Wimbo wa taifa kwanini hauanzi na Mungu ibariki Tanzania?

bigmash

JF-Expert Member
Apr 8, 2017
416
421
Charity begin at home, ni msemo wa kiingereza uliozoeleka kwamba jambo lolote zuri lianzie kwako kwanza kabla ya kulipeleka kwa jirani/mwenzio.

Sasa turudi kwenye mada yangu ili mnielewe. Wimbo wetu wa Taifa sina tatizo nao hasa kwa vionjo vilivyo ndani yake ni vizuri na vinaeleweka na kukubalika vizuri bila ya kujali asili ya wimbo wenyewe.

Tatizo langu kwenye huu wimbo ni ile beti ya kwanza inayosema MUNGU ibariki Afrika, badala ya kuanza kwa kusema MUNGU ibariki Tanzania. Hapa namaanisha Tanzania ingeanza kwanza kwenye beti ya kwanza halafu beti ya pili itaje Africa na si vice versa.

Unawezaje kumuomba MUNGU awabariki wengine kwanza kabla ya kumuomba MUNGU akubariki wewe kwanza, hii haijakaa sawa. Jiombee wewe kwanza ndipo uwaangalie wenzako na sio kuacha kwako kukiteketea huku ukienda kuokoa kwingine. Mambo mengine tunayaona kama madogo vile lakini impact yake ni kubwa katika maisha ya kila siku na ndio watanzania tunajiuliza kila siku nani katuroga kumbe tunajiroga wenyewe.

MUNGU huyu ataanza kubariki wengine kwanza (kwa kuwa sisi wenyewe tumetaka hivyo) ndipo atugeukie sisi, sasa hapa sijui huyu MUNGU atamaliza lini kuwabariki hawa wenzetu kabla yetu, hapa inabidi tubadilishe jamani.

Nawasilisha.
 
Umefikiria nje ya box, hili ni jambo la kufanyia kazi kwa haraka. Jambo hili nalifananisha na kuweka twiga kama nembo ya taifa. Twiga ni mnyama anayewindwa huko mwituni. Tunahitaji kuweka myama anayewinda wenzake, kama vile MAMBA au PAPA au SIMBA.
 
Tunaanza na Africa kwanza kwani mtazamo wetu ni Africa moja halafu mataifa baadaye. Ndio wigo wa mwanzilishi wetu ulivyokuwa mpana
 
Kwa mjibu wa maandiko matakatifu MUNGU anasema yule anaewaombea wengine na kuwapa kipaumbele wengine anabarikiwa Mara dufu zaidi kuliko yule Anajitanguliza yeye na kujiombea yeye binafs. MUNGU siyo mwendawazimu Awabariki wale uliowapa kipaumbele kuwaombea kisha Akakuacha na kukusahau wewe ambaye ni mfereji wa mbaraka kwa wengine, ndiyo maana hata ktk maisha ya kawaida wakati mwingine hatupokei tunayoyaomba maana tumekuwa wabinafs na kutanguliza Umimi, Tujifunze kwa watumishi wa Mungu Kama Nabii Musa alikuwa anaanza kuwaombea msamaha Wana wa Israel kwanza na shida zao ndo anamalizia na yeye mwenyewe Hivyo mwasisi wa wimbo wetu wa Taifa Alikuwa na maono ya kiroho,Tujifunze kuwaombea wengine automatically tutakuwa tumepokea mbaraka
 
Sisi ni nchi na Taifa kubwa sana ...bado hatujaexplore our potential...siku tukifanikiwa kujua umuhimu wetu kwenye dunia ndio utaelewa maana ya wimbo huu.
 
Mkuu, Mungu akiibariki Afrika na sisi tunabarikiwa pia. Au hujui kwamba na sisi tupo Afrika? Acha uchoyo na ubinafsi mkuu.
 
Tanzania ifutwe katika wimbo wa taifa kwani ukitaja Africa na Tanzania ipo humo humo hivyo haina haja ya kuchoshana na maneno mengi yasiyo na maana
 
Kwa mjibu wa maandiko matakatifu MUNGU anasema yule anaewaombea wengine na kuwapa kipaumbele wengine anabarikiwa Mara dufu zaidi kuliko yule Anajitanguliza yeye na kujiombea yeye binafs. MUNGU siyo mwendawazimu Awabariki wale uliowapa kipaumbele kuwaombea kisha Akakuacha na kukusahau wewe ambaye ni mfereji wa mbaraka kwa wengine, ndiyo maana hata ktk maisha ya kawaida wakati mwingine hatupokei tunayoyaomba maana tumekuwa wabinafs na kutanguliza Umimi, Tujifunze kwa watumishi wa Mungu Kama Nabii Musa alikuwa anaanza kuwaombea msamaha Wana wa Israel kwanza na shida zao ndo anamalizia na yeye mwenyewe Hivyo mwasisi wa wimbo wetu wa Taifa Alikuwa na maono ya kiroho,Tujifunze kuwaombea wengine automatically tutakuwa tumepokea mbaraka
Tuna omba hayo maandiko yaliyosema hivyo ni kitabu gani Biblia, Quran, Bagavd Gita au nini? ... tupe ukurasa, na mstari husika ...
Mkuu nimekuelewa wazo zuri.
 
Tanzania ifutwe katika wimbo wa taifa kwani ukitaja Africa na Tanzania ipo humo humo hivyo haina haja ya kuchoshana na maneno mengi yasiyo na maana
Msihi mbunge wako afikishe muswada Bungeni wa kufuta huo ubeti. La sivyo utabaki kulalamika bila mafanikio.
 
Ni masuala ya kimantiki mkuu.
From the general to the specific
or vice versa. Mama Afrika kwanza nchi moja moja baadaye. Mantiki ya Pan Africanism na muktadha wa maono ya mbali zaidi..
 
Huu wimbo na kuuimba miaka yote bado Afrika masikini, conclusion moja tu, mungu hayupo. So hata waiweke katikati haina msaada wowote bora waifute tu.
 
Hao wengine ni akina nani? Kwani ukisema Africa unakuwa umeiondoa Tanzania? Au wewe unaelewaje?
 
Back
Top Bottom