hippocratessocrates
JF-Expert Member
- Jul 1, 2012
- 3,598
- 1,539
Salaam.
Hivi karibuni tumeshuhudia wimbi kubwa la wanachama mbalimbali wakiwemo na na viongozi wa ngazi ya Udiwani hadi Taifa kukimbia vyama vyao kuelekea vingine. Hasa hili liitwalo "mafuriko" la wanachama wengi wa CCM kuhamia CHADEMA/UKAWA.
Ninajiuliza ni nini hasa kilichopelekea 'mbio' hizi?
1. Uoga:
Hofu ya kuona ukihama hali haitakuwa shwari ya usalama binafsi na kwamba kiongozi mmoja akianzisha na akawa 'salama', basi wengine wanaweza kufuata? Kama ndivyo ni aina gani ya viongozi(wasio shupavu tulikuwa/tulio nao), pili ni aina gani ya udikteta wa viongozi ndani ya vyama kuwapa "hofu" wanachama? Tutegemee nini pale Baraza la mawaziri likivunjwa?
2. Sifa:
Nchi hii tumetawaliwa na mihemko, hata kama jambo hatujalitafakari lakini kwa sababu ya ushabiki, wengi wetu tumekuwa katika mkumbo. Kama ndivyo, inatusaidia nini hasa kwa hawa wanaohama?
3. Maslahi:
'Muda wa kufanya/kupiga mahesabu ndiyo huu'
Tumeshuhudia wengi wa walio "katwa" ndiyo walio na wanaoendelea kuhama! Je, ni kweli wangeonyesha nia hiyo hiyo ya kutaka mabadiliko hata ndani ya vyama vyao kama 'wasingekatwa'? Kinachowaleta ni demokrasia au Maslahi? Kama ni demokrasia kwanini wasikubali kushindwa ndani ya vyama vyao?
Ni nini hasa lengo lao na zaidi kama CHADEMA/UKAWA tumejiandaaje/ni mkakati gani 'tulionao' kuhakikisha wanaokuja ni 'safi' na si mamluki au "Makapi"?