wimbo bora wa injili kwa mwaka 2009 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

wimbo bora wa injili kwa mwaka 2009

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Rubi, Dec 28, 2009.

 1. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #1
  Dec 28, 2009
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Wimbo Nibebe wa Rose Muhando umechaguliwa na watanzania kuwa Wimbo bora wa Injili kwa mwaka 2009. Wimbo huu umeshika namba 1 baada ya kuzipiku nyimbo 30 zilizotolewa na TBC1 kama zawadi ya x-mass. kwa kushindanishwa kwa siku tatu kuanzia tarehe 25 - 27 Desemba, 2009.

  Wimbo wa Nibebe umepigiwa kura zaidi ya 7000 na kushika nafasi ya kwanza ukifuatiwa na wimbo wa Bwana Yesu ni tegemeo langu na Wimbo wa tatu ni Waraka wa Bahati Bukuku uliopata kura 6000. Washindi wamejipatia vikombe pamoja na pesa taslimu Tshs 50,000 kwa mshindi wa tatu; Tshs 100,000 kwa mshindi wa pili na Tshs 200,000 kwa mshindi wa kwanza.

  Hongera TBC1 kwa kipindi kizuri na hongereni waimbaji wote maana nyimbo zenu hakika ni nzuri na mchuano ulikuwa ni mkali sana kiasi kwamba ilikuwa vigumu kutabiri mshindi.
   
 2. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #2
  Dec 28, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  binafsi ningeupa wimbo wa WARAKA nafasi ya kwanza!......

  BAHATI BUKUKU IS MY GUY BWANA!....
   
 3. Lily Flower

  Lily Flower JF-Expert Member

  #3
  Dec 28, 2009
  Joined: Oct 16, 2009
  Messages: 2,555
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Naomba nikusahihishe kidogo nafasi ya pili ilishikwa na Solomon Mukubwa na wimbo wake wa MFALME WA AMANI.

  Nawapa hongera waimbaji wote walioshiriki.
   
 4. GP

  GP JF-Expert Member

  #4
  Dec 28, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  yah yah!
  Bukuku anaimba nyimbo kweli unazisikilizia moyoni live, nyimbo zinagusa, nyimbo zinaleta hisia.
  rose muhando nyimbo zake ziko kibiashara zaidi, kidunia zaidi.
   
 5. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #5
  Dec 28, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  nyimbo za rose mcharuko
   
 6. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #6
  Dec 28, 2009
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  Lakini mimi pia zaidi ya waraka kuupenda sana pia wimbo wa Neema Mwaipopo usijinyime raha na ule wa AIC wa mpinga Kristo nilizipenda sana bahati mbaya kura hazikutosha.
   
 7. C

  Chaka Member

  #7
  Dec 28, 2009
  Joined: Nov 13, 2008
  Messages: 36
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 15
  Tuko pamoja.
   
 8. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #8
  Dec 28, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Hapa tunaenda sawa homu boi.....Waraka iko safi sana mazee!
   
 9. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #9
  Dec 28, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  hahahaha!
  YUVEEEE!?:D
   
 10. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #10
  Dec 28, 2009
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 520
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Huo wimbo Nibebe unaimbwa sana kwenya harusi, na watu wanakata viuno utafikiri sio wa dini!! Hata The comed naona wameshaumeza!!
   
 11. ZionTZ

  ZionTZ JF-Expert Member

  #11
  Dec 28, 2009
  Joined: Oct 6, 2009
  Messages: 1,276
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  Mi naukubali ule wimbo wa marehemu chibalonza...Toka chini kwenda juu...

  [ame]http://www.youtube.com/watch?v=meixmZOZi0o[/ame] tumempoteza mmoja wa waimbaji

  wazuri ambao hawajawahi tokea.....lakini si mbaya sana kwa sababu yule alieshika

  namba mbili(SOLOMON MUKUBWA) ndie alienusurika kwenye ile ajali iliyomuua angela(ndipo alipopoteza ule mkono mmoja)

  hakuna lisilowezekana kwa mungu.....RIP angel chibalonza
   
 12. GP

  GP JF-Expert Member

  #12
  Dec 28, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  halafu ZD,
  NAOMBA MUONGOZO KUHUSU URAIA WA ANGELA CHIBALONZA NA MUMEWE:
  A. NI WAKONGO??
  B. NI WAKENYA??
   
 13. Teamo

  Teamo JF-Expert Member

  #13
  Dec 28, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 12,286
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  ni wakenya!
  samahani.mimi zio zd:D
   
 14. ZionTZ

  ZionTZ JF-Expert Member

  #14
  Dec 28, 2009
  Joined: Oct 6, 2009
  Messages: 1,276
  Likes Received: 241
  Trophy Points: 160
  naomba nikurekebishe, mimi sio ZD. any way angela na mumewe ni wakongo kama alivyo solomoni ila kikazi wapo kenya, yani kama walivyowasanii wa kongo tz. kwenye album yao ya kwanza walizungumzia hili.
   
 15. GP

  GP JF-Expert Member

  #15
  Dec 28, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Oooh, sorry i meant ZIONTZ
  NASHUKURU KWA MUONGOZO!.
   
 16. Triplets

  Triplets JF-Expert Member

  #16
  Dec 28, 2009
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 1,103
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  mimi bado hakuna wimbo ulio upiku ule wa 'amenitendea'
  napenda na hizo nyingine lakini amenitendea ndio funga kazi katika injili
   
 17. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #17
  Dec 28, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Ningekuwa mimi ndo nachagua, ningewapa AIC Chang`ombe.

  Napenda mno jinsi yule dada mwimbishaji anavyokuwa free wakati anaimbisha, utadhani yuko chumbani kwake!...Hakuna kupandisha mishipa ya shingo kama huyu nani huyu..!
   
 18. C

  Chupaku JF-Expert Member

  #18
  Dec 28, 2009
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 1,045
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Jamani mbona zawadi zenyewe kiduuunchuuu!!! Laki mbili mwimbaji bora wa mwaka, heh! Wangewaambia Cocacola, etc etc wawasaidie, wangepata zawadi zaidi mbona?
  Wimbo wa Nibebe kelele tu, na sijui watu wanaupendea nini?
   
 19. C

  Chupaku JF-Expert Member

  #19
  Dec 28, 2009
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 1,045
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160

  Au wewe ni Msukuma???
   
 20. GP

  GP JF-Expert Member

  #20
  Dec 28, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  kwani AIC ni ya kikabila????
   
Loading...