William Malecela kajiondoa JF kwa sababu ya ITIKADI. Zitto ndani ya ndege ya JK ni us

Status
Not open for further replies.

Warue

JF-Expert Member
Aug 9, 2012
423
809
Leo star tv William Malecela Kasema alikuwa moja wa waanzilishi wa JF lakini alilazimika kujiondoa kwa sababu ya Itikadi ya kisiasa. Je Zito kuandamana na JK kwenda Ethiopia inatoa picha gani?. Je aoni kwamba wafuasi wake wanaonekana wamepotea?. The only trust I had for him is gone.
 
Mbona mada inaonekana kama ya Le Mutuz kujiondoa JF ila hiyo hujaidadavua vya kutosha umejikita kwa Zitto? Hebu lete alichokizema William kuhusu kuwa mwanzilishi wa JF na kujitoa kwa sababu ya itikadi za siasa. Itikadi gani hizo?
 
Leo star tv William Malecela
Kasema alikuwa moja wa waanzilishi wa JF lakini alilazimika kujiondoa
kwa sababu ya Itikadi ya kisiasa. Je Zito kuandamana na JK kwenda
Ethiopia inatoa picha gani?. Je aoni kwamba wafuasi wake wanaonekana
wamepotea?. The only trust I had for him is gone.

The same 2 me mkubwa.
 
Katika kipindi cha StarTV Wiliam Malecela amefunguka ya kuwa kujiondoa JF, "KUJIONDOA JF KUNATOKANA NA TOFAUTI ZA KIITIKADI".

Inavyofahamika JF watu wote au washiriki wote wanashiriki katika hoja mbalimbali kwa mstakabali wa kulijenga taifa letu kukosoana, kutoa mawazo n.k bila kujali itikadi, jinsia, kabila, dini n.k.

Kauli ya Mh. William Malecela imethibitisha kitu kimoja sera ya CCM kinyume ya mahubiri yao majukwaani ya kudumisha upendo,mshikamano bila kujali itikadi, jinsia, kabila,dini n.k. Kama umeondoka kwa sababu za kiitikadi hapa alama ya kuuliza ???????.

Na picha ambayo naipata ni kwamba CCM midahalo, kukosoana n.k. HAVITAKIWI ili kupata uongozi wa CCM unapashwa kukaakimya katika kukikosoa chama CCM ama kuyataja maovu yake.

Nafikiri hii ni moja ya masharti ambayo yamekusukuma kutoka JF.
 
Umesahau ya Tido Mhando,tbc na kipind cha Mchakato majimbon,wamekwisha...
 
Katika maisha jambo zuri na endelevu kwa mtaka maendeleo ni kuamini kuwa kuna wengine wanaojua zaidi yako hivyo utakuwa kubali kukosolewa na hatimaye wazo zuri na endelevu katika utatuzi wa changamoto mbalimbali za kidunia. Nadhani ndugu zangu wa ccmwanakosoa kwa kuwavamia wanaotoa hoja juu yao (person attack) badala ya kujibu hoja ni njia ya kuelekea kuizika ccm na kuifanya kuwa legelege, viongozi legelege matokeo yake kwa kuwa ni chama kinachoongoza dola ni kuwa na taifa legelege.
 
uko ni kuogopa hoja zenye mashiko kwani kiongozi imara na mwenye msimamo hawezi kufanya hivyo eti kwa kuogopa kutokubaliana,hapa mimi nawatahadharisha ccm kuwa wakizidi kumpatia vyeo siku moja akishindwa kukubaliana na hoja zao ataondoka tu so wasimwamini na hata cdm akija asipewe nafasi,the guy is not stable
 
Binafsi yangu nilikuwa sifaidiki chochote na uwepo wake hapa jukwaani maana muda mwingi alikuwa ana utumia kwa ajili ya kujisifu na kutetea mambo ya ajabu ajabu yasiyo kuwa na tija kwa mustakabali wa taifa letu!

Kuna mjadala ulisha wekwa kuhusu tabia zake za kuanika picha zake na wadada wakiwa viwanja wakijirusha kwenye blog yake. Nadhani huu ndio muda muafaka wa yeye kwenda kuendeleze blog yake ya madada poa home of great thinkers viatu vimembana!

Sent from BlackBerry 8520 authorized by JamiiForums
 
Nilipata bahati ya kusafiri naye gari moja for long trip toka Dodoma mpaka Dar na tulizungumzia kujitoa kwake, kwa vile sababu zake pia ameisha ziwasilisha rasmi kwa uongozi wa jf, kiukweli, sio za kupuuzwa!.

Kwa vile mazungumzo yetu hayakuwa rasmi, kama nilivyoongea na Dr. Slaa, sio busara kuyaleta humu ila hoja za William sio za kupuuzwa.
 
Aje basi tudiscuss, akijichimbia huko vichochoroni tutajuaje kama anahoja.

Akumbuke kuwa MWANAUME HASUSI ANAPAMBANA.

Come on mpambanaji William
 
Nilipata bahati ya kusafiri naye gari moja for long trip toka Dodoma mpaka Dar na tulizungumzia kujitoa kwake, kwa vile sababu zake pia ameisha ziwasilisha rasmi kwa uongozi wa jf, kiukweli, sio za kupuuzwa!.

Kwa vile mazungumzo yetu hayakuwa rasmi, kama nilivyoongea na Dr. Slaa, sio busara kuyaleta humu ila hoja za William sio za kupuuzwa.

Hata sijui nikuelewe vipi..
Lakini unanishangaza mno...
Ulipata 'bahati' really ?

JF si inatambulika ni 'user generated contents'?
uongozi wa Jf hauwezi lazimisha wana JF 'wampende au wamfagilie mtu'
Kama kaona hawezi tu 'challenges za watu wa jf' ataweza vipi challenges wa wananchi anaotaka kuwaongoza?
Huu ugonjwa wa 'entitlement' na wewe umeanza 'kuushikia bango' ?????
seriously ?????
 
Ni mambo ninayojianda kuyasikia kwa viongozi wengi toka ccm kwani jf imekuwa ikianika maovu yao mengi sana
 
Nilipata bahati ya kusafiri naye gari moja for long trip toka Dodoma mpaka Dar na tulizungumzia kujitoa kwake, kwa vile sababu zake pia ameisha ziwasilisha rasmi kwa uongozi wa jf, kiukweli, sio za kupuuzwa!.

Kwa vile mazungumzo yetu hayakuwa rasmi, kama nilivyoongea na Dr. Slaa, sio busara kuyaleta humu ila hoja za William sio za kupuuzwa.

Wewe nawe! Kuna umuhimu gani sasa wa kutuambia kwamba umesafiri naye na ukaongea naye kama hutaki kutueleza mlichoongea? Unapenda sifa eeeh
 
huyu mtu hana hoja! nimemsikia star tv. mwacheni aende amezidi kujigamba! pia nafikiri atapata muda mzuri wa kuwatumia makahaba wake!
 
Huyu (WM) anashangaza sana, kwani wakati anaingia hapa alienda kutangaza kwenye sahara communications!! kama aliingia kimya kimya kuna haja gani ya kubeba matalumbeta wakati anajitoa? JF akili kubwa.............
 
Status
Not open for further replies.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom