Wimbo Kijiwe Nongwa wa ROSTAM na Nay wa mitego ni noma

hooligan01

JF-Expert Member
Nov 21, 2013
662
523
Humo ndani wameimba kimafumbo wamewataja wafuatao:-
Mondi bin la deni
Lowassa
Dogo janja
Uwoya
Zari
Tanasha
Amber ruty
Shilole
Gwajiboy
Uchebe
Amunike
Mzee wa liqwidi
Ruge
Lissu
Wema sepetu
Ila wamewataja kimafumbo...take your time kuinjoy nyimbo na kuwarecognize

====

Wimbo: Kijiwe Nongwa wa ROSTAM Feat NAY WA MITEGO

Alikuja kama Masii tukamchangia sadaka Tukamwona nabii aliyeshushwa siku ya pasaka Tukamtolea na zaka ili kanisa lijengwe Eeh-eh na bado wakamlaza nabii kifo cha mende Hivi unamkumbuka babu?

Babu wa Loliondo Ah-ah yule mfugaji mwenye beach la kikogo Watu wamekufa, watu wamefungwa, watu wamepoteza biashara Sasa umekaribia uchaguzi amerudi chama tawala Vipi dada yetu wa Ihunga, simwoni udangani Ah mbona ashapata mchumba sio viben 10 wa zamani Yule fundi gereji chawa, si kamateka bibiye Na wamefungua mkahawa, yaani wote mama ntilie Na kuna dem aliyeachiwa mtoto akaolewa na mtoto Akaachana na mtoto akabaki anamlea mtoto Hizi ndoa za mjini bwana, zinasikitisha Eeh wanaofungiwa chumbani nauvunjikia --

So soka la Bongo linakwama wapi?

Tifwefu maanake nini Tanzania football failure, ndo nacho jua mimi Unamfukuzaje Hamunike ili udhaifu wenu umvuge Wakati mlimpeleka mlevi akacheze na mavude

Nasema leo hakilali kiporo, imeshakuwa kero Ukuta tunavunja kwa tindo Wameshapigwa guu wako telo Na kiki za kikolo Majita tushapiga kishindo Hili ni fagio la chuma Linang'oa visiki Safisha vichaka kwa moto

Simba kageuka duma Jangwa halipitiki Ukitufuata we toa boko Marehemu alimsema mnyonyaji, kwani mziki una maziwa?

Sasa Mungu kamhitaji na bado hajafanikiwa Hivi unadhani ndani ya mjengo nani ataliziba pengo? Wacha maisha yaendelee, jasiri ameumaliza mwendo Aliyeokota almasi mchangani alikuwa Miss Tanzania Na aliyekuja inunua dukani ni mganga aliyekuwa na nia Ya dhati la pakato akatokea mara mia Akawatumia ila mwamba ni mnyanyasaji wa kijinsia Sa skiza man hii--

my one Ah tupo tupo tu ila hatupo ka zamani Nawe vipi kwani, mbona wife simuoni nyumbani Hey chill man, sina majibu deal done Mbungeni daily majanga, viongozi wameishiwa mada Hivi mbunge wako wa Tanga hoja zake unaziskiaga? Sa nitazisikiaje?

Na ana spika mbovu za wana kijiji Ila fundi wao anakuja soon kutoka Ubelgiji Na Bi Tito na Dr Shika, tayari wamesahauliwa Mwenzao Mariamu, biriani anapika anapakuliwa Bongo bwana, ndo nchi inayosupport ujinga Utashangaa Amber Rutty kala shavu la babu Gwajima Yaliyosemwa yamesemwa Kazi kwenye mmezoea kutema Wakitaka tuwatafte tena Waambie muda sio rafiki mwema (Yeiye iyee )

Kusema kweli hatuchoki Na kwenda jela hatuogopi Tutabanana ata kama hapatoshi Hatupindishi ata kwa dumba Nasema leo hakilali kiporo, imeshakuwa kero Ukuta tunavunja kwa tindo Wameshapigwa guu wako telo Na kiki za kikolo Majita tushapiga kishindo Hili ni fagio la chuma Linang'oa visiki Safisha vichaka kwa moto Simba kageuka duma Jangwa halipitiki Ukitufuata we toa boko
 
Soka la bongo linakwama wapi, TFF Maana yake nini?, ameuliza Stamina kwenye line ambayo Roma amejibu kwa kusema TFF ni Tanzania Football Failure. Kama ulikuwa haujui Rostam wamerudi kwenye spika zako na brand new hit ‘Kijiwe Nongwa’ ambayo ni kolabo yao ya kwanza na true boy Nay Mitego.
Sio TFF tu ambao wametupiwa shot kwenye wimbo huu ulioachiwa siku ya Alhamisi, Septemba 19,2019, Watu wengi wamefikishiwa meseji zao na moja kwa moja tunaweza kuelewa Rostam na Nay Wa Mitego wamewaambia nini kina nani. Kijiwe Nongwa ni wimbo wa Hip-Hop uliotengenezwa na Bin Laden pamoja na Mr. Ttouch, wimbo huu umebeba stori nyingi ikiwemo ya mastaa wawili waliowahi kutrend na ndoa yao ambapo tofauti ya umri wao iligeuka gumzo, Mwanamke alikuwa ni mama wa mtoto mmoja ambaye baba yake alifariki, na mwanaume aliyekuja kumuoa mwanamke huyo alikuwa ni mdogo kiumri.
chukua point hiyo fananisha na mistari hii
”na kuna demu aliachiwa mtoto
akaolewa na mtoto,
akaachana na mtoto
akabaki anamlea mtoto” (Roma amejibu kauli hii huku anacheka).
Ukiunganisha matukio unakumbuka kuhusu ndoa hiyo ambayo imevunjika na kila mmoja anaendelea na maisha yake.Unataka kujua ni Kina nani hao?, bila shaka hawa ni Irene Uwoya na Dogo Janja ambao inasemekana sasa hivi haziivi tena.
Vipi dada yetu wa igunga, simuoni udangani?
Mbona ashapata mchumba sio vibenten wa zamani,
Yule fundi gereji chawa si kamteka bibie,
na wamefungua mgahawa yaani wote mama ntilie,
Tukirudi kwenye line hizo hapo juu tunakutana na Boss wa ShishiFood Shilole na mume wake Uchebe ambaye ameziba nafasi ya Vibenten kwa mrembo huyo mwenye asili ya Igunga Tabora, nani kibenten wa shilole?, aliwahi kuwa Nuh Mziwanda au kuna mtu mwingine?.
Shot nyingine zimeelekezwa kwa Diamond Platnumz na wapenzi wake, Wema Sepetu ni Miss Tanzania aliyeokota almasi mchangani wakati Zari ni mganda aliiyekuja kuinunua dukani kwa nia ya dhati, lakini hawa maharamia waliojitekeza hapa kati huyu mwamba akawanyanyasa kijinsia ni kina nani?.
Tukiachana na Diamond na watu wake Roma na Stamina wamegusia ndoa zao kwa kuulizana maswali na kupeana majibu yasiyoeleweka. Kwenye dakika ya 02:01 ya ‘Kijiwe Nongwa’, Stamina anauliza ‘sa sikiza man, vipi shem mama Ivan?, Roma anajibu, ‘aah tupo tupo tu ila hatupo kama zamani, na kuuliza Nawe vipi kwani mbona wife simuoni nyumbani? Stamina anajibu kwa kusema, ‘hey chil man, sina majibu, deal done’. Tunachofahamu KUHUSU Roma na mke wake hatujasikia mgogoro licha ya mwenyewe kusema hawapo kama zamani, hatujui wanapitia nini, Tukirudi kwa Stamina tunakosa majibu tunaposikia “sina majibu , deal done”. Stamina anatuambia vitu viwili hapa moja ni kwamba yeye na mke wake wanapendana kiasi hawezi kujibu chochote au deal done kwa maana ya kwamba wamemalizana na ndoa imeishia hapo?,
Wengine ambao shot zao zimepigwa kwao ni wale waliowahi kumsema vibaya marehemu, Rostam wametukumbusha kuhusu Ruge na wanamuziki waliokuwa wakitofautiana. Roma anaanza kwa kuuliza Marehemu walimsema mnyonyaji kwani muziki una maziwa ?, Stamina anapokea mstari huo kwa kusema ‘ sasa mungu kamuhitaji na bado hawajafanikiwa , Stamina anaendelea kuuliza ‘ hivi we unadhani ndani ya mjengo nani ataliziba pengo? . Sad stori ni kwamba ndani ya mjengo hakuna atakayeziba pengo hilo kutokana na kauli ya Roma inayosema ‘acha maisha yaendelee jasiri ameumaliza mwendo’.
C.E.O wa FreeNation Nay wa Mitego kama kawaida yake ametembea na korasi ya kibabe, unaweza kuimagine mzuka wa Nay kwenye kolabo na Rostam ni mwendo wa kuongea ukweli tupu.
Kama kuna kitu Rostam hawatakiwi kukosea ni kuacha kutembea Nay Wa Mitego kwenye perfomance za ‘Kijiwe Nongwa’, kolabo hii inatakiwa kutendewa haki na watatu wote hawa wote kwa pamoja kwani kama ni Chemistry, hii ipo lit.

Credit :GP
 
alikuja kama masihi tukamchangia sadaka, tukamuona nabii aliyeshushwa siku ya pasaka, tukamtolea na zaka ili kanisa lijengwe, na bado akamlaza muumini kifo cha mende....
hivi ni mlevi gani alienda kucheza namba ya mkude timu ya taifa..
 
sasa hivi vitaarabu ndio unatuletea wanaume tujadiri?
 
Back
Top Bottom