Wimbo Wa Taifa La Zanzibar Kupigwa Baraza La Wawakilishi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wimbo Wa Taifa La Zanzibar Kupigwa Baraza La Wawakilishi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Junius, Oct 29, 2009.

 1. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #1
  Oct 29, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema inakusudia kupiga wimbo wa taifa katika kikao cha baraza la wawakilishi kijacho kutokana na marekebisho ya kanuni za baraza la wawakilishi zilizofanywa na wajumbe wa baraza hilo.

  Waziri wa Nchi Afisi ya Waziri Kiongozi Hamza Hassan Juma aliwaambia wajumbe wa baraza hilo wakati akifanya majumuisho ya kanuni za baraza la wawakilishi toleo la mwaka 2007 katika kikao hicho kinachoendelea kwa wiki ya tatu sasa.

  "Kuimbwa wimbo wa taifa katika baraza letu hili tukufu litawathibitishia wale wanaosema Zanzibar sio nchi wanajua sasa kama hii ni nchi kamili ninachoomba kwa wajumbe hivi sasa waanze kujifunza wimbo huo wa taifa waaze mazoezi ya kuuhifadhi mapendekezo yakipita tu kikao kijacho tunaanza na kuweka CD yetu ambayo itatuongoza na sisi wajumbe sote tutaanza kuimba" alisema Waziri huyo kwa kujiamini.

  Kwa mujibu wa marekebisho ya kanuni ya 27 pendekezo la kupigwa wimbo wa taifa limeelezwa kuwa ni kujenga utaifa na kukuza uzalendo wa wajumbe na wananchi wote kwa jumla pamoja na kutoa ishara ya umuhimu wa shughuli zinazofanywa na baraza kitaifa.
  Katika marekebisho mengine ya kanuni hizo imependekezwa kwua utaratibu wa uchaguzi katika kuwatafuta wajumbe wa baraza wanaochaguliwa na baraza ili kuwa wajumbe wa tume ya bajeti urekebishwe ili wanaocfhaguliwa wasiwe mawaziri, wala manaibu wala wakuu wa mikoa na angalau mmoja kati yao ni lazima awe mwanamke.

  Waziri Hamza alisema kanuni ya 143 mapendekezo hayo yanalenga kuipa uhuru zaidi tume hiyo na kuzingatia usawa wa kijinsia katika vyombo vya kufanya maamuzi ya baraza la wawakilishi.

  Waziri huyo pia alisema katika marekebisho mapya marekebisho yamependekeza katika kanuni ya 10 kuwa wenyeviti wa baraza wawe wawili badala ya mmoja kama ilivyo na uchaguzi wao uzingatie jinsia.

  Pendekezo hili linalenga kutoa fursa ya kijinsia katika "uongozi wa baraza. Hata hivyo endapo itatokezea waliojaza fomu na kuomba kuchaguliwa wenyeviti ni wajumbe wa jinsia moja tu basi uchaguzi utafanyika kwa wajumbe hao walioomba. Aidha kuna mapendekezo yanayotolewa kwa ajili ya kuoainisha maneno yaliyotumiwa kwenye kanuni na yale yaliotumiwa kwenye katiba. Mfano wa marekebisho hayo ni kanuni ya 59(10)"alisema Waziri huyo.

  Katika marekebisho hayo kamati ya PAC inapendekezwa ipewe uwezo zaidi inapopitia hoja za mshibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ili ijiridhishe pia kwa kiwango cha fedha kinachotumika kulingana na thamani halisi ya kitu au kazi iliyofanywa au kitu kilichonunuliwa (value for money), (kanuni 112).

  "Spika atalazimika kukubaliana na ushauri wa kamati ya maadili na endapo atakuwa na mawazo tofauti atapaswa apeleke ushauri huo kwneye baraza kwa uwamuzi wa mwisho (kanuni 114) vile vile idadi ya wajumbe wa kamati teule inapendekezwa iongozwe kupitia marekebisho ya kanuni 115 halikadhalika inapendekezwa kuwa mwenyekiti wa kamati teule awe na kura ya uwamuzi tu bila ya kura ya kawaida" amesema Waziri Hamza.

  Katika marekebisho hayo ya kanuni pia kuna marekebisho yanayopendekezwa ili kuondoa kasoro zinazoonekana kuathiri utekelezaji wa kanuni zenyewe. Mapendekezo ya aina hiyo ni pamoja na utekelezaji wa kanuni zenyewe.

  "Mapendekezo ya aina hii na marekebisho ya kanuni ya 24 ambayo yanalenga kumpa uwezo Spika kuahirisha kikao cha baraza bila ya kuwahoji wajumbe endapo shughuli za kikao zimemalizika mapema kabla ya kufikia muda wa kawaida wa kuahirisha baraza" alisema Waziri huyo na kusisitiza kwamba kifungu hicho ni muhimu kwa kuwa ipo siku wajumbe watafanya vituko kwa kumkatalia Spika kumaliza shughuli na kubakia kutazamana hivyo kufanyiwa marekebisho hayo kutaongeza ufanisi.

  Hata hivyo Waziri huyo alisema inapendekezwa kwamba endapo mapendekezo ya marekebisho hayo yatakubaliwa na kupitishwa basi yaanze kutumika kwenye mkutano ujao wa 18 wa baraza la wawakilishi yaani kikao kinachokuja.

  Wakitoa maoni yao wajumbe wa baraza hilo wamekubaliana na hoja zilizotolewa na zaidi hoja ya kupigwa wimbo wa taifa wamesema itakuwa ni furaha ya kuonesha kuwa Zanzibar hivi sasa inaonesha kuwa ni nchi kwa kupigwa wimbo huo ambao kwa muda mrefu wajumbe hao walikuwa wakiulilia na kutaka utumike katika chombo hicho muhimu cha kutunga sheria.

  SOURCE:ZANZIBAR YETU WEB BLOG.
   
 2. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #2
  Oct 29, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  wimbo wenyewe ni:

  Mungu ametubarikia, Unguja na Pemba yote.
  Sote tunashangillia, Jamhuri kutuletea.
  Mungu ametubarikia, Jamhuri kutuletea
   
 3. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #3
  Oct 29, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Mizengo Pinda upo...we baki na katiba yako ya ki-CCM, sisi yetu tunasema ni nchi...mkipenda msipende ndo hivyo.
   
 4. m

  mtemi Member

  #4
  Oct 29, 2009
  Joined: Jun 17, 2009
  Messages: 56
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  washamba nyie nani kakwambieni wimbo ndio nchi?? hata vichaa huimba!!! yaani kama genge la majuha
   
 5. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #5
  Oct 29, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,647
  Likes Received: 1,475
  Trophy Points: 280

  hahaha, Junius, hiyo Jamhuri ndio ipi hapo? LOL
   
 6. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #6
  Oct 29, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Wimbo huo utaimbwa hapo nje ya jengo la kusanyiko la genge pekee . Wimbo hauwezi kuvuka mipaka . Mkuu wa Mkoa ambaye ni Rais huko hawezi kuibiwa wimbo huo .Hata Passport ambacho kitu muhimu , pesa na jeshi .Kweli mko gizani nyie . Poleni sana . Endeleeni kuimba .

  Nitawaona kama Nchi mkianza na pesa yenu, Passport yenu, Jeshi la polisi lenu, Amiri Jeshi mkuu wenu , nk
   
 7. Babylon

  Babylon JF-Expert Member

  #7
  Oct 30, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 1,338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mungu awazidishie kuwatowa katika Giza Hilo walilo Gubiziwa na waleeeeeee.
   
 8. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #8
  Oct 30, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Kuimba wimbo wa "taifa" haifanya nchi kuwa taifa. Kuimba kuhusu Jamhuri haikufanyi Unguja na Pemba kuwa jamhuri. Je unajua mkuu Palestina na Somalilannd wana nyimbo za taifa? Je nazo ni nchi? Kuangalia kama Zanzibar ni nchi lazima tuandike mamlaka liyo nayo na "power capacity" yake.
   
 9. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #9
  Oct 30, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Hata jimbo la Maryland lina wimbo wake wa jimbo. Lakini hauitwi wimbo wa taifa. Wimbo wa Taifa la Tanzania ni Mungu Ibariki Afrika. Full stop!
   
 10. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #10
  Oct 30, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Ni jamhuri ya watu wa Zanzibar ambayo ilikuwapo kabla ya Januari 12 1964 na April 1964, hata hiyo inayoitwa Jamhuri ya Muungano inatokana na Jamri mbili kuungana japo kidhambi dhambi...au pia hili unakataa Mkuu?
  Wenzako tunajimezua kidogo kidogo, kweli tunaendelea kuimba lakini tumeanza na kupepea bendera...mkabaki kusema eti ni kama bendera ya Yanga...tukahodhi mafuta...sasa tunakuja kwenye wimbo wa taifa...hujuwi kinachofuata...? subirini tu...
  Nani kakwambia kuwa Somaliland na Palestina si nchi...hiyo power capacity iwe kwa kiwango kipi ndo nchi iwe nchi...chukuwa mfano England, Scotland, Welsh na N.Ireland..zote hizi zina hiyo "Power Capacity" unayosema na wanabaki katika Muungano wa Himaya za Ufalme "United kingdom&N.Ireland...lakini bado zinatambulika kama nchi...na hakuna hata moja yenye kiti cha UN, zote zinakwenda kwa mwamvuli wa UK, lakini bado ni nchi..labda nikujuvye, usifate mkumbo wa hawa vichwa maji...ww si kichwa maji...unafahamu vizuri...kuna tofauti kati ya "country" and "state", mimi sijadai Zanzibar ni "state" bali nasisitiza kuwa zanzibar ni "country". Kwakuwa "state" must mantain full sovereinty though sometime it can be limited, but its not necessary for the country to be fully soveregnty it can be semi-autonomous or soveregn,the same case to Zanzibar and Tanganyika...kwa kesi kama ya Palestina ni Mamlaka ambayo inatambuliwa "authority" na inakiti mpaka Umoja wa Mataifa...saa kwanini unakataa kuwa si nchi? (don't confuse this situation with U.S)
  Mimi siongei bari za wimbo wa taifa la Tanzania...naongea wa Zanzibar ambao ni "Mungu ametubarikia..." unapigwa kila siku inapofunguliwa redio zanzibar na televisheni ya zanzibar...kila siku wanafunzi wanapokuwa assembly wanaimba...hapaimbwi "Mungu ibariki.." wimbo huo mmi hata mashairi yake siyajuwi vizuri...ujuwe kuwa si maarufu Zanzibar...upo!
   
 11. October

  October JF-Expert Member

  #11
  Oct 30, 2009
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 2,147
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kuwa na wimbo hakumaanishi kwamba mnakua taifa, hata shuleni tulikua tuna wimbo wa shule lakini umuhimu wa nyimbo zile ulikua unaishia palepale shuleni, hata tulipokua tukienda Umiseta tukua hatuwezi kuimba wimbo wa shule yetu.

  Wimbo huu wa Zanziba ni kichekesho tu na ni sawa tu na wimbo wa shule maana hauwezi kuvuka mipaka ya Zanzibar. Kama kweli una maana wautumie wanapokwenda nje ya nchi ili tujue kua una maana, Otherwise ni sawa na wimbo wa shule tu...tena shule ya chekechea.

  Acheni kushangilia wimbo wa chekechea
   
 12. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #12
  Oct 30, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Hata Rome haikujengwa kwa siku moja.

  HONGERA SAAANA WAWAKILISHI KULIONA HILO. Na Insh'Allah tutatoka kwenye ukoloni huu mkongwe.

  haya tuimbe kwa pamoja:
  Mungu ametubarikia, Unguja na Pemba yote.
  Sote tunashangillia, Jamhuri kutuletea.

  Mungu ametubarikia, Jamhuri kutuletea
   
 13. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #13
  Oct 30, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  October,
  Wivu tu!!!!
   
 14. u

  under_age JF-Expert Member

  #14
  Oct 30, 2009
  Joined: Apr 17, 2007
  Messages: 317
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  uhuru wetu wazanzibari unanukia. mbaya wetu sio ccm wala cuf . kuna mtu anatutia vijiti vya masikio tugombane atutawale. tumeanza kuamka . Mungu ametubarikia unguja na pemba yote, soote tunashangilia , jamhuri kutuleteaa , Mungu ametubarikiaa Unguja na Pemba yoteee. hongereni baraza la wawawikilishi, hatua kwa hatua tutafika.

  wazenji tumechoka!
   
 15. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #15
  Oct 30, 2009
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kwa hiyo kama Jamhuri ya Zanzibar na Serilaki ya Jamhuri ya Tanganyika ni wanyama waliokuwapo kabla ya 1964 kama Dinosour, maana yake ni kwamba Dinosour mmoja marehemu kafufuka?

