William Ngeleja - Waziri Anayetuhumiwa kwa Wizi!

Uzalendo tz hakuna,kila m2 ni mwizi ila inapobainika tu ndio matatizo huanza.Jiulize,kwa nini maeneo mengine tz hii yameendelea, lami hadi vijijini na mengine hakuna?je walichangishana hela wakajenga au ni wizi? Mimi nikiwa waziri haki ya MUNGU lazima niibe.tena waziwazi kabisa! Hawa wote wanaopiga makelele si wanatafuta mpunga tu,hakuna lolote.
 
Taarifa hizi zilipotolewa mwanzo kabisa, nilijitahidi kuzifanyia kazi kwa kumfuata huyu MR MEGA...WHAT ili nisikie kauli yake, huwezi amini alinitolea njea na kudai kuwa ni uzushi, nilipotoka tu nje ya ofisi yake pale Wizarani aliwasiliana na bosi wangu kujitetea na kufanya alilolifanya ili habari hii isitoke na ndivyo ilivyokuwa.
Media za TZ MHHHHH!
:shut-mouth::shut-mouth:
 
Tupe jina moja tu la waziri aliyejenga nyumba ya maorofa kama hayo enzi za Mwalimu

Tena huyu ana vimiradi vingi sana kwenye migodi ambavyo kaandikisha vijikampuni vyake kwa majina tofauti na ingekuwa TAKUKURU inafanya kazi basi wangesha mtoa hadharani
Maisha ya wakati wa Mwalimu na sasa ni tofauti kabisa. Wakati ule nyumba za serikali zilikuwa ni za kutosha na ndiyo zilizokuwa zinaonekana ni za kisasa zaidi, kwa hiyo haikuwa inashawishi mtu yeyote kujenga. Tena ukumbuke kuwa hakuna mfanyakazi wa serikali aliyekuwa anajenga wakati ule. Ninawafahamu ndugu zangu wengi sana waliokuwa na vyeo vikubwa sana tu serikalini lakini walikufa bila hata kibanda. Lakini si maisha ya sasa, ambapo hata walimu wa shule ya msingi wanajenga. Sasa jiulize kama mwalimu wa shule ya msingi na mshahara wa laki moja na nusu kwa mwezi anaweza kujenga nyumba yake, iweje kwa waziri kushindwa kujenga pamoja na marupurupu yake.

Kuhusu uwazi, ni dhahiri kwamba hawezi kufanya hivyo kwa kuwa watanzania mna mitizamo hasi na viongozi. Kiongozi akifanya chochote cha kuboresha maisha yake mnachukulia kwamba ameiba. Hapo ndipo penye tatizo bandugu. Lakini si kweli kwamba kwa level ya waziri tena aliyefanya kazi miaka karibu saba atashindwa hela ya kujengea gorofa la floor tano. Mimi mwenyewe msukuma mkokoteni, nafikiria kujenga angalau nyumba ya gorofa moja.
Kama tuna ushahidi kwamba ameiba, basi tulete ushahidi wa wizi wake na si hizi porojo za anajenga ametoa wapi hela! Kama ndiyo hivyo wafanyakazi wote wa serikali hawatakaa wajenge. maana wakijenga tu mtawauliza walikotoa hela.
 
Mimi siku zote napenda kuingia hivi!! Kama ifuatavyo
HII TZ MIMI NA IFANANISHA NA FRASH,MEMORYCARD NA EXTERNAL ZINGNE AMBAZO ZIMEJAA MA VIRUS
SASA IMEKUWA KILA SIKU NI KUDELETE TU! HAYA MATROJAN(kujivua gamba) MIMI NIONAVYO BORA KU FORMAT KULIKO KUSCAN NA MA ANT-VIRUS AMBAYO NI NOT UPDATED!!!! Sh***@@##zy kabisa
BORA KUIFORMAT KWA MGOMO NCHI NZIMA
TUANZE KUINGIZA FILES UPYA!
yaani nipo moto acha tu!

sorry! Cannot format. The device is protected...!
 
Uzalendo tz hakuna,kila m2 ni mwizi ila inapobainika tu ndio matatizo huanza.Jiulize,kwa nini maeneo mengine tz hii yameendelea, lami hadi vijijini na mengine hakuna?je walichangishana hela wakajenga au ni wizi? Mimi nikiwa waziri haki ya MUNGU lazima niibe.tena waziwazi kabisa! Hawa wote wanaopiga makelele si wanatafuta mpunga tu,hakuna lolote.
Ukiongelea unequal distribution of resources hapa nchini hilo naliafiki kwa kiasi kikubwa sana. There is no any reason why the northern part of the country should be more developed than the rest of the country. Haitoshi kutuambia kwamba uwepo wa mlima kilimanjaro pekee ndo ulitosha kuifanya Kilimanjaro kuwa that much developed, kushinda kule Mwadui, au geita. Katika hilo kuna shida kubwa sana, na ninafikiri idea ya akina Mbowe ya serikali ya majimbo inaweza kuwa ni jibu. Kila kinachochumwa mahali fulani kitumike kupajenga hapo kilipochumwa. Ni aibu kwa mikoa kama Songea au rukwa kuwa maskini ilihali ndiyo kisima cha uzalishaji nchini. Lakini hizi habari za fulani mwizi kaiba sijui nini, hazileti maana kama hazina ushahidi wa kutosha.
 
KATUNI%2BNGELEJA..jpg
 
hii nchi hii nchi hii ila ngoja tuuuuu...kwani nimeshaona kitu kinachoitwa THE BEGINNING OF THE END..
 
Wewe Gembeson Unatumia makamasi badala ya Ubongo kufikiri.
Kamasi zako zipo wapi hapo!. Umeambiwa Client wa hilo jengo ni Jakandom investment co.Ltd. Ni mfanyabiashara wa samaki hapo mwanza. Basi tumia akili zako zenye makohozi umtafute huyu akupe data kapataje mshiko wote huo wa kujengea gorofa kama samaki hawauziki. Mr.Ngeleja anahusika vipi hapo?. Muite ngeleja mwizi kwa kutumia ushahidi kama ule wa CAG, na sio huu uzushi wenu. atawashinda. Ukweli bado unabaki kuwa hii nchi kila mbuzi anakula kwa urefu wa kamba yake. Ninahisi hata wewe Maarko ukipewa hii wizara ya ngeleja tena utatamani uongeze kamba kutoka Geita gold mine hadi hapo kwenu Lindi. Suluhisho ni kuondoa madarakani hawa waliochoka na kuweka mvinyo mpya wenye uchungu na maisha ya wa tZ.
 
mnaangalia mawaziri2, wananchi wengine hamuwaangalii?
Wananachi wengine wanajifanyia biashara zao. Hakuna anyesema mwananchi ye yote awe wa kawaida au waziri asiwe tajiri (kumbuka tuko katika itikadi ya utajirisho). Mawaziri wanaandamwa kwa sababu ndio serikali ambayo ndio inajukumu la kulinda raslimali za taifa na kusimamia hiyo keki kwa haki ili kila mtu apate haki yake. Sasa tunapoona wao wanajigawia vipande vikubwa kuliko stahiki ni lazima tuwaangalie kwa macho makali maana huo ni UFISADI. UFISADI maana yake ni wizi wa mali za umma unaofanywa na wale waliokabidhiwa madaraka ya kusimamia mali hizo.
 
Tumechoka sasa! Atakayemwona alipo Mr Megawati niambieni. Potelea mbali!

Wanatembea na silaha za kivita!!! Utatolewa kamasi oh oh kwani hukuona mambo ya makamu wake?! Labda tumia ile mbinu ya Moro peleka CD ampe nusu kaputi kwanza!!! Teh tehe!!!
 
Wivu tu!, nyie kinawauma nini Mr.megawati kujenga gorofa?. Mbona mshahara wake na posho anazopewa spika zinatosha kujenga hata gorofa kumi?. sembuse hizo tano!.

Hallo! Wengine hawapati milo miwili kwa siku, we waona ni wivu kuuliza wenzetu kujichukulia mahela kutokana na rasilmali zetu. Tumewapa dhamana wasimamie kwa niaba yetu, halafu wajizolea wenyewe. Sio urefu wa kamba ya mbuzi huo. Ni ufisadi!!
 
Back
Top Bottom