Wimbo wa Sikukuu ya kuzaliwa: Ifike mahali tuwe na wimbo kwa lugha yetu ya kiswahili na Serikali kwa kushirikiana na wadau isimamie jambo hili

Sasa tujiulize,kwa upande wetu sisi watanzania,je,i ni sahihi mpaka leo kusherekea sikukuu ya kuzaliwa huku tukiimba wimbo huu wenye maneno ya kingereza na wakati huo huo tukijinadi kukuza lugha yetu ya kiswahili?

SImple

Tengeneza wa kwako na familia yako imba hakuna mtu atakuingilia kwakuwa siyo jambo la kitaifa
 
Nilivyokiwa kijana wa form IV nilijiuliza mwenyewe kwa nini inakuwa rahisi kutongoza kwa kiingeleza kuliko kwa kiswahili...nikaenda mbali zaidi na kujaribu kutafuta maneno kwa kilugha changu cha kikabila lah nikabakia kucheka mwenyewe.

Sijui tutafanyaje kuikwepa hii lugha wapendwa!
 
Hata ungesema serikali kwa kutumia aliens...bado wazo lako ni la kijuha!

Au kama vipi si umwombe Mange akutungie huo wimbo....

Stupid.
Kumbe upumbavu na ujinga ndio jadi yenu eeh!
Umemuelewa mleta mada au una chuki zako kama kaka yako mtukufu?
 
Tumetawaliwa mpaka hatujielewi kabisa!!!

Eti mnaimba birthday sijui dear nani na mnaono mko sawa tu!!!
Ajabu ni kuwa hao hao wanaokubeza ndio wanao kataa tukisema mtu mwenye digrii tatu kimombo kutokijua ni aibu. Wanasema lugha ya mabeberu sio lazima.
Ila kwenye mada yako kuhusu wimbo tuu kuwa wa kiswahili wanakejeli eti sio lazima! Ajabu sana hii!
 
Nilivyokiwa kijana wa form IV nilijiukiza mwenyewe kwa nini inakuwa rahisi kutongoza kwa kiingeleza kuliko kwa kiswahili...nikaenda mbali zaidi na kujaribu kutafuta maneno kwa kilugha changu cha kikabila lah nikabakia kucheka mwenyewe.

Sijui tutafanyaje kuikwepa hii lugha wapendwa!
Mkuu,hebu jiulize,Raisi wa nchi anasheherekea sikukuu yake ya kuzaliwa na anaalika viongozi wenzake na watu wengine mashuhuru pale Ikulu,then katika kusindikiza sherehe ya kuzaliwa kwake,Raisi na wageni wake wote wanaimba, "happy birthday Mr.President.......".

Swali ni je,hali hii inapendeza ila hali sisi ni waswahili?

Mimi nafikiri kama hatuwezi kuwa na walau wimbo wetu kwa lugh yetu,basi ni bora kusherehekea tukio kama hilo bila kutumia huu wimbo kwani unatufanya hata hawa watu weupe kutudharau japo hawasemi.

Ni bora kuwa na wimbo kwa lugha yetu ambao utakuwa umerekodiwa na ambao unaweza kuwa unapigwa kusindikizi sikukuu hizi za kuzaliwa kuliko hii habari ya kuimba sijui happy birthday dear.
 
Ajabu ni kuwa hao hao wanaokubeza ndio wanao kataa tukisema mtu mwenye digrii tatu kimombo kutokijua ni aibu. Wanasema lugha ya mabeberu sio lazima.
Ila kwenye mada yako kuhusu wimbo tuu kuwa wa kiswahili wanakejeli eti sio lazima! Ajabu sana hii!
Hawa watu wanaongozwa na chuki na si kitu kingine mkuu.

Wanaona sawa kutumia lugha ya kiswahili kwenye shughuli za kimataifa ila hawaoni tatizo kwa watu wazima wakiwemo viongozi kuimba happy birthday kusherehekea sikukuu ya kuzaliwa

In short,tumetawaliwa mpaka hatujielewi/hatushituki.

Ukweli ni kwamba,ukishindwa kuona kasoro katika jambo dogo kama hili,basi huwezi kuona kasoro kwa mambo makubwa.
 
Tumetawaliwa mpaka hatujielewi kabisa!!!

Eti mnaimba birthday sijui dear nani na mnaono mko sawa tu!!!
Ni kwa sababu kuadhimisha siku ya kuzaliwa sio utamaduni wetu. Watu na wanaiga tu na mbaya zaidi siku hizi walivyoiga wanawashinda hata wenye asili ya hii sherehe kwa matumizi na madoido. Watu wanatumia gharama kuuuuubwa huku wakiishi kwenye ufukara uliopindukia wakati wenye utamaduni wa kusherehekea hufanya vitu simple kabisa.
 
Sisi si weusi katika ngozi tu,bali hata katika akili zetu!!
 
Back
Top Bottom