  Inanikumbusha zamani wakati hadithi vijijini kwetu zilikuwa zinazagaa kwamba marehemu wamekutwa wanaoga kisimani mchana kweupeeee! Ilinitokea hata mimi live nikiwa mdogo na dada yangu ambaye sasa ni marehemu. Tulienda jioni kuteka maji kisimani, kisima kimefichika inabidi upige hodi kabla hujaingia kule. Tulipofika tulikutana na makelele mengi ya watu wanaooga ambao wanaombana sabuni, sauti za kike mabinti.

  Tukapiga hodi, ghafla sauti zikapotea. Tukapiga hodi ya pili, kimyaaaa! Tukaingiwa na woga maana tulikuwa wadogo. Tukakubaliana tuingie tu. Hatukukuta mtu hata mmoja, tena mawe yaliyopo pale ni makavu kabisa kuashiria hapakuwapo mtu. Tukachota maji haraka na kukimbilia nyumbani mlimani. Tukawasimulia wazazi, nao wakakaa kimya kutusikiliza. Mama akanung'unika kidogo, hatukuelewa kitu. Hatukuchukua mwezi, dadangu akaugua na akaaga dunia.

  Kelele hizi za Zanzibar zinanikumbusha vibaya, niliitafsiri hadithi yangu ile kama ni marehemu kuja kumchukua dadangu, ndio maana hakuchukua time. Je, ina maana marehemu sasa marehemu anaashiria kuja kumchukua Tanganyika wangu tena? Maana Jamhuri ya Zanzibar ilishakufa katika head on collision na Jamhuri ya Tanganyika.

  Hapo sasa patamu kweli!

  Leka
   
 16. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #16
  Oct 30, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Mkuu Pole sana kwa msiba wa dada yako..inasikitisha kweli na hakuna wa kulaumiwa hapo kwani ni kazi ya Mungu naye alimpenda zaidi, lakini kwa msiba wa "dada yako Tanganyika" umlaumu Nyerere...maana aliiuwa na kilichokufa katika "head on collision" ni Tanganyika na si Zanzibar... Zanzibar ipo...Tanganyika haipo(rejea kumbukumbu za G55) na hilo neno "Tanzania" halitokani kabisa na kuunganisha vitu hivi viwili kwa maana kwamba ingelikuwa hivyo basi na Zanzibar isingelikuwapo...so find your sister while we are working on keeping ours.
   
 17. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #17
  Oct 30, 2009
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hiyo kali mkuu! Napokea pole zako kwa moyo mkunjufu. Sasa, ina maana Tanganyika ndio hawezi tena kufufuka? Mbona Mtikila na G55 wamejitahidi kumpa uhai bila mafanikio na ni JKN huyohuyo aliye wafunga kamba kila anayetaka kumfufua msukule Tanganyika? Sasa kwa kuwa Nyerere hayupo tena, kwa nini tusimpeleke msukule Tanganyika kuombewa Kimara? (soma Bungeni).

  Leka
   
 18. m

  maswenga Member

  #18
  Oct 30, 2009
  Joined: Nov 10, 2007
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 15
  Ndani ya nchi, tunatambuana wenyewe kuwa tuna mamlaka mbili tofauti, japo wenzetu huko visiwani mwasema ni nchi kamili. Lakini nje ya nchi tuna taifa moja tu nalo ni Tanzania. Sasa waweza kujitapa sana kuwa "Mungu Ibariki...." sio maarufu Znz, lakini utambulisho wa huo wimbo nje ya nchi ndio unaotufanya tuwe NCHI moja. Ndio wimbo anaopigiwa kiongozi yeyote wa ngazi ya kitaifa aendapo nje ya nchi. Sio tu wimbo, ila pamoja na jeshi, polisi, mahakama, sarafu na hata uwakilishi wa nje (balozi) vyote shina lake ni moja (chini ya serikali ya muungano). Sasa kwakuwa nimetaja jeshi, usianze tena kuhoji vitu kama KMKM au mwingine ataje mgambo, tutakuwa tunarudi nyuma ki-ufahamu!. Ni hayo tu ndugu yangu.
   
 19. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #19
  Oct 30, 2009
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Huenda ndio ule ulevi aliousema JKN, lakini kweli Unguja na Pemba wanaiva chungu kimoja? Au tungojee wimbo mwingine wa Jamhuri ya Pemba? Maana nao wananung'unikia Unguja inawameza.

  Leka
   
 20. d

  dos.2020 JF-Expert Member

  #20
  Oct 30, 2009
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 208
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 45

  Yale mauaji ya 64 ndio yalioleta Jamhuri
   
Loading...