Wimbo huu unavuma sasa.................. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wimbo huu unavuma sasa..................

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Eeka Mangi, Feb 14, 2011.

 1. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #1
  Feb 14, 2011
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Nimekuwa nikisikiliza nyimbo mbalimbali za hapa nchini lakini kuna huu unanivutia zaidi!
  Naaam unanivutia maana kila uchwao una kibwagizo kipya, wimbo huu sio kama BG za mchina ni zile origino. wanapenda kuuimba sana wabunge na zidi mawaziri wetu hughani kwa hisia na mashairi yenye kuleta hamasa. Naam wimbo mtamu ka nini.
  Hebu nasi tuongeze mashairi yetu kwenye hiki kibwagizo!

  Naanza
  Mgao huu wa umeme utatufikisha wapi!
  Tangu nizaliwe sikuwahi kuuona umeme,
  Niliusikia tu huko mjini kuna umeme
  Unazalishwa kwa maji hata sikuelewa nini maana ya umeme

  Kuja mjini nikajua umeme,
  Lakini umeme huu ni wa mgawo
  Nilizoea mgawo wa unga wa yanga
  na sasa hata mgao wa umeme

  Nyimbo zingine ziliimbwa
  Zikachuja zoote
  Tulipoanza bongo fleva
  Ikazaliwa richmond
  bahati mbaya rich ikafa

  Naskia alimrithi dowa wa nzi
  huyu kataka tumlipe
  wakubwa wamekaa nao hawasemi
  Kiranja naye ananung'unika kwa nini walipwe
  aseme tu kuwa hatulipi yaishe,,,,,,,,,,,,,,,,,,
   
 2. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #2
  Feb 14, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Haha haa! Wimbo huu wimbo gani?
  Hata me unanitatiza
   
 3. Eeka Mangi

  Eeka Mangi JF-Expert Member

  #3
  Feb 14, 2011
  Joined: Jul 27, 2008
  Messages: 3,182
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Mgawo wa umeme mpaka lini. kwa nini wimbo usiishe tu tangu asubuhi mpaka tunaenda kulala waimbwa tuu?
   
 4. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #4
  Feb 14, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Ni taarab, dansi, reggae, hiphop au bongo fleva??
   
 5. mwana wa mtu

  mwana wa mtu JF-Expert Member

  #5
  Feb 14, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 220
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mhhh..huo nao kweli ni wimbo..nachelea kusema kuwa unaweza usichuje...ukaimbwa daima, labda kama kutakuwa na UMMA wenye kuweza kutaka na kutenda ili wimbo uchuje...
   
Loading...