Wimbo wa taifa kwanini hauanzi na Mungu ibariki Tanzania?

Tunaanza na Africa kwanza kwani mtazamo wetu ni Africa moja halafu mataifa baadaye. Ndio wigo wa mwanzilishi wetu ulivyokuwa mpana

Mtazamo wenu wa kwanza ni Afrika moja?

Kama mnapenda sana umoja kwa nini basi isiwe mtazamo wa dunia moja?

Semeni Mungu Ibariki duniaaa...

Tujue kweli mnapenda umoja
 
Charity begin at home, ni msemo wa kiingereza uliozoeleka kwamba jambo lolote zuri lianzie kwako kwanza kabla ya kulipeleka kwa jirani/mwenzio.

Sasa turudi kwenye mada yangu ili mnielewe. Wimbo wetu wa Taifa sina tatizo nao hasa kwa vionjo vilivyo ndani yake ni vizuri na vinaeleweka na kukubalika vizuri bila ya kujali asili ya wimbo wenyewe.

Tatizo langu kwenye huu wimbo ni ile beti ya kwanza inayosema MUNGU ibariki Afrika, badala ya kuanza kwa kusema MUNGU ibariki Tanzania. Hapa namaanisha Tanzania ingeanza kwanza kwenye beti ya kwanza halafu beti ya pili itaje Africa na si vice versa.

Unawezaje kumuomba MUNGU awabariki wengine kwanza kabla ya kumuomba MUNGU akubariki wewe kwanza, hii haijakaa sawa. Jiombee wewe kwanza ndipo uwaangalie wenzako na sio kuacha kwako kukiteketea huku ukienda kuokoa kwingine. Mambo mengine tunayaona kama madogo vile lakini impact yake ni kubwa katika maisha ya kila siku na ndio watanzania tunajiuliza kila siku nani katuroga kumbe tunajiroga wenyewe.

MUNGU huyu ataanza kubariki wengine kwanza (kwa kuwa sisi wenyewe tumetaka hivyo) ndipo atugeukie sisi, sasa hapa sijui huyu MUNGU atamaliza lini kuwabariki hawa wenzetu kabla yetu, hapa inabidi tubadilishe jamani.

Nawasilisha.

Pengine baraka zikitoka juu,zinaanzia ngazi ya bara na kusambaa nchi moja moja katika nchi zilizoomba baraka hizo kwamba zikitupwa zinatupwa afrika halafu nchi inayozitaka baraka hizo inazivuta kwake,
Ni kama umeme unapozalishwa hauji direct kwako unapita sehemu mbalimbali kwako kunakuwa kwa mwisho,huwezi kuiombea baraka dar es salaam bila kupitia tanzania,

Kama umenielewa sema Ameen!
Kama hujanielewa naomba nikague cheti chako
 
watu wanajadili,chini ya kiwango ase..labda ungesema tutoe ubeti wa kuiombea tanzania,ubaki wa kuibariki africa maana tanzania imo ndani ya africa.
then pia hata katika,hali ya kawaid kuomba lazima uwaombee kwanza wazazi kama ni baba au mama ama familia ndipo unafata kujiombea wew,so ni jambo jema ama utartibu mzuri kumwombea aliyekuumba ukiwemo ndani yake halafu ufate wew.
Mungu ibariki Afrika Mungu ibariki Tanzania? Amin.
 
Kwa mjibu wa maandiko matakatifu MUNGU anasema yule anaewaombea wengine na kuwapa kipaumbele wengine anabarikiwa Mara dufu zaidi kuliko yule Anajitanguliza yeye na kujiombea yeye binafs. MUNGU siyo mwendawazimu Awabariki wale uliowapa kipaumbele kuwaombea kisha Akakuacha na kukusahau wewe ambaye ni mfereji wa mbaraka kwa wengine, ndiyo maana hata ktk maisha ya kawaida wakati mwingine hatupokei tunayoyaomba maana tumekuwa wabinafs na kutanguliza Umimi, Tujifunze kwa watumishi wa Mungu Kama Nabii Musa alikuwa anaanza kuwaombea msamaha Wana wa Israel kwanza na shida zao ndo anamalizia na yeye mwenyewe Hivyo mwasisi wa wimbo wetu wa Taifa Alikuwa na maono ya kiroho,Tujifunze kuwaombea wengine automatically tutakuwa tumepokea mbaraka
Miaka yooote hiyo tunawaombea na hatujabarikiwa cha maana. Tupo kama hatupo vile
 
Mtoa mada unajua kuimba wimbo wa taifa wote? Au hapo tu ndo unapopajua?
 
Umefikiria nje ya box, hili ni jambo la kufanyia kazi kwa haraka. Jambo hili nalifananisha na kuweka twiga kama nembo ya taifa. Twiga ni mnyama anayewindwa huko mwituni. Tunahitaji kuweka myama anayewinda wenzake, kama vile MAMBA au PAPA au SIMBA.

Hata mimi twiga sijarizika nae. Japo kumbuka naye anachungulia wenzake kutokea juu baada ya mwewe kama USA baby. sisi tulitakiwa tuweke Kipanga yule mwewe hatari kwa kwa speed na kunyakua.

harafu pembeni azungukwe na big 5.

Pia tunasahahu bila dunia hakuna Afrika na TZ isingekuwepo
 
Back
Top Bottom