Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,787
- 30,084
SALUM ABDALLAH NA CUBAN MARIMBA CHACHA BAND NYIMBO ''MKONO WA EID''
Sikumbuki ilikuwa kitu gani lakini ninachokumbuka ni kuwa nilikuwa likizo Tabora niko uani na bibi yangu Zena bint Farijala mwaka wa 1965 na ni muda mfupi toka Salum Abdallah amefariki.
Nadhani ilipigwa nyimbo ya Salum Abdallah katika radio bibi akaniona nimeifurahia ile nyimbo ndipo akaniambia, ''Salum Abdallah alikuwa rafiki sana ya baba yako. Akija Tabora na bendi yake lazima aje hapa nyumbani kumsalimu baba yako.''
Bila shaka hii ilikuwa katika miaka ya 1950 wakati Salum Abdallah anaanza muziki wake.
Siku moja nilimuona Salum Abdallah Mtaa wa Stanley na Nyamwezi, mbele ni Mtaa wa Swahili.
Hapo ndipo ilipokuwapo Cuban Marimba Chacha Band Branch.
Nimemkuta Salum Abdallah amekaa ndani na mwenzake, Salum Abdallah kashika guitar anapiga.
Yule mwenzake aliyekuwanae pale jina lake anaitwa Almasi maana nilimsikia Salum Abdallah akimwita kwa jina hilo.
Ilikuwa mwaka wa 1964.
Sikunyanyua mguu.
Nilibakia pale nimesimama nasiikiliza muziki waliokuwa wakipiga.
Mwaka uliofuatia Salum Abdallah akafariki.
Salum Abdallah kwa sisi tuliozaliwa katika miaka ya 1950 tunamkumbuka kwa nyimbo ya ''Mkono wa Eid.''
Miaka ili ilikuwa baada ya tangazo la radio la kuandama mwezi likitanguliwa na takbira mwanzo na mwisho kinachofuatia ni nyimbo ya Salum Abdallah, ''Mkono wa Eid.''
Ikiwa umepata kusikia muziki wa Septet Habanero bendi iliyokuwa maarufu sana Cuba na muziki wake ukipigwa katika Sauti ya Dar es Salaam katika miaka ya 1950 utangazaji wa radio ulipoanza, utagundua kuwa upigaji ala wa Cuban Marimba na uimbaji wa Salum Abdallah na uitikiaji wa ''chorus,'' vimeshabihiana sana.
Nyimbo inaanza kwa trumpet ambayo imetiwa ''mute,'' ili itoke sauti kali nyembamba iliyojaa ''treble.''
Salum Abdallah anaingia kuimba kisha anafuatiwa na waitikiaji.
Marehemu mama yake Salum Abdallah alikuwa kila inapofika Eid na kumsikia mwanae akiimba nyimbo hii alikuwa akilia.
Allah awarehemu wote.
Amin.