Wimbo mpya wa Ali Kiba 'KADOGO': Toa Maoni na ushauri wako hapa

Msanii anayejitabainisha kama King wa Muziki Tanzania, Ali Kiba ametambulisha ngoma yake mpya rasmi leo akiwa kwenye kituo cha Redio kinachopenda kumbeba kwa gharama yoyote 'Clouds FM'.

Ngoma hiyo inakwenda kwa jina la 'KADOGO' na inatarajiwa kupakiwa kwenye mtandao wa YouTube leo ALHAMISI kama masharti ya mtaalam yanavyomtaka.

Kwa wale msiojua ni kwamba Ali Kiba ana masharti ya kuweka nyimbo zake Youtube siku za ALHAMISI tu na yeye amewahi kukiri baada ya kupakia wimbo wa ''HELA'' na kushambuliwa na mashabiki zake kutoa ngoma ya hovyo.

Katika utetezi wake alisema alikosea masharti labda ndio maana alishambuliwa sana, na baadaye aliipakia upya ngoma hiyo siku ya ALHAMISI na kelele hazikusikika sana.

Kila La kheri King Kiba. Yooooo... Pop it up ''Papiri papiri'
Acheni utani basi jamani yaani mnaaminishwa na clouds kuwa alikiba ni mfalme wa bongo fleva kwa kipi alichofanya tangu aanze muziki?au ameifanyia nini Tanzania kimataifa au wasanii wenzake?maana mm najua hata hata ukiwa sehemu yoyote duniani ukitaja bongo fleva basi utaulizwa kuhusu diamond platnumz basi maana ndie ambae kila tuzo za kimataifa zikitangazwa yupo hata mwaka huu kitu ambacho alikiba cjui Mara ya mwisho alitajwa wapi na hata wakitajwa pamoja labda yesu ashuke kibakuli kupata nafasi ya juu ya mondi kwenye tuzo,na ndani ya nchi kuna kina dully Sykes,angalau huyo anastahili kwa Kuanzisha hii fleva,acheni kumpamba uyo jamaa pacha wa bush man wa God's must be crazy.asante ila muache roho mbaya za unafiki yaani mnakera kulazimisha mkaa kuwa mweupe.
 
M nlshamkimbia uyu jamaa nau nko WCB, any wei ngoja tuone ngoma hii na ya darasa ipi itakimbiza...
 
Dah ngoma mbovu kishenz alafu ulivyo mpuuz unaisifia tu

Huyu jamaa ataachaga lini kuimba mapambio?
 
Huyu kiba mnakingia kifua na kumdekeza sana...

Ila ukweli ni kuwa huyu jamaa ni mzembe sana katika mziki wake kwa sasa, na tokea diamond ashike usukani amekuwa ni mtu wa kupenda kubebwa bebwa sana na kutegemea mashabiki wamtetee ila ubunifu siku hizi ni zero kabisa....
 
Back
Top Bottom