Wimbi kubwa la vijana wasomi 20's kujitoa uhai, nini maoni yako?

sky soldier

JF-Expert Member
Mar 30, 2020
5,408
19,026
NI wiki iliyopita kuna kijana alijinyonga ma jana naskia mwingine tayari, Mwaka jana kuna aliyejitupa ghorofa ya supermarket. Hao wote walikuwa wasomi wenye miaka ya ishirini na kitu wakidai wana stress.

Hili wimbi pengine linaweza kuwa kubwa sana tusipojiangalia.

Mchango wako ni wa muhimu
 
Vijana wengi ambao ni graduates hawana imani na uvumilivu.

Vilevile watu (ndugu, jamaa na rafiki wa karibu) waliopaswa kuwapa psychological support ndio wanawakejeli na kuwatukana.

Mimi nilikejeliwa na kuchekwa sana kwa kumaliza chuo mwaka 2009 na kuchelewa kupata ajira kwa miaka 2 ila nilikuwa mvumilivu na mwenye imani chanya kuwa ipo siku zamu yangu itafika na Mungu atanifungulia milango ya baraka.
 
Ngoja nieleze situation yangu.
Nilimaliza chuo 2015. Kwa upande wangu tangu nipo mwaka wa pili chuo nilijisemea kwamba sitaajiriwa na wala sitakaa nitume maombi ya kwenda kwenye interview, nitapambana mwenyewe kwenye biashara mpaka nitoke.
Nilipomaliza chuo nikaondoka home kwenda mjini kuanza biashara, nilisave Tsh laki 5 za bum, mambo yakawa magumu mpaka nalala njaa, lakini nilikomaa.
Nilikuwa nasoma sana vitabu, kila mwezi vitabu viwili au vitatu vilinipa hope sikukata tamaa.
Nilikuwa na maono makali sana kiasi hakuna mtu wa kunipindisha. Biashara nilikuwa napata faida elfu 50 mpaka 70 kwa mwezi, maisha yanilipiga kofi kweli nilichakaa mwili na roho kidogo nikate tamaa.

Wazee hawakunielewa walinambia nimepotea , nimepatwa na pepo gani mchafu?? Kila wakinipigia simu waniuliza mwanangu lini unatuma maombi ya kazi, tunataka uajiriwe.
Ndugu zangu kila siku wakinipigia simu wanauliza umeajiriwa? Mpaka kuna wakati wazee wakinipigia simu sipokei, wanasema si urudi tu nyumbani maana hatuoni unalolifanya huko mjini.
Kuna wakati nililia machozi nikasema Mungu wasamamehe maana hawaoni ninachokiona.
Nilikomaa mpaka mwaka 2018 nikaanza kupata faida nzuri walau laki 5 kwa mwezi, nikakomaa zaidi now napata walau mil 2 mpaka 2. 5 kwa mwezi net profit kwenye biashara na bado napambana zaidi, nyumbani kidogo heshima ipo yale maswali ya utaajiriwa lini yameisha maana sikosi kutuma pesa za mboga.
Sasa vijana wengi wanakata tamaa mapema, ulijumlisha na kejeli na masimango kutoka kwa ndugu ndo inapelekea depression mpaka mtu anajitoa uhai.
Vijana tupambane tuwe na BIG PICTURE THINKING, tusiwaze leo bali miaka 10 ijaytutafanikiwa tu
Naambatanisha na kitabu hichi kilinisaidia sana kuwa positive mda wote wa hustle.

JPEG_20201004_173701_7878693369716352327.jpg
 
View attachment 1590206
Apreciation
 
Vijana wengi ambao ni graduates hawana imani na uvumilivu.

Vilevile watu (ndugu, jamaa na rafiki wa karibu) waliopaswa kuwapa psychological support ndio wanawakejeli na kuwatukana.

Mimi nilikejeliwa na kuchekwa sana kwa kumaliza chuo na kuchelewa kupata ajira mwaka 2009 ila nilikuwa mvumilivu na mwenye imani chanya kuwa ipo siku zamu yangu itafika na Mungu atanifungulia milango ya baraka.
Umemaliza chuo 2009?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom