Wimbi la mababu na mabibi linaongezeka kwa kasi ya 4G hapa Tanzania

Ntandaba

JF-Expert Member
Jul 30, 2015
922
1,472
Si ajabu leo hii hapa Tz kukuta mwenye umri wa miaka 25 tayari anawajukuu wawili, zamani mambo hayo yalikuwa ni nadra sana kuyakuta katika jamii zetu.

Ongezeko hili sijui linachangiwa na nini. Leo hii unamkuta mzazi na mtoto wake wapo kwenye mashindano ya kuzaa, binti wa darasa la sita naye unamkuta ana mtoto. Kwa kweli watanzania bado tupo kwenye safari ndefu sana kufikia uchumi wa kati.

Maumbile na vyakula tunavyokula huenda yanachangia mambo hayo. Wanafunzi wengi miaka hii wanaohitimu elimu ya msingi au sekondari (olevel) katika shule zetu asilimia kubwa wanakuwa na miili midogo lakini cha ajabu wanawahi sana kubalehe na hivyo kupelekea sana kuanza kuvunja amri ya sita.

Je kama taifa na wazaz ili kulinda busara za wazee na heshima zao tufanyeje kunusuru janga hili? Kwa maana imekuwa kama fashion kuona mwenye miaka 21 akijisifu mi nina wajukuu wawili au zaidi hatimaye kuishia kulalamika tu mbona TASAF wanachelewesha pesa.
 
Si ajabu leo hii hapa tz kukuta mwenye umri wa miaka 25 tayar anawajukuu wawili,zamani mambo hayo yalikuwa ni nadra sana kuyakuta katika jamii zetu.
Ongezeko hili sijui linachangiwa na nini,leo hii unamkuta mzazi na mtoto wake wapo kwenye mashindano ya kuzaa,bint wa darasa la sita naye unamkuta anamtoto kwa kweli watanzania bado tupo kwenye safar ndefu sana kufikia uchumi wa kati
Maumbile na vyakula tunavyokula huenda yanachangia mambo hayo,wanafunzi wengi miaka hii wanaohitimu elimu ya msingi au sekondar (olevel) katika shule zetu asilimia kubwa wanakuwa na miili midogo lakini cha ajabu wanawahi sana kubalehi na hivyo kupelekea sana kuanza kuvunja amri ya sita
Je kama taifa na wazaz ili kulinda busara za wazee na heshima zao tufanyeje kunusuru janga hili?kwa maana imekuwa kama fashion kuona mweny miaka 21 akijisifu mi ninawajukuu wa wili au zaidi hatimaye kuishia kulalamika tu mbona TASAF wanachelewesha
Hakuna cha chakula wala nini,uchumi wa nchi ni mbovu na unaliwa na wachache ambao wanajineemesha na keki ya taifa,waliobaki ni mafukara na wanataka waishi katika standard ya walionacho,sasa unategemea mabinti wapate wapi pesa ili kuishi katika dot com,kwa hiyo kuwalaumu ni kuwaonea coz kama wewe au mtu mungine yeyote anamiliki vitu vizuri luxurious unadhani wasio nacho hawatamani?,kumbuka wanaume wana take advantage hiyo ya ufukara wa mabinti na kuwarubuni kwa vitu vya anasa na kupelekea kuwatumia na hatimae kuwapa mimba katika umri mdogo,na hiyo inaendelea kuwa vicious cycle ambayo binti mdogo anazalishwa anazaa mapema sana na mtoto aliozaliwa anakuwa akifukuzana na mama yake kiumri mpaka wanakuwa kama mtu na mdogo wake,halafu na yeye anaingia katika mahusiano mapema kwa vishawishi kama vile vilivyompitia mama yake na kuzalishwa katika umri mdogo,hapo sasa binti mdogo anakuwa bibi coz binti yake kazalishwa.
 
upuuzi tuu na akili fupi unakuta ka mwanamke ka miaka 20 kama mtoto wengine 18 hadibb17 sasa unajiuliza huyo mtoto atakae mzaa atamwita dada au mama? shame.
 
Back
Top Bottom