William Ngeleja na Hamis Mgenja wapongezana kwa kutapeliwa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

William Ngeleja na Hamis Mgenja wapongezana kwa kutapeliwa!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by luckman, Feb 7, 2012.

 1. l

  luckman JF-Expert Member

  #1
  Feb 7, 2012
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 174
  Trophy Points: 160
  William Ngeleja na Hamis Mgenja wapongezana kwa kutapeliwa!​

  KWA siku mbili mfululizo kumekuwepo na propaganda na uzushi mkubwa unaonezwa kupitia njia mbalimbali kuwa Waziri William Ngeleja ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Sengerema, amehamisha uongozi wote wa juu wa CHADEMA Wilaya ya Sengerema.
  Kupitia taarifa hii kwa umma, CHADEMA Wilaya ya Sengerema tunapinga uzushi huo, ambao watu wazima na akili zao wameamua kukaa chini na kuupika, wakiwa na madhumuni yao ambayo kwa bahati mbaya sana yanajulikana siku nyingi sana, kwa sababu CHADEMA ni chama imara kuanzia ngazi ya taifa hadi ngazi ya chini kabisa inayoitwa msingi.
  Tunajua kuwa uzushi huo ni sehemu tu ya mpango mkakati ambao CCM inafikiri itaweza kujinusuru, kuwasahaulisha na hatimaye kuirejesha Kanda ya Ziwa katika nchi ya Misri, baada ya watu Kanda ya Ziwa kuonesha kasi ya ajabu kuikimbia nchi hiyo ya mateso kwenda nchi ya ahadi, CHADEMA.

  Tumelazimika kutozipuuza na kuamua kuzungumzia uzushi na propaganda hizi kwa sababu moja mkubwa, moja ya malengo yake makuu ni kutaka kuwavunja nguvu wananchi, Watanzania wema ambao wameamua kwa dhati kabisa kuunga mkono upinzani wa kweli unaongozwa na CHADEMA, kwa ajili ya kufikia mageuzi ya kweli ya uongozi na kupata mfumo mpya wa utawala.
  Ni mwendelezo ule ule wa CCM na serikali yake kuwarubuni na kununua makapi ya uongozi ambayo yamejificha katika mwavuli wa upinzani. Mbinu hii haijaanza jana wala leo, na kwa namna ambavyo siasa za nchi hii sasa zinavyokwenda, huku CCM ikiendelea kuwadanganya……….

  Lakini pia propaganda na uzushi huo ulioanzishwa na Mbunge Ngeleja na viongozi wake wa wilaya na sasa umedakwa juu kwa juu bila hata tafakuri na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgenja, pia hauwezi kuachwa hivi hivi kwani ndani yake umedhihirisha kwa kiwango cha hali ya juu namna CCM na viongozi waandamizi wa serikali yake, wanaweza kudiriki kuudanganya umma wa Watanzania mchana kweupe kwa nia ya kutimiza mchezo mchafu kwa ajili ya manufaa ya watu binafsi na chama chao. Hawaangalii taifa, wala wananchi.

  Uongo na upotoshaji mkubwa katika mpango wa Ngeleja na wenzake Sengerema
  Kwanza imepotoshwa kuwa mmoja wa wanaotajwa kuwa wanachama wa CHADEMA ambao wamehamia CCM, Bw. Ayub Thomas Malima, alikuwa ni Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Sengerema, huu ni uongo na upotoshaji mkubwa, lakini ni aibu kubwa kwa CCM na serikali yake kwa sababu umefanywa kwa maelekezo na chini ya Waziri Ngeleja.
  Ukweli ni kwamba, Bw. Malima alivuliwa uongozi na uanachama tangu Julai 20, 2010, katika Mkutano Mkuu ulioitishwa kujadili utovu wa nidhamu wa bwana huyo. Moja ya tuhuma zilizowasilishwa kwenye mkutano wa maamuzi ni kubainika kwa mipango yake ya kujipatia fedha kutoka kwa mgombea ubunge wa CCM, William Ngeleja ili amfanyie hujuma na kumwangusha mgombea ambaye angesimamishwa na CHADEMA.

  Kila mtu anayefuatilia siasa za Sengerema tangu wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka jana, mpaka sasa anafahamu hali ya Ngeleja ilivyokuwa ya hati hati kuweza kurudi bungeni, kutokana na chama chake na yeye mwenyewe kuchokwa na wananchi.
  Kwa hiyo moja ya mbinu kabambe ilikuwa ni kuhakikisha kila njia inatumika, kuhakikisha anapita bila kupingwa, akiogopa kubwagwa.

  Kwa umakini wa CHADEMA kama tulivyosema hapo juu, chama kiliweza kujua hata mipango ya hujuma hizo ilipokuwa inafanyika. Ilikuwa ikifanyika katika moja ya hoteli mjini hapa iliyopo Barabara ya Kamanga. CHADEMA kilikuwa na ushahidi mkubwa juu ya njama hizo, ikiwemo sauti zilizorekodiwa na hata wajumbe aliowaita ili wamsaidie kufanikisha suala hilo, bahati nzuri walikuwa waaminifu na wapambanaji wa kweli, hivyo walileta taarifa zote.

  Baada ya wajumbe kumvua uanachama, Kamati Tendaji ya Jimbo la Sengerema ilimteua Ndugu Said Shabaan kukaimu nafasi ya Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Sengerema ambaye anaendelea kukaimu hadi leo.
  Sarah Mathayo, siyo Katibu wa BAWACHA kama ilivyoripotiwa katika vyombo vya habari kadhaa, bali ni mke wa Katibu wa Wilaya (Kesy Misalaba) ambaye yeye pamoja na mmewe wana tuhuma ndani ya chama kuhusika kugawa fedha, tisheti na chumvi, vitu vilivyotolewa na CCM ili kuwapatia wapiga kura. Kiongozi pekee wa Wilaya wa BAWACHA ni Bi. Agnes F, ambaye ni Mratibu. CHADEMA hatuna cheo cha katibu wala mwenyekiti wa BAWACHA Wilaya kwa mujibu wa katiba yetu. Hii yote inathibitisha namna uongo huo ulivyo mkubwa!

  Mwenyekiti wa BAVICHA Wilaya ya Sengerema ni Deus Juma, ambaye mpaka tamko hili linapotolewa yuko kazini, akitekeleza majukumu yake kama ilivyo kawaida ya CHADEMA, hivyo aliyetajwa katika vyombo vya habari, Stanslaus Pastory kuwa ni Mwenyekiti wa BAVICHA ni uongo mkubwa.
  Baadhi ya watu hao waliokimbia majukumu ya kutumikia umma, kwa sababu ya uroho wao na kuwasaidia wananchi kuijua rangi yao halisi, walishafukuzwa siku nyingi kwa sababu walikiuka taratibu za chama kwenda mahakamani kupinga uteuzi wa Diwani wa Viti Maalum, Bi. Sarah P. Nyanda.

  Kiuhalisia, waliowahi kuwa wanachama wa CHADEMA Sengerema waliovutana na akina Ngeleja kwenda safari moja ya kifo cha CCM, ni Ayub Malima na mke wake, Bi. Luci Mussa na Kesi Misalaba na mke wake, Bi. Sarah Mathayo, wengine waliotajwa katika vyombo vya habari kuwa ni wanachama wa CHADEMA wala hata hatujui uanachama wao unafanana vipi, maana hawakuwahi kuwa wanachama wa chama hiki makini.
  Chama kinapanga kufanya mikutano ya hadhara wilaya nzima ili kuwafikishia ukweli wanachama na Watanzania wote wenye moyo wa dhati katika mapambano ya kweli ya awamu ya pili, kuipigania nchi yao inayomalizwa na chama kilichofikia mwisho wa kufikiri na kuongoza.

  Tuwaambie Ngeleja, Mgenja na wenzao wote katika mpango huo na CCM kwa ujumla, kuwa chama chao kinaumwa ugonjwa wa Nambulila ambao watu wa Iringa wanajua. Mtu anakuwa ni mzima, lakini hajiwezi kabisa kuzungumza. Yeye anajiona kuwa ni mzima, lakini wenzake wanaona tayari ni mfu. Hivyo wanambeba kwenda kumzika akingali mzima lakini hawezi kutamka kuwa yeye ni mzima, mpaka anazikwa akingali hai.

  CCM waulize ugonjwa huo huwapata watu wenye makosa gani. CCM inaugua ugonjwa huo kwa makosa hayo hayo ambayo imefanya kwa Watanzania. Isubiri kuzikwa ikijiona!
  Imetolewa leo, Januari 7, 2012


  Said Shaaban
  Kaimu Mwenyekiti wa CHADEMA, Sengerema
   
Loading...