William Ngeleja arejesha fedha za mgao wa Escrow kiasi cha Tsh Milioni 40.4

Vizuri sana!
Naona amesoma alama za nyakati!
Kwani utawala wa Rais Magufuli umemgaya!
Ila jimbo la Sengerema,2020 linaenda kwa Tabasamu!
Ajiandae kuliangalia Bunge kwenye tv!

Nilitegemea ungeshauri avuliwe nyadhifa zote, na ashitakiwe kwa kosa la kumsaidia mhujumu uchumi RUGE kutakatisha fedha zake... na pia itolewe amri ya kufuatiliwa vyanzo vyake vya mapato na ikibainika vimepatikana kwa kiasi kikubwa kwa kutumia madaraka vibaya basi afilisiwe...

kuukosa ubunge tu eti 2020 haiwezi kuwa adhabu kwa watu kama hawa..
 
Kinachonishangaza ni kwanini asimrejeshee Rugemalila ??sababu ndo aliyempa zawadi na pe sa tuliambiwa sio za uma
Amrudishie aliye mpa zawadi
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Habari wanaJF,

Waziri wa zamani wa Nishati na Madini na Mbunge wa Jimbo la Sengerema, William Ngeleja amerejesha rasmi Serikalini fedha alizozipokea kutoka kwa James Rugemalira mnamo tarehe 12/2/2014 katika mgao wa Escrow ambazo ni kiasi cha Shilingi Milioni 40.4 ili kukwepa kuendelea kuandamwa na kashfa hiyo.

Ngeleja amesema kuwa ''Nimeamua kurejesha fedha hizi hata kama aliyenipa msaada bado ni mtuhumiwa tu, kwa sababu sitaki kuwa sehemu ya kashfa/tuhuma hizo'' Ngeleja.

'Leo nina zaidi ya miaka 12 nikiwa kiongozi wa Umma lakini sijawahi kukumbwa na kashfa ya rushwa au ufisadi.

Kwa vile sasa imedhihirika kwamba aliyenipa msaada huu anatuhumiwa kwenye kashfa ya akaunti ya ESCROW nimeamua kuchukua hatua.

Kupokea msaada ni jambo la kawaida, ila ikibainika kuna harufu ya uchafu hata kama haujathibitishwa na vyombo husika ni vyema kujiepusha nao.

Nimerudisha fedha hizi ili kulinda maslahi ya nchi yangu na heshima ya chama changu, Serikali, wanasengerema, familia yangu na heshima yangu.

Nimepima na kutafakari, na hatimaye nimeamua, kwa hiari yangu mwenyewe, kurejesha kiasi cha Milioni 40.4 serikalini.

Kama umeamua kurudisha kwanini urudishe TRA?

Kwanini hukuona haki umrudishie aliyekupa? Au umemhukumu kabla kuwa ni za serikali? Weka pay in slip tukmwamini zaidi.

Je huyo mhesimiwa hakupata tioka stanbic kweli?
 
wewe nae! hivi kama alipokea msaada halalii kwanini arudishe? Nani aliyemshauri arudishe sasa?
amemrudishia nani? kama serikali kwanini airudishe serikalini na sio kwa aliyempa?

Kama ni serikalini hivi tra wamepokea kama malipo ya kitu gani?amepewa risiti?
either baada ya hii maneno kuwa mingi,hataki mashida shida kwahiyo kaamua kurudisha ama atakuwa amesetiwa kwa ajili ya kick ili akickstart chain reaction ya watu kurudisha hela,mwisho wa siku watu waseme si mmeona,niliwambia pesa ya serekali haipotei labda apotee mtu
 
Sasa hela alipewa na TRA au na RUGEMALIRA?

Sent from my GT-N7105 using JamiiForums mobile app
 
hakuna sheria inamzuia mbunge kupokea contribution toka kwa private entity ama mtu yeyote yule,as long as zinalipiwa kodi,etc.
Tatizo wabongo tunapenda mno kuhukumu kabla sheria haijafuata mkondo wake ,tunafurahi sana mtu akipata majanga,

sasa hata tukisema labda ilikuwa rushwa,ngeleja katumiwa rushwa ili afanye favour ipi wakati kipindi anatumiwa alikuwa tayari si waziri wa nishati?,

au jiulize mfano askofu kilaini nae alipewa rushwa ili atoe favour ipi kwa Ruge?.

Haya mambo mbona ukijiuliza tu jibu liko wazi,
Hiyo hela angeingiziwa kwenye akaunt ya mfuko wa jimbo saww,hela anaingiziwa kwenye akaunt yake binafs hapo utasema ameitumia kwenye maendeleo ya jimbo?

May Allah bless Me and You
 
Kurudisha hela tu peke yake haitoshi.

Mshikwa na ngozi hapaswi kurudisha ngozi tu na kesi kumalizika.
 
Alipewa pesa nyingi zaidi ya hizo alizorejesha. Nyingine ziko wapi?
 
Aliyempa ni Rugemalira, iweje arudishe serikalini?
Shangaa sasa. Ila ni game linachezwa. Hapa wanaandaa mazingira ya kusema zile fedha hazikuwa za Rugemalira, kwa hiyo yeye na wote waliopeea ule mtonyo inaubidi waurudishe kwa bwana Magu. Sasa kama Mama Tibaijuka ile B na ushee aliikabidhi kule shuleni (I doubt) wakanunulia tofali, imekula kwao. Majaji wa kesi hii wana wakati mgumu sana. No wonder wengi wao siku hizi wanajiombea kustaafu mapema wasije wakafa kwa pressure uzeeni kabla ya siku zao.
 
Kazi imeanza, hizi pesa JK alisema sio za umma sasa kwanini wanamhangaisha mzee Rugemarila?

JK alikua rais lakini napata mashaka juu ya uadilifu wake, upande wa kutumia busara katika maamuzi alijitahidi namsifu.
Kumuongelea Jk kwa sasa ni kupoteza nguvu zako
Huyo ngeleja alitakiwa aeleze na kuonesha msaada ulikuwa wa nini,halafu kama anamiini alempa ni bado mtuhumiwa,kwa nini karudisha serikalini?
Mijizi awamu hii itapata tabu sana
 
Kazi imeanza, hizi pesa JK alisema sio za umma sasa kwanini wanamhangaisha mzee Rugemarila?

JK alikua rais lakini napata mashaka juu ya uadilifu wake, upande wa kutumia busara katika maamuzi alijitahidi namsifu.
Wakitajwa waliochukua zile za STANBIC na mmiliki wa Simba Trust basi Nchi itatetemeka!
 
Karudisha exact amount aliyochukua 40.2mil sasa waliopewa 1.6bil sijui kama nao watarudisha. Hapa Ndo pale unaposhukuru Mungu ulipata mgao Mdogo, ila bado ni fisadi
Alipaswa arudishe na riba tena kubwa kwakuwa amekaa nayo kwa miaka mitatu na nusu na aswekwe jela.

Na hao wengine wanaweza wasirudishe kwakuwa wanaogopwa.

WEZI WA MALI ZA UMA, MAFISADI HAO WOTE WA CCM WATIWE MBARONI.

La sivyo ni sawa na kucheza makida.
 
Habari wanaJF,

Waziri wa zamani wa Nishati na Madini na Mbunge wa Jimbo la Sengerema, William Ngeleja amerejesha rasmi Serikalini fedha alizozipokea kutoka kwa James Rugemalira mnamo tarehe 12/2/2014 katika mgao wa Escrow ambazo ni kiasi cha Shilingi Milioni 40.4 ili kukwepa kuendelea kuandamwa na kashfa hiyo.

Ngeleja amesema kuwa ''Nimeamua kurejesha fedha hizi hata kama aliyenipa msaada bado ni mtuhumiwa tu, kwa sababu sitaki kuwa sehemu ya kashfa/tuhuma hizo'' Ngeleja.

'Leo nina zaidi ya miaka 12 nikiwa kiongozi wa Umma lakini sijawahi kukumbwa na kashfa ya rushwa au ufisadi.

Kwa vile sasa imedhihirika kwamba aliyenipa msaada huu anatuhumiwa kwenye kashfa ya akaunti ya ESCROW nimeamua kuchukua hatua.

Kupokea msaada ni jambo la kawaida, ila ikibainika kuna harufu ya uchafu hata kama haujathibitishwa na vyombo husika ni vyema kujiepusha nao.

Nimerudisha fedha hizi ili kulinda maslahi ya nchi yangu na heshima ya chama changu, Serikali, wanasengerema, familia yangu na heshima yangu.

Nimepima na kutafakari, na hatimaye nimeamua, kwa hiari yangu mwenyewe, kurejesha kiasi cha Milioni 40.4 serikalini.

Anarudishaje serikalini wakati alipewa na Ruge? Angemrudishia mwenyewe, aache unafiki. Hiyo hela bila hata kufanya biashara, ukiiweka miaka 3 kwenye fixed account unapata at least 55M.

Sent from my E2105 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom