Wimbi la wizi arusha laanza tena

Jethro

JF-Expert Member
Mar 23, 2009
2,219
370
Wana JF,

TUKIO HILI LILITOKEA 27/02/2010

Last week nilikuwa napita arusha nikakutana na wimbi la wizi ambalo wao ni kuvamia maeneo ya Glossary, Bar, Maduka, na majumbani Na wakija ni wako kundi la kuanzia sita na wawili huwa na siraha na wengine wao ni ku search watu na kuchukuwa walivyo navyo, Hili tukio lili tokea ambako mdogo wangu ali alikwa na rafika ya mke wake pale shamsi pala pale kwa kituo cha Dala dala ukiwa waelekea arusha air port kuna glossary inaitwa PARK SIDE , mdogo wangu na mkewe walifika saa 4 kasoro usiku na wakawakuta rafikizao wameketi na walikuwa ni wanne na wao wakaongezeka wakawa sita dani ya dakika 5 walipo keti na kuletewa vinywaji wezi(Majambazi) wakatinga ndani wakiwa na bastora majambazi wawili walikuwa na siraha nakuanza kukusanaya simu,pochi,pesa za wale waliokuwepo na counter, waka mtaka mwenye mali ambaye ndie rafiki wa mke wa mdogo wangu wakamwambia akafungue gari na wakabeba pesa zizlizoko kwa gari za mchango wa harusi,laptop na external hard drives na walipo maliza wakasema sasa tulitumwa kukuua dada wa watu alipiga magoti na kuomba msamaaa wakamwacha waka sepa zao.

Kumbe tukio kama hilo lilitokea jana yake kwenye bar njia ya kwenda mbauda.

Kwakweli nilistahajabika sana ila nirishukuru kuwa wote walikuwa hai,

swali laja je wale police wetu wanao tumia pikipiki a.k.a (Voda faster) siku hizi wako wapi patroooo zao wanazipiga saaa ngapi na wanapita mara ngapi kwa hiyo mitaaaa, Nilimuuliza mdogo wangu je wakati wanaenda huko(Park-Side Glossary) ulipisha hata na one ten zao au Voda faster zao akajibu hapana kwanza siku hizi ni mara chache sana kukutana nao mwanzoni nasikia kila muda tu unawaona ukihama mtaaa utawakuta siku hizi wamepunguza kabisa kufanya patrooooo zao. Na utakuta one ten imepaki karibu na petrol station sasa sijui wanalinda mauzo ya mwenye petrol station au?

Kwakweli nimeanza kuamini wimbi la wizi arusha sasa limeanza kushamiri na pia watu siku hizi wanaogopa mtu anaye endesha piki piki hao ndio wauwaji wa kuvizia watu ma getini.au ukimwona mtu wa pikipiki anakuja huku waendesha gari waanza kupandisha vioo.

Hii hali itaisha lini?? Je nitatizo letu sisi watanzania? au ni Ajira hakuna au ni visasi vya wafanya biashara?Wivu wa kimaendeleo hupendi mwenzio aendeshe biashara yake eneo fulani sasa wamtumia majambazi wamharibie biashara ili ahame ilo eneo?

Au tatizo nililo gundua arusha ni mtu akifungua biashara furani basi ukizunguka kidogo tu utaona watu si chini ya kumi nao wamefungua biashara kama yako na itashamiri kwa wengine kufungua.watu wawe creative kwa biashara jamani na sio kuiga

Police wetu wanataka Task force ya namnagani waandaliwe ili wahimili hili wimbi la ujambazi? waongezewe mishahara au vifaa vya utendaji kazi means magari ya patroo yawe mengi na Voda faster ziwe nyingi pia na vifaa vya kujirinda?

Siraha zakodisha kama njugu! kwanini nasema hivyo iweje tukio mojo la aina hiyo latokea labda kwa siku mara mbili au na kesho yake siraha zatokea wapi?

Au urudishwe mfumo wa enzi ya mwalimu kila mara usalama wataifa wanatinga kwako na kutaka kujua siraha umeitumia vipi au kila baada ya miezi kadhaa ikakaguriwe?
 
Back
Top Bottom