Wimbi: Nguvu ya umma Africa, ugumu wa maisha na Tanzania yetu...taa ya kijani hiyo! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wimbi: Nguvu ya umma Africa, ugumu wa maisha na Tanzania yetu...taa ya kijani hiyo!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Phillemon Mikael, Jan 28, 2011.

 1. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #1
  Jan 28, 2011
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,853
  Likes Received: 2,426
  Trophy Points: 280
  Nani anaamini kuwa utawala wenye nguvu na kama wa IVORY COAST ...ya Gagbo ...ni historia... utawala wa TUNISIA wa Ben Ali na chama chake Tawala kilichokaa madarakani umeondoka ...sasa ndani ya siku nne ...mtawala mwenye nguvu AFRICA ...rais Hosni Mubarak ...sasa utawala wake unapumulia mashine.....na moto wa petroli unaendelea....yote haya yanatokea ndani ya mwezi mmoja tu...januari.

  Hii sasa ni taa ya kijani kwa chama cha MAPINDUZI ...kinatakiwa kibadili mwelekeo haraka kiheshimu wananchi, kisiwaone kuwa ni wajinga na mazuzu,...maamuzi kinayochukua..ni wazi Tanzania haina intelligence wala jeshi lenye nguvu kuliko EGYPT...Au Tunisia....ambako wanajeshi na wanausalama wameamua kujiunga na waandamanaji...

  Serikali yetu haiwezi kuwa salama ...kwenye nchi ambayo leo hii kila mahali ni migomo ....hadi polisi wanakatwa mishahara...HAZINA HAKUNA PESA...umeme hakuna kwa hiyo hata KODI INASHUKA SANA!!!

  Hofu nyingine na dalili mbaya ninayoiona Tanzania ni kuwa zamani tulizoea kuona maandamano yanakuwa na kitovu DAR ES SALAAM ...leo hii mikoani ndiko kumekuwa kitovu cha mabadiliko ....ARUSHA, DODOMA, SONGEA, MBEYA.etc...hii ni dalili kuwa hata wananchi tunaowachukulia wapole wa mikoani wameshindwa na uvumilivu....

  Naomba serikali ichukulie tahadhari hasa ugumu wa maisha unaoendelea ...nachelea kusema kuwa wakiendeelea hivi watapinduliwa.........

  FIKIRIA EGYPT rais alishafikia hadi kutaka kumuachia urais mwanae GAMAL MUBARAK ...lakini nadhani kufikia wiki ijayo Hosni atakuwa tayari amepinduliwa na familia yake yote kukamatwa..tunapooongea leo hii Tunisia wamekamata FAMILIA NZIMA YA BEN ALI....just imagine ...nimeone footage wanaingizwa kwenye karandinga ...nikasema huu ni mshahara wa dhambi!!!
   
 2. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #2
  Jan 28, 2011
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,314
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  PM,

  Unayosema yana ukweli mtupu! Its only a fool who would refuse to recognize the quick changes we see in the mind of Tanzanians today.We are in the mid of dormant volcano which awaits forces of nature to take place before it erupts.

  Kazi ya viongozi sio kuzitengeneza Dowans....wao wanaona sifa na kitu rahisi kucheza na feelings za watu maskini kwa kujilimbikizia mali wenyewe.
   
 3. Kimox Kimokole

  Kimox Kimokole Verified User

  #3
  Jan 28, 2011
  Joined: Jun 9, 2010
  Messages: 968
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Niko hapa kama mtego vile nasubiri kufyatuliwa tu!
   
 4. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #4
  Jan 28, 2011
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,853
  Likes Received: 2,426
  Trophy Points: 280
  ..kaana matajiri kama rostam na subash wanaoiunga mkono ccm..wanataka usalama wa mali zao ..ni bora wamwambie huyo kijakazi wao aendeshe nchi vizuri...maisha yanakuwa magumu kila siku hadi chumvi inapanda bei?
   
 5. kkakuona

  kkakuona Member

  #5
  Jan 28, 2011
  Joined: Jan 12, 2010
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Acha wafurahie kutanua kwa mashangingi kupitia migongo ya raia masikini wa TZ kwa njia za ufisadi. "Yana mwisho hayo", na nadhani mwisho uko karibu.
   
 6. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #6
  Jan 28, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Not a big public threat; just a quiet word. That could make all the difference. And if Egypt goes, the dominoes will really start to fall. Plus, if this relatively secular protest is suppressed, the odds of a radical Islamist revolt instead will go way up.
   
 7. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #7
  Jan 29, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,779
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  mwisho umeisha fika. ni issue ya muda muda tu!
   
 8. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #8
  Jan 29, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Tatizo tunaongea sana mitandaoni badala ya kuchukua hatua zinazohitajika.
   
 9. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #9
  Jan 29, 2011
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Unemployment and Food Crisis are the problems need to be solved ASAP. Mtu hana menu then hana hata uhakika wa kesho???? get ready has kwa mvua hizi? Kilimo Kwanza itakuwa kibwagizo.
   
 10. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #10
  Jan 29, 2011
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,853
  Likes Received: 2,426
  Trophy Points: 280
  Unajuwa hata kabla ya uchaguzi ndani ya CCM walikuwa wanaliwazana wanasema CHADEMA ni chama cha mtandaoni..na ukanda wa kaskazini..na CUF walishawavika udini
  Lakini matokeo ya uchaguzi yametoka yakaonesha picha tofauti kwa CHADEMA kupata kura kwa uwiano wa kuridhisha nchi nzima....
  Siku za karibuni wananchi wa pembezoni mwa nchi wameibua ujasiri wa ajabu.......so hatuwezi kusema yanayotokea Tunisia Na Misri hayatatokea hapa....serikali must pull up its sox ..really!! mimi naogopa kwa kweli............kama huamini soma mioyo ya watu mitaani imejaa masononeko...ya ugumu wa maisha....hii inaweza kuzaa mlipuko wa vurugu muda wowote............hasa unapogusa chakula...ada ..na bado watoto wanaosomeshwa kwa kufunga mikanda wanafeli.....soma ukutani!!!
   
 11. K

  Kide Member

  #11
  Jan 29, 2011
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 74
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  sooner or later wananchi wataafanya maamuzi mazito na yasiyotarajiwa!wengi tunasubira japo wiki 2 za kwanza za bunge tujue mbivu na mbichi!kwani hajachoka na uchumi kudorola,bei za vyakula na kila kitu kupanda karibu every week?
   
 12. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #12
  Jan 29, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,287
  Likes Received: 810
  Trophy Points: 280
  Du bado nasema Chama tawala na Serikali yetu mumlipe Dowans tu, ya Misri yatawakuta si Chama Pinzani, UVCCM wala hao maaskari waliokatwa mishahara watakubali kadhia hiyo tena ni barabarani tu WOTE (hivi ni nani asiyelipa deni la bill zake Tanesco? leo hata wasiotumia wanakamuliwa patachimbika :roll: :roll: :roll:
  Dalili za mvua.... kote ni ufisadi unaoleta umaskini na matabaka ya ki-maisha
  MUNGU ibarikia Tanzania MUNGU ibariki Afrika
   
 13. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #13
  Jan 29, 2011
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Akisogea karibu jipendekeze kisha achia kitu, utatambulika duniani kote!
   
 14. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #14
  Jan 29, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,845
  Likes Received: 11,964
  Trophy Points: 280
  Katavi you are behind the clock, usidharau mitandao, mitandao hii ndiyo iliyochochea na kuhamasisha wananchi wa Egypt na bado leo inatumika ku mobilize hiyo protest hadi serikali imefikia hatua ya kufunga internet kwa kujua nguvu yake.

  na kwa taarifa yako kuwa mitandao iko kwenye chart na ina nguvu zake jana Obama amelizungumzia hili wakati anatoa msimamo wake kuwa serikali ya Egypt iache watu wawasiliane.
   
 15. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #15
  Jan 29, 2011
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Nakuunga mkono mkuu, tumezidi longo longo bila kuchukua hatua kama Tunisia.
   
 16. Innobwoy

  Innobwoy JF-Expert Member

  #16
  Jan 29, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 980
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 60
  Now mwanza kuna vurugu,machinga vs mgambo wa jiji,bt machinga tumekuwa wengi kuliko askali wa jiji,its just a begining let us see whats gonna in the coming few days, My take;Misiri waliorganize maandamano via facebook na watu 90000 waliconfirm kuandamana,naamini Tanzania nguvu ya jf itaunganisha nguvu ya wataTanzania kwenye maandamano yanayokuja,..i lv Tanzania i hate Mkwere regime,.
   
 17. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #17
  Jan 29, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,845
  Likes Received: 11,964
  Trophy Points: 280
  Sure PM watu walikuwa wanabeza projection ya JF kwa CDM kuwa kinakuwa kwa kusema hayo ni ya mitandaoni lakini hali halisi ilivyo sasa ni kuwa CDM iko masikioni mwa watanzania wengi na CCM inalijua hilo ni mwenye roho ngumu tu ndani ya CCM atapinga na mashabiki wachache waliobaki nje ya CCM.
   
 18. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #18
  Jan 29, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,229
  Likes Received: 4,949
  Trophy Points: 280
  Yatosha sasa CCM kutambua kua siku ya hukumu yao itawadia..wanaharakati wamepiga kelele sana lakini hawakusikia,wameoneshwa wazi wazi matendo yao yanayowachukiza Wananchi ila hawakuona...laiti wangalijua kusoma wakati wangejua kalenda ya siku zao ilivyomalizika! Kama wakitumia enzi za "zidumu fikra sahihi za mwalimu" watagundua kua sasa ni sawa na sawa na upatu uvumao ama mpira usio na upepo!
   
 19. Innobwoy

  Innobwoy JF-Expert Member

  #19
  Jan 29, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 980
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 60
  Km makamu mwenyekiti wa ccm jana ndo alikuwa vile kwe nye mdaharo basi nimegundua kwanini makamba ni katibu wa sisiem,,wameisha,
   
 20. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #20
  Jan 29, 2011
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  CCM ina viongozi wengi tu wenye elimu ya kutosha na akili timamu ya kujua Uoza wa Chama chao mmoja wa viongozi hao ni ni PIUS Msekwa.
  kujikanyaga kwa Pius Msekwa kunatokana ukweli kwamba amekalia JITI la CCM linamfanya vibaya mzee wa watu kiasi cha kuonekana chizi kwenye TV.
  Tatizo la viongozi wa CCM ni kutetea UFISADI kwa nguvu yao yote, damu yao na nyama ya misuli yao yote bila kujali ukweli wa mambo namwelekeo wa kisiasa.
  Hakuna kiongozi wa CCM anayetumia akili zake kuchambua mambo, kila kiongozi anachukua sehemu ya ujinga wa HIZA TAMBWE na kuukuza.
  Maana yake viongozi wa CCM wanawekewa maneno midomoni mwao ili waseme kutetea uoza na uvundo. Hawana hiari katika kusema na kunena uongo.
  Ukiwekewa maneno mdomoni hata uwe na kichwa au jasiri na shupavu wa kuongea kiasi gani utapwaya kama suruali yakuvalia matakoni.
  Pius Msekwa anachemka kwa sababu anaongea maneno yakuwekewa mdomoni, akiongea mind yake wote tutashanga umahiri wake.

  Kakalia vibaya JITI la CCM sasa analazimika kuvumilia maumivu yake.
   
Loading...