Wimbo kwa Mzee Mwanakijiji, Dr. Slaa na wapiganaji wengine | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wimbo kwa Mzee Mwanakijiji, Dr. Slaa na wapiganaji wengine

Discussion in 'Entertainment' started by Sikonge, Aug 19, 2009.

 1. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #1
  Aug 19, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Nimekuwa mpenzi mkubwa sana wa nyimbo za marehemu Roger Troutman. Kwa wale vijana wa zamani watakuwa wanazifahamu nyimbo zake za Computer love na I want to be your man. Siku moja nilishangaa kusikia anaimba na hawa waimbaji wa Gospel. Nilikuwa na cd yao ila sikufahamu kuwa Roger aliamua kuongeza kinanda chake (Talk Box) na kuufanya huu wimbo ubadilike kabisa.
  Kwa vijana wa miaka ya 2000, Roger ndiye aliweka ile sauti ya talk box kwenye wimbo wa Tupac wa Carfonia Love, Johnny Gill (your body), Keith Sweat (Put your lovin' through the test) na nyingine nyingi.

  Leo nakuleteeni huu wimbo kwa wale wote wanaokata tamaa kuhusu mapambano ya kuibadilisha Tanzania. Na kwa mafisadi na wapambe wao wote lazima MSIKILIZE maneno mazito yaliyo kwenye huu wimbo kuwa THE CHANGE IS COMING - Just hold on......
  Sorry kwa watu mlio na speed ndogo za kuangalia Youtube. Someni tu walau maneno na tuendelee na VITA ya mabadiliko. Mungu Ibariki Tanzania.

  [ame]http://www.youtube.com/watch?v=tlBvVbhDpRA[/ame]


  Live version:
  [ame]http://www.youtube.com/watch?v=Av9OoWJfxNA&feature=related[/ame]

   
 2. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #2
  Aug 19, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Duu, hapa ntakuwa nimefanya makosa sana kutowaweka watu kwa majina yao:-

  1. Maxence Melo - Kazi yako kubwa sana mkuu katika kuleta Mabadiliko.

  2. Mkuu Field Marshal ES, somo na kazi yako yaonekana ...... Keep going.

  3. Game Theory na Dilunga ....... kwa ZERO TOLERANCE.......

  4. ......................................... (Mwaweza ongeza wengine).
   
 3. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #3
  Aug 19, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Unaonekana kijana sikonge ni mtu unaependa kujipendekeza pendekeza.........thread haina kichwa wala miguu....Mods pls do some
   
 4. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #4
  Aug 19, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Na wewe je? Mbona umekaa na Kifront front saaana. Kulialia kwa Mods mtu mzima na tena umeowa Msukuma ni aibu hiyo.

  Ngaja nimpigie simu dada yangu awe anakuzaba makofi mbele ya kadamnasi ya watoto wa Kike. Na ukizabwa makofi huko, usianze kulia "Mama weee, Invisible nakufa mie, niokoe...". Hapo mie ntakuwa nazidi kumpa maneno dada yangu "mtandike sasa la kifuani kama Hogan".
   
 5. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #5
  Aug 19, 2009
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,896
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  1. Maxence Melo - Kazi yako kubwa sana mkuu katika kuleta Mabadiliko.

  2. Mkuu Field Marshal ES, somo na kazi yako yaonekana ...... Keep going.

  3. Game Theory na Dilunga ....... kwa ZERO TOLERANCE.......

  4. Shapu......................................... Havumi lakini yumo msimwache.

  5........................................................(Mwaweza ongeza wengine).
   
 6. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #6
  Aug 19, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Sikonge umedata!

  Lakini these younguns wanamjua T-Pain and them, hao kina Roger Troutman na Sam Cooke waulize kina Rev. Kishoka huko.

  wenzetu wamesema change gon' come mpaka wamemuweka Obama White House. Chaellenge hiyo kwetu.

  Real Talk.
   
 7. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #7
  Aug 19, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Bluray,

  Heshima yako kwanza.

  Unafahamu hawa vijana wetu wa leo wanavamia vitu kwa na kuvimeza bila hata ya kutafakali. Ukiwauliza wanamuziki kama hawa watasema wao hawawafahamu. Ila hao akina T-Pain wenyewe na akina Wayne wadogo (Lil Wayne) ingawa mdogo huyo kajichora mwili mzima. Nilimwonyesha kijana mmoja BET music award ya mwaka jana. Alipokuja kuimba Al Green, walionyesha hao akina T-Pain, Sean John, Lil Wayne nk wakiimba wimbo wake na wakiwa wanayafahamu maneno vizuri sana. Huwezi kusema unapenda R&B na mtoto wake RAP au Hip hop wakati huo hao wazee wenyewe waanzilishi huwahafamu.

  Ukija kwenye ujumbe wenyewe, nashukuru kuwa umeona maneno mazito yaliyopo ndani ya wimbo, tofauti na Yo Yo ambaye yeye kaona eti najipendekeza. Mie nina imani kuwa kuna mabadiliko yatakuja. Hili joto linalofukuta lazima kuna kitu kitapikika. Kibaya ilikuwa kama wakati wa Nyerere wakati tulikuwa tumelala na hakuna hata anayesema. Mgomo wa madereva pale Dar juzi, migomo ya wanafunzi, wafanyakazi nk ni dalili kuwa watu wanazidi kupata mwamko. Kuwepo kwa JF tu kumetufungua macho watu wengi sana.

  Champions wa mabadiliko haya tuombe Mungu wasife moyo au wasiangukie kwenye DARK SIDE kama Mzee Mzindakaya (Mzee wa Mabomu) aliyepelekwa kwenye dangulo la Ufisadi na Mkapa na kutoka hapo Mzee wa Kifipa Kaufyata fyataaaaaa!!!!!!.

  Kila kitu huwa kina mwanzo na mwisho.
   
 8. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #8
  Aug 19, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Unfortunately, watu wengi hawamjui Mzindakaya; huyu bwana maisha yake yote amekuwa mamluki ambae alikuwa anatumiwa na wenye fedha kuwaangusha maaduizao. Alitumiwa na maadui wa Iddi Simba kummaliza kisiasa; lakini alikuanafanya hivyo akitumia ubunge wake kama kitega uchumi[ he was doing it for a FEE], kwa misingi hiyo basi sidhani kama anastahili kuitwa mpambanaji wa kiwango cha wakina Slaa!
   
 9. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #9
  Aug 20, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Mkuu Bulesi,

  Sasa wewe unazidi kunikatisha tamaa. Yaani yale mabomu alikuwa anapewa alipue wapinzani wa watu? Nilifikiri alikuwa akiyachimba mwenyewe kwa faida ta Taifa. Hebu mwaga data zaidi ya huyu FISADI. Nilifikiri jamaa kabadilika mwishoni kumbe ni tangu siku nyingi?
  Naamini sasa maneno ya jamaa yangu mmoja asemaye "USIMWANI MWANASIASA".
   
Loading...