindi wa kishindo wa CCM, ambayo tayari imeishashinda uchaguzi Mkuu huu mioyoni mwa watu, na uchaguzi ni kwa ajili tuu ya kukamilisha taratatibu za uchaguzi, au kutakuwa na ushindani wa kweli wa kisiasa au CCM tuu huku ikisindikizwa na vyama vingine?.

Angalizo:
Wakati hata mimi nikiendelea kujishauri na kujiuliza, ndani ya siku mbili hizi, kama na mimi nijitose au laa, naomba kuwapa angalizo dogo, kuwa sio kila anayejitokeza kuchukua fomu kugombea ubunge au udiwani kupitia CCM, yuko very serious kugombea ili kupata ubunge au udiwani!, kuna baadhi wanagombea kwa sababu nyingine kabisa na wala sio kuutaka ubunge, udiwani au uwakilishi wa wananchi. Hivyo hawa wagombea wanaogombea kwa sababu nyingine, hata wasipochaguliwa, wanakuwa wametimiza malengo maana kwao kugombea tuu, ni ushindi tosha. Hivyo naombeni sana, mkisikia na mimi nimejitosa, kugombea kupitia CCM, nawaombeni msinishangae!.

Kwa vile hili la kazi nzuri ya Rais Magufuli niliisha lizungumza humu tangu ile 2015, mara tuu baada ya uchaguzi, nikizungumzia uchaguzi Mkuu huu wa 2020, na sasa hii ndio 2020 yenyewe na uchaguzi wenyewe ndio huu, kuna haja ya kujikumbusha tu ile 2015 nilisema nini kuhusu Magufuli na uchaguzi wa 2020, na sasa hii 2020 ndio hii, nini kinatokea...

Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?

Na October yenyewe ndio hiyo inakuja, iko just around the corner, jee sasa tunakwenda kwenye uchaguzi kuchagua au ni kwenda tuu kuithibitisha kazi nzuri ya JPM na CCM tuu ili aendelee?.

Paskali
 
Wewe bana sema tu kwamba saizi umetizamwa kwa jicho la huruma kidogo.

JPM HANA ALICHOFANYA ambacho kinamgusa mwananchi wa hali ya chini moja kwa moja.

Ujanja anaotumia kuonesha kwamba ni mtu wa watu, ni ivi vimisaada anavyotoa barabaran kwa wajane mmoja mmoja... basi Wajinga wenu wanamuona mtu wa mtu .
 
Wakuu yaani kila ninayemfahamu anaona anaweza kuwa mbunge kupitia CCM.

Niko na mdogo wangu hapa ananiambia hata yeye anaona kama anaweza kuwa mbunge wa CCM mwaka huu akiamua wakati hajui hata Polepole ni nani au katibu mkuu wa CCM ni nani.

Maana kila mtu anaona anaweza.

NINI MAONI YAKO.

1: Je, Ubunge umerahisishwa sana wakati huu?

2: Je, CCM Imekuwa safi kiasi kwamba hakuna hata wasio na pesa nao wanaweza kupita kuwa wabunge?

3: Je, Ubunge Watu wanatamani kufanya kazi na Raisi ajaye ikiwa mwenyekinti wa CCM atashinda?

Nini maoni yako
 
'Na moja kati ya kazi nzuri serikali ya awamu ya 5 ni kukurudishia wewe kibali chako cha kurusha matangazo kwny maonyesho ya saba saba.'


Tangu arudishiwe kile kibali chake, naona mzee mzima akili imemvuruga kabisa. Kuna kila dalili ya mwandishi wetu nguli na mbobezi kufuata nyendo za rafiki yake manyerere

Maana kwa sasa huwezi kumuambia chochote kuhusu Magufuli.
 
NINI MAONI YAKO.

1: Je Ubunge umerahisishwa sana wakati huu?

2: Je CCM Imekuwa safi kiasi kwamba hakuna hata wasio na pesa nao wanaweza kupita kuwa wabunge ?

3: Je Ubunge Watu wanatamani kufanya kazi na Raisi ajaye ikiwa mwenyekinti wa CCM atashinda?



nini maoni yako

Kwa maswali yako hayo mazuri, na wewe ungeazisha thread yako inayojitegemea!
 
Back
Top Bottom