SI KWELI Wimbo wa Nay wa Mitego uitwao Nitasema, umefutwa youtube na yeye hajulikani alipo

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Nimekutana na post katika mtandao wa X ikisema Wimbo wa Nay wa Mitego alioutuoa hivi karibuni umefutwa na yeye hajulikani alipo, je kuna ukweli wowote?

Screenshot 2024-09-25 085957.png

 
Tunachokijua
Emannuel Elibariki maarufu kama Nay wa Mitego ni mwanamuziki wa Tanzania ambaye anafanya muziki wa “Hip Hop’ lakini mara kadhaa pia amekua akitumia sanaa yake ya muziki kufanya muziki wa kiharakati kwa kukemea mambo mbalimbali.

Nay wa Mitego ameshawahi kukamatwa na jeshi la polisi mara kadhaa kutokana baadhi ya nyimbo zake alizokuwa akizitoa. Lakini pia amewahi kuitwa na baraza la sanaa Taifa (BASATA) katika nyakati tofautitofauti kutokana na muziki wake.

Tarehe 23/09/2024 alitoa taarifa kuhusu kazi yake mpya ya muziki atakayoitoa ikujilakana kwa jina la Nitasema Na tarehe 24/09/2024 alitoa wimbo huo ambapo ndani yake ameongelea mambo tofautitofauti ikiwemo yaliyotekea nchini.

1727245144165-png.3106021
Imekuwepo taarifa ikieleza kuwa wimbo wa Nay umefutwa katika mtandao wa Youtube na yeye mwenyewe pia hajulikani alipo.

1727245233952-png.3106024

Ukweli upoje?

JamiiCheck imefuatilia taarifa hiyo na kubaini kuwa taarifa hiyo ni ya uzushi kwani video hiyo haijafutwa katika mtandao wa youtube lakini yeye mwenyewe pia kupitia mtandao wa instagram ali post kuonesha kuwa wimbo huo upo Youtube ukiwa nafasi ya kwanza kwenye trending, pia ameonesha kwamba wimbo huo upo kwenye mitandao mingine ya muziki.

Aidha, hakuna taarifa zozote kutoka kwenye vyanzo vinavyoaminika wala ndugu au jamaa wa msanii huyo walioripoti kutoweka kwa Nay wa Mitego hali inayothibitisha kuwa taarifa hiyo ni ya uzushi.

Pia kwa kupitia utafutaji wa kutumia keywords “Nay hajulikani alipo” kama maneno yanayopatikana kwenye ujumbe huo JamiiCheck haijapata taarifa inayofanana na hiyo katika vyanzo vingine.
Asanteni kwa taarifa..

Na hii inashangaza kwa sababu BASATA au serikali inaweza kufanya lolote juu ya msanii huyu..

Lakini kuufuta wimbo kwenye platforms mbalimbali kama YouTube, Instagram nk, hawawezi isipokuwa wanaweza kuzuia usipigwe/rushwe kwenye local media pekee...
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom