William Erio: Mwisho wa Enzi kwa Boss wa NSSF au Mwanzo Mpya?

Zaidi ya yote ili kumkomoa kahyarara alitia ubaya kwenye miwa ili isiote kahyarara aonekane haja perfom
Wazito PPF wachota 'vijisenti'

Mwandishi Wetu Mei 7, 2008
Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo

Walipwa kama wastaafu, kisha warudi kazini

WAKURUGENZI kadhaa wa Mfuko wa Pesheni ya Mashirika ya Umma (PPF), wamejilipa mamilioni ya fedha, ikiwa ni mafao yao ya kustaafu kazi, lakini imebainika kuwa wanaendelea na nyadhifa zao licha ya kujilipa.

Habari ambazo Raia Mwema imezipata wiki hii zinasema kuwa mafao ya wakurugenzi hao yanafikia kati ya Sh. milioni 130 na 220 kwa kila mmoja, kiwango ambacho kinafikia jumla ya Sh. bilioni 1.2, kilichotolewa na PPF kwa 'wastaafu' hao.

Raia Mwema imearifiwa kuwa malipo hayo yamefanyika kwa kufuata utaratibu uitwao Group Endowment Scheme, ambao unahusu mafao ya wafanyakazi yanayopaswa kutolewa kwa mtumishi anapostaafu kazi katika PPF.

Kwa mujibu wa habari hizo, chini ya mpango wa Group Endowment Scheme, wafanyakazi hukubaliana na mwajiri kabla ya kuanza kazi, ambapo shirika linakuwa linachangia kiasi fulani cha fedha kama akiba ya mfanyakazi, ambayo hupewa mara anapostaafu.

"Mnakubaliana wewe mfanyakazi na mwajiri. Ni kama mkataba wa aina fulani. Shirika linatoa fungu, linakuchangia…Unapoondoka kazini wakati unastaafu, unapewa fedha zako ili zikusaidie kwenye maisha yako mengine.

"Ukipewa fedha chini ya utaratibu wa Group Endowment Scheme, hatutarajii kuona mhusika anabaki kazini. Kama kuna watu wanafanya hivyo, basi wanauhujumu utaratibu huu," alisema Mkurugenzi Mkuu wa zamani wa PPF, Naftali Nsemwa, ambaye aliombwa na Raia Mwema kutoa ufafanuzi wa jinsi mpango huo unavyofanya kazi.

Lakini Raia Mwema imeambiwa kwamba katika jambo ambalo linashangaza, wakurugenzi hao sita wa PPF wamejilipa mafao hayo ya Sh. bilioni 1.2, kwa maana ya kustaafu, lakini hadi jana Jumanne walikuwa wakiendelea na kazi, wakiwa tayari wameweka mafao yao vibindoni.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Badru Msangi, alipoulizwa kuhusu suala hilo, alikiri kuwapo kwa utaratibu wa Group Endowment Scheme, lakini akakataa kuzungumza zaidi kwa maelezo kuwa yeye si msemaji wa PPF, bali Mkurugenzi Mkuu mwenyewe, William Erio ambaye yuko safarini Afrika Kusini.

Hata baada ya kumsihi azungumze, Msangi alisema: "Msubiri Msemaji wa Shirika, ambaye ni Mkurugenzi Mkuu. Atakuwepo ofisini wiki ijayo. Unapotaka sisi ndio tuzungumze, hututakii mema, unataka tufukuzwe kazi."

Mwenyekiti wa Bodi ya PPF, Gray Mgonja hakupatikana jana kuzungumzia suala hilo, na hata pale Raia Mwema ilipojaribu kuwasiliana naye, simu yake ilikuwa ikiita mfululizo na baadaye ikafungwa.

Raia Mwema ina majina ya wakurugenzi hao lakini kwa kuwa haikufanikiwa kuzungumza nao kuoata maelezo ya upande wao kwa sasa hawatatajwa.

Habari zaidi zilizopatikana zinasema kulipana huko kumehojiwa na mmoja wa wajumbe wa Bodi ya PPF, Monica Mbega akitaka kujua ni nani aliyeyaidhinisha.

Mbega alihoji suala hilo katika mkutano wa Jumamosi iliyopita wa timu ya ukaguzi ya Bodi ya PPF ambayo yeye ndiye Mwenyekiti wake. Yeye na Erio, na baadhi ya wakurugenzi ambao ni wajumbe wa timu hiyo, wako safarini Afrika Kusini.

Mikataba ya Group Endowment Scheme katika PPF imekuwa ikifanyika kila baada ya miaka mitatu, na mwenye kufaidika na mpango huo anapaswa kuwa awe anastaafu na kuondoka kabisa katika ajira ya PPF.

.
Vijisenti vyaigawa PPF

Waandishi Wetu Mei 7, 2008
Raia Mwema

KUNA utata wa dhahiri katika Mfuko wa Pensheni ya Mashirika ya Umma (PPF), uliogubikwa na maamuzi ya kutatanisha, ikiwa ni pamoja na mafao ya wakurugenzi sita ‘waliostaafu' kutokuwamo kwenye bajeti ya shirika kwa mwaka huu.

Kumekuwa pia na kauli za kupingana, baadhi zikitaka waajiriwa wanaostaafu chini ya utaratibu wa Group Endowment Scheme, wapewe mafao mara ajira zao zinapokoma, na nyingine zikitaka mafao hayo yatolewe hata kama mfanyakazi anaendelea na ajira.

Taarifa zinasema kwamba lengo kuu la utaratibu wa Group Endowment Scheme lilikuwa ni kutoa zawadi kwa ustaafu na si kama mafao ya wafanyakazi kwa kuzingatia mikataba ya ajira, kwa kuwa utaratibu huo si sehemu ya marupurupu ya mwisho wa kila mkataba.

"Utaratibu wa Group Endowment Scheme ufanyike mwisho wa ajira ili kuhakikisha kuwa wafanyakazi wazuri na wazoefu wanaheshimu kanuni na taratibu muda wote wa ajira, ili kuhakikisha hawafutwi kazi kabla ya kufikia kikomo cha ajira.

"Utaratibu wa Group Endowment si wa kisheria bali ni tuzo maalum ya kustaafu kazi...haitakiwi kulipwa wakati huu kwa wafanyakazi watajwa, ambao wataendelea na ajira katika Mfuko (PPF). Ni utaratibu unaodhibiti nidhamu kwa wafanyakazi ili waepuke kufukuzwa. Kuwalipa wakati huu itakuwa ni kumomonyoa kusudio lake la awali," unasema waraka mmoja ambao Raia Mwema imefanikiwa kuuona.

Lakini taarifa ya PPF kwa umma, inasema kwamba wakurugenzi sita wa PPF walilipwa mafao ya Group Endowment, na kwamba malipo yalifanyika kufuatia kumalizika kwa mikataba yao ya ajira, ambayo ilimalizika Machi 31, mwaka huu, kwa wakurugenzi watano na Aprili 30, mwaka huu, kwa mkurugenzi mmoja.

"Ifahamike zaidi kuwa kufuatia kumalizika kwa ajira hizo, wakurugenzi hao waliomba kazi tena na Bodi (ya PPF) ikaridhia waajiriwe upya kuanzia tarehe 01.04.2008 kwa wakurugenzi watano na 01.05.2008 kwa mkurugenzi mmoja," inasema taarifa hiyo lakini bila kueleza hata hivyo kwamba mmoja wa wakurugenzi hao amelipwa kabla ya siku yake ya mwisho kazini kufika.

Pamoja na utata wote huo, bado Raia Mwema imedokezwa kuwa malipo yaliyofanyika, ambayo yanafikia Sh. bilioni 1.2, hayakufanywa kwa kuzingatia maamuzi yaliyofanywa kwenye bajeti ya PPF ya mwaka huu wa fedha, jambo ambalo linatia shaka kwenye mfumo wa maamuzi wa shirika hilo la umma.

Bajeti iliyopitishwa kwa mwaka 2008 huu wa fedha, ambayo imo kwenye kifungu namba 3.1.19 cha Group Endowment Expenses ni Sh. 1,730,187,000, lakini ukapitishwa uamuzi kwamba hakuna fedha itakayolipwa mwaka huu labda kama mfanyakazi atakua anacha kabisa ajira katika Mfuko.

Kwamba kiwango hicho hakitafaa kutolewa kwa mwaka huu, na badala yake kinapaswa kufanywa wakati mwajiriwa anapoacha kazi katika PPF.

Mgongano wa taarifa za ndani ya PPF baina ya mabosi wa shirika ni kielelezo kingine kwamba kuna mchezo mbaya unaofanyika, ikiwa ni pamoja na kujinufaisha kwa kisingizio cha "kwa mujibu wa mikataba, kanuni za utumishi za Mfuko na idhini ya Bodi ya Wadhamini."

Wakurugenzi hao sita, ambao wamelipwa mafao na kuendelea tena na kazi, walisaini mikataba ya miaka mitano ya kufanya kazi katika shirika hilo.

Mafao ya wakurugenzi hao yanafikia kati ya Sh. milioni 130 na 220 kwa kila mmoja, kiwango ambacho kinafikia jumla ya Sh. bilioni 1.2, kilichotolewa na PPF kwa ‘wastaafu' hao.

Chini ya mpango wa Group Endowment Scheme, wafanyakazi hukubaliana na mwajiri kabla ya kuanza kazi, ambapo shirika linakuwa linachangia kiasi fulani cha fedha kama akiba ya mfanyakazi, ambayo hupewa mara anapostaafu.

Raia Mwema ina majina ya wakurugenzi hao lakini kwa kuwa haikufanikiwa kuzungumza nao kupata maelezo ya upande wao kwa sasa hawatatajwa.

1. Bw. William Chenza (Mkurugenzi): Huyu alifikishwa mbele ya Bodi ili afukuzwe lakini bodi ikaona hakukua na sababu za kumfukuza wakati huo. Baada ya hapo akawa hashirikishwi kwenye kazi za uwekezaji na mipango. Mazingira ya kazi kwa Bw. Chenza yalikuwa magumu sana akaacha kazi. Kwa sasa baada ya kuona hawezi kuajiriwa ameamua kuwa mjariamali na sasa anaendesha shule.

2. Bw. Oscar Mwachang'a(Mkurugenzi) : Huyu alifariki tayari akiwa amefikishwa mbele ya Bodi ili afukuzwe kazi. Alifariki kabla hajafukuzwa kazi. (kifo cha kawaida)

3. Bw. Michael Mjinja (Mkurugenzi): Huyu alifikishwa mbele ya Bodi ili afukuzwe kazi. Bodi ilikataa na akarudi kazini lakini akawa anafanya kazi katika mazingira magumu sana. Aliwekwa pembeni kwenye mambo mengi. Hatimaye alikuja kufukuzwa "technically". Kurugenzi yake iliunganishwa na Kurugenzi nyingine akaambiwa akitaka aombe. Aliomba kazi hiyo akaitwa kwenye interview lakini akashindwa na msaidizi wake.

4. Bw. Baduru Msangi: (Mkurugenzi) Mzee huyu bahati mbaya hakuwa amempenda muda mrefu tu. Lakini kwa kuwa mzee huyu alikuwa hana makuu na watu hakuweza kupata sababu za kumshitaki kwenye bodi. Yeye aliondoka technically. Idara yake iliunganishwa naye kama ilivyokua kwa Bw. Mjinja akaambiwa akitaka aombe. Aliomba akaitwa kwenye interview akapigwa chini.

5. Bi. Irene Isaka (Meneja): Huyu baada ya Bw. Chenza kuondoka yeye ndiyo alikuwa awe Mkurugenzi, alienda Benki ya Stanbic na baadae SSRa ambako sasa ni DG wa SSRA.

6. Bi Carina Wangwe (Mkurugenzi): Ameenda SSRA (hajafukuzwa).

7. Bw Emmanuel Kakuyu (Meneja): Aliondolewa kwa tuhuma mbalimbali. Kumekuwa na madai kwamba yeye ndiye anatuhumiwa kutoa siri nje.

8. Bi Siriel Mchembe (Meneja): Ameachishwa kazi akituhumiwa kutoa siri nje ya PPF.

9. Bw. Kedron Mbwilo (Meneja); Alikua idara ya Uhasibu akahamishiwa idara nyingine kabla ya kuhamishiwa Mbeya kabla ya kuondolewa kazini moja kwa moja.

Erio hajaanza wizi, na visasi leo,
Huyu ni swa na shetani popote anapoenda.
Enyi FCC staff jiandaeni
 
Unasema, “...Hili alilionyesha sana kipindi ameteuliwa kwenda NSSF ