Wimbo ''Happy'' wa Pharrel Williams wawasababishia matatizo Iran

Status
Not open for further replies.

maroon7

JF-Expert Member
Nov 3, 2010
11,050
14,931

Kikundi cha mashabiki wa muziki nchini Iran walioiga wimbo maarufu wa mwanamuziki maarufu wa Marekani Pharrell Williams, 'Happy' wamejipata matatni baada ya kukamatwa na polisi.

Kanda ya video waliyoirekodi wakiiga wimbo huo, inaonyesha vijana watatu na wanawake kadhaa ambao hawakuwa wamejitanda mitandoa, wakicheza densi kwenye barabara za nchi hiyo na kwenye paa za nyumba mjini Tehran.

Mkuu wa Polisi, Hossein Sajedinia, alisema kuwa kanda ya video inayoonyesha vijana hao wakicheza, imekiuka maadili ya jamii.
Kituo cha televisheni ya serikali kilionyesha vijana hao wakikiri makosa siku ya Jumanne.

Inaarifiwa maelfu ya wananchi wa Iran wamekamatwa katika miaka 35 iliyopita wakisherehekea na kujiburudisha kwa mambo ambayo serikali inaona kama ya kukiuka maadili.

Hata hivyo vijana hao wanaosema ni waigizaji wanadai kuwa walihadaiwa kushiriki katika kanda hiyo na watu waliokuwa wanatafuta waigizaji wakisema ulikuwa kama mtuhani kwao.

140521090010_iran_happiness_video_512x288_getty_nocredit.jpg

Wamekiuka maadili'
Kulingana na taarifa ambazo bado hazijathibitishwa, watu 13 walikamatwa kuhusiana na kanda hiyo, ingawa idadi kamili ya waliokamatwa haijatangazwa rasmi.

Pharrel aliyeteuliwa kwa tuzo la Oscar kwa wimbo wake huo mwaka huu ambao umekuwa maaruufu sana duniani, alielezea kukasirishwa na hatua ya vijana hao kukamatwa.

"yani siamini kama watoto hawa walikamatwa kwa kujaribu kueneza furaha,'' alisema Pharrell katika ukurasa
wake wa Facebook.
140521092657_happy_512x288_bbc_nocredit.jpg

Chini ya sheria za kiisilamu, sharti mwanamke ajitande kutoka kichwani hadi katika viganja vya mguu.

Polisi ambao jukumu lao ni kuhakikisha kuwa sheria ya mavazi inafuatwa, hushika doria mara kwa mara katika barabara za mji mkuu Tehran.

Kanda hiyo ya "Happy we are from Tehran" ilionekana kwenye mtandao wa Youtube tarehe 19 Mei na kufikia sasa imetazamwa mara 40,000.

Baadhi wametuma ujumbe wa kukejeli serikali ya Iran wakisema kuwa Iran ni nchi ambako ni hatia kwa mtu kuwa na furaha.

Wimbo halisi wa Pharrell 'Happy' umepelekea maelfu ya watu kote duniani kuiga video ya wimbo huo na kutengeza video zao wenyewe. Kutoka Kenya, Marekani , Uingereza yaani nchi nyingi duniani tu, watu wameiga video hiyo kwa kutengeza yao wenyewe.

Chanzo:
BBC

=================

Hukumu iliyotolewa

Watu sita nchini Iran waliokamatwa baada ya kuonekana kwenye kanda ya video iliyokuwa inaiga wimbo wa 'Happy' wake mwanamuziki mashuhuri Pharrel Williams, wamehukumiwa kifungo cha hadi mwaka mmoja jela kila mmoja pamoja na adhabu ya kuchapwa mijeledi 91.

Wakili wa sita hao amesema kuwa hukumu hiyo itaahirishwa kwa miezi sita ikmaanisha kuwa watafungwa tu jela ikiwa watarejelea kosa hilo. Kanda hiyo inaonyesha wanaume watatu na wanawake watatu ambao hawajafunika vichwa vyao wakicheza densi kwenye barabara na katika paa za nyumba mjini Tehran.

Kanda hiyo iliyowekwa kwenye mtandao wa kijamii wa You Tube, imetazamwa na zaidi ya watu milioni moja. Wengi wa waliohusika kuitengeza kanda hiyo, walifungwa kwa miezi sita , huku mmoja wao akifungwa kwa mwaka mmoja, alinukuliwa akisema wakili wao Farshid Rofugaran.

Mmoja wa watu waliokamatwa kwa kucheza densi
Kanda hiyo kwa jina, "Happy we are from Tehran" ilifikishwa kwa maafisa wakuu nchini Iran mwezi Mei baada ya kutazamwa na watu 150,000 kwenye You Tube.

Waliohusika pia walikamatwa na kushitakiwa kwa kosa la kukiuka sheria za kiisilamu ambazo zinawazuia wanaume kucheza densi na wanawake na pia wanawake kutoka nje bila hijab.

Baadaye washukiwa walionekana kwenye televisheni wakijitetea kwamba wao ni waigizaji walihadaiwa kushiriki katika kanda hiyo Kukamatwa kwa vijana hao kulizia ghadhabu kutoka anga za kimataifa huku watetezi wa haki za binadamu

wakianzisha kampeni kwenye mitandao ya kijamii kutaka waachiliwe.

Mwanamuziki Paharrel Williams mwenyewe, ambaye wimbo wake huo, uliteuliwa kwa tuzo la Oscar,pia alieleza kukerwa na kukamatwa kwa watu hao.

Chanzo: BBC
 
Last edited by a moderator:
non-secular state hiyo, sheria kama hizi inabidi tuziangalie afu tuwaache kama walivo, say anything watu wataanza kukupa majibu ya ajabu ajabu...
 
because am happpppppppyyyyyyyyyy

Clap along if you feel like a room without a roof
Because u're happy
Clap along if you feel like happiness is the truth
Because u're happy
Clap along if you know what happiness is to you
Because u're happy
Clap along if you feel like that's what you wanna do
 
Clap along if you feel like a room without a roof
Because u're happy
Clap along if you feel like happiness is the truth
Because u're happy
Clap along if you know what happiness is to you
Because u're happy
Clap along if you feel like that’s what you wanna do

it might seem crayz what am about to say
sunshine she is here you can take a break
 
Hit single ya ‘happy' ya Pharrell Williams ni single ambayo ukiangalia kwenye mtandao watu wengi walitengeneza video zao na kuziweka humo lakini kwa kutumia wimbo huohuo ambao kiukweli wanasema ni wimbo uliovunja rekodi kwenye nchi ambazo hata hakuwahi kuifikia hiyo rekodi.

Kama ilivyotokea kwa mataifa mengine, mashabiki sita wa Pharrell nchini Iran waliamua kutengeneza video yao wakiwa ni wasichana na wavulana na baada ya kuirekodi wakaiweka kwenye mtandao.

Iran ikiwa ni nchi ambayo ina sheria zake kazi ikiwemo za dini zinazobana, iliwachukulia hatua kwa kuwakamata wote sita walioonekana kwenye video hiyo ambapo mkuu wa Polisi Tehran Hossein Sajedinia alithibitisha hilo na kwamba baada ya video kusambaa walianzisha uchunguzi uliofanikishwa watu hao sita kukamatwa baada ya saa sita.

Mkuu huyu wa Polisi amewaonya vijana wa Iran kwamba yeyote atakaekwenda kinyume na taratibu au kanuni za nchi na dini atakamatwa kama ilivyotokea ambapo CNN walisema moja ya makosa yaliyofanya watu hao kukamatwa wakiwemo wasichana ni kucheza kwa kushikana na pia kuacha wazi nywele na sehemu nyingine za mwili.

Baada ya watu hawa kukamatwa walikiri kwamba haikua lengo lao kuiweka hiyo video online ambapo mwingine alisema walitokea kwenye video ikiwa ni sehemu ya mazoezi ya kuigiza kwenye TV.

Baada ya kukamatwa kwa watu hao sita Mwandishi wa habari wa Iran Golnaz Esfandiari aliandika ‘Iran ni sehemu ambayo ukiwa na furaha unakamatwa'

Tweet ya Pharrell
Screen-Shot-2014-05-22-at-12.02.01-PM.png

Hata hivyo taarifa za saa kadhaa zilizopita zinasema watu hawa inaaminika wameachiwa kwa dhamana baada ya kuchukua headlines iliyoanzia kwenye kituo cha taifa cha TV ambapo walihojiwa camera zikichukua picha kutoka migongoni mwao, yaani hawakuonekana sura.

Mmoja wa sita hao walikua wameshikiliwa aitwae Taravati alipost kwenye Instagram na kummention Pharrell kwa kusema ‘hI, nimerudi… asante sana Pharrell na kila mmoja alietujali nawapenda wote sana na niliwamiss'

Credit: Millardayo

Video yenyewe hii hapa,

Last edited by a moderator:

Watu sita nchini Iran waliokamatwa baada ya kuonekana kwenye kanda ya video iliyokuwa inaiga wimbo wa 'Happy' wake mwanamuziki mashuhuri Pharrel Williams, wamehukumiwa kifungo cha hadi mwaka mmoja jela kila mmoja pamoja na adhabu ya kuchapwa mijeledi 91.

Wakili wa sita hao amesema kuwa hukumu hiyo itaahirishwa kwa miezi sita ikmaanisha kuwa watafungwa tu jela ikiwa watarejelea kosa hilo. Kanda hiyo inaonyesha wanaume watatu na wanawake watatu ambao hawajafunika vichwa vyao wakicheza densi kwenye barabara na katika paa za nyumba mjini Tehran.

Kanda hiyo iliyowekwa kwenye mtandao wa kijamii wa You Tube, imetazamwa na zaidi ya watu milioni moja. Wengi wa waliohusika kuitengeza kanda hiyo, walifungwa kwa miezi sita , huku mmoja wao akifungwa kwa mwaka mmoja, alinukuliwa akisema wakili wao Farshid Rofugaran.

Mmoja wa watu waliokamatwa kwa kucheza densi
Kanda hiyo kwa jina, "Happy we are from Tehran" ilifikishwa kwa maafisa wakuu nchini Iran mwezi Mei baada ya kutazamwa na watu 150,000 kwenye You Tube.

Waliohusika pia walikamatwa na kushitakiwa kwa kosa la kukiuka sheria za kiisilamu ambazo zinawazuia wanaume kucheza densi na wanawake na pia wanawake kutoka nje bila hijab.
Baadaye washukiwa walionekana kwenye televisheni wakijitetea kwamba wao ni waigizaji walihadaiwa kushiriki katika kanda hiyo Kukamatwa kwa vijana hao kulizia ghadhabu kutoka anga za kimataifa huku watetezi wa haki za binadamu

wakianzisha kampeni kwenye mitandao ya kijamii kutaka waachiliwe.

Mwanamuziki Paharrel Williams mwenyewe, ambaye wimbo wake huo, uliteuliwa kwa tuzo la Oscar,pia alieleza kukerwa na kukamatwa kwa watu hao.

Chanzo:BBC

"inachukiza kwamba vijana waliokuwa tu wakijaribu kujifurahisha wanakamatwa,'' aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Watu sita nchini Iran waliokamatwa baada ya kuonekana kwenye kanda ya video iliyokuwa inaiga wimbo wa 'Happy' wake mwanamuziki mashuhuri Pharrell William, wamehukumiwa kifongo cha hadi mwaka mmoja jela kila mmoja pamoja na adhabu ya kuchapwa mijeledi 91.Wakili wa sita hao amesema kuwa hukumu hiyo itaahirishwa kwa miezi sita ikmaanisha kuwa watafungwa tu jela ikiwa watarejelea kosa hilo.

Kanda hiyo inaonyesha wanaume watatu na wanawake watatu ambao hawajafunika vichwa vyao wakicheza densi kwenye barabara na katika paa za nyumba mjiniTehran.

Kanda hiyo iliyowekwa kwenye mtandao wa kijamii wa You Tube, imetazamwa na zaidi ya watu milioni moja.
Wengi wa waliohusika kuitengeza kanda hiyo, walifungwa kwa miezi sita , huku mmoja wao akifungwa kwa mwaka mmoja, alinukuliwa akisema wakili wao Farshid Rofugaran.

Kanda hiyo kwa jina, "Happy we are from Tehran" ilifikishwa kwa maafisa wakuu nchini Iran mwezi Mei baada ya kutazamwa na watu 150,000 kwenye You Tube.
Waliohusika pia walikamatwa na kushitakiwa kwa kosa la kukiuka sheria za kiisilamu ambazo zinawazuia wanaume kucheza densi na wanawake na pia wanawake kutoka nje bila hijab.
Baadaye washukiwa walionekana kwenye televisheni wakijitetea kwamba wao ni waigizaji walihadaiwa kushiriki katika kanda hiyo
Kukamatwa kwa vijana hao kulizia ghadhabu kutoka anga za kimataifa huku watetezi wa haki za binadamu wakianzisha kampeinii kwenye mitandao ya kijamii kutaka waachiliwe.
Mwanamuziki Paharrel Williams mwenyewe, ambaye wimbo wake huo, uliteuliwa kwa tuzo la Oscar, pia alieleza kukerwa na kukamatwa kwa watu hao.
"inachukiza kwamba vijana waliokuwa tu wakijaribu kujifurahisha wanakamatwa,'' aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Video yenyewe ni hii hapa chini...

Last edited by a moderator:
Sheria zingine mh. Ningekuwa mi ni mwananchi wa Iran au nchi yoyote Ile ya kiislamu ningeshasepa kitambo sana. Watu Hamna uhuru na nchi yenu wenyewe, hivi wananchi wanajisikiaje wakiangalia uhuru ambayo wananchi wa nchi zingine wanao alafu wao wanakabwa na sheria Kali namna hiyo?

kwa akili na ufahamu wako unadhani wewe hapa tz uko huru!?
 
Status
Not open for further replies.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom