gemmanuel265
JF-Expert Member
- Feb 16, 2016
- 8,485
- 18,045
Wajibu na majukumu ya mbunge kikatiba ni kutunga sheria, kuisimamia serikali na kuiwajibisha pale inapobidi
Wabunge wote bila kujali vyama vyao vya kisiasa majukumu yao kikatiba hayatofautini, hivyo ni aibu kubwa sana kuona wabunge wa chama tawala wanapogeuka kuwa sehemu ya serikali iliyoko madarakani
Hii ni aibu kubwa sana kwa muhimili huu wa bunge kwa kukosa sifa ya uwakilishi wa wananchi na kuwa sehemu ya uwakilishi wa serikali, na kibaya zaidi watu wanaokosoa utendaji kazi wa bunge hili kwa hoja wanaonekana ni wachochezi
Mbunge badala ya kujadili bajeti ya maendeleo anaishia kujadili udaku wa kutunga kwenye chama pinzani na chama tawala ili kufurahisha wabunge wa chama cha upande wake
Wabunge wa ccm wanakosa kabisa sifa za kuwa wawakilishi wa wananchi sababu wanachokijadili ndani ya bunge ni kuattack vyama pinzani pekee badala ya kuungana na wabunge wa upinzani kuisimamia ipasavyo serikali, lakini wao ndio wanakuwa madodoki ya serikali kusafisha uchafu wake
Hili ni bunge kibogoyo kabisa kuwahi kutokea toka kuondoka kwa wakoloni weupe ambalo haliwezi kuiwajibisha serikali, kazi yake iliyobaki ni kujipendekeza kwa serikali iliyopo madarakani
Wabunge wa ccm ni tatizo kubwa ndani ya bunge, hawajui kilichowapeleka mule, hawajui kujitofautisha wao na serikali kama ni mihimili tofauti wa dola inayojitegemea
Wabunge wa ccm hii ya kulazimisha watu wote kusifia sifia yale yanayofanywa na serikali kana kwamba maendeleo ni fadhila ni ujinga wa mwendo kasi, serikali iko kwa ajili ya wananchi na inawajibika kwa wananchi moja kwa moja, sasa hii tabia ya kulazimisha kushangilia na kusifu kwa kupewa kidogo na kunyimwa vingi inatoka wapi!
Kutegemea mabadiliko chanya katika taifa hili kupitia bunge la aina hii ndani ya Tanzania ni kuchoma mahindi kwa kutumia mwanga wa mbalamwezi.