Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 46,998
- 144,329
Tangu nikiwa mtoto mdogo mpaka leo hii nikiwa ni mtu mzima,sijawahi kusikia wimbo ya kusindikiza sikuku ya mtu kuzaliwa(birthday) unaoimbwa kwa lugha ya kiswahili zaidi ya huu tuliouzoea wa kutumia maneno ya kingereza jambo ambalo mimi huwa siku zote naliona haliko sawa japo linaoneekana ni la kawaida tu kwa watu wengi.
Hata katika nchi nyingine za kiafrika,sijui kama nao wana wimbo unaoimbwa kwa kutumia lugha zao za asili au za mataifa yao kusindikiza sikukuu hii na hii inatokana na ukweli kwamba, sikukuu hii ya kuzaliwa haikuwa utamaduni wetu na kama tulikuwa na utamaduni huu,basi wimbo wa kusindikiza sikukuu hii kwa lugha zetu za asili au za mataifa yetu ya kiarika ni jambo ambalo hatukuwahi kuwa nalo(tulikuwa tunasherehekea bila kuimba).
Sasa tujiulize,kwa upande wetu sisi watanzania,je,i ni sahihi mpaka leo kusherekea sikukuu ya kuzaliwa huku tukiimba wimbo huu wenye maneno ya kingereza na wakati huo huo tukijinadi kukuza lugha yetu ya kiswahili?
Labda niulize,hivi wachina,wakorea na hata warusi,nao husherekea sikukuu hii kwa kutumia wimbo huu wenye maneno ya kingereza?
Binafsi nato wito kwa serikali kutangaza donge nono kwa mtu yoyote iwe mtu binafsi,mwanamuziki,bendi ya muziki,n.k atakaeweza kutunga maneno/wimbo mfupi wa kusindikiza siku hii ya kuzaliwa utakaotumia maneno ya kiswahili ili na sisi tuwe na wimbo unaotumia lugha yetu ya Taifa badala ya kuiga kila kitu.
Kama tunaona kutumia kingereza katika mawasiliano yetu ni kutukuza kingereza na kupuuza lugha yetu,basi tujue matumizi ya huu wimbo ni muendeleo ule ule wa kuthamini vya wenzetu na kupuuza vya kwetu.
Labda nimalizie kwa kuuliza, hivi watu mmekaa kama familia alafu kuanzia baba,mama,watoto,ndugu na jamaa mko busy kuimba sijui happy birthday dear nani, hivi huwa hatujishitukii au kuona hili jambo haliko sawa?
In short,hatuoni kuna kasoro katika hili jambo?
Au timu fulani ya wabantu na mashabiki wao kuimba happy birthday pale uwanjani siku ile nako kulikuwa sahihi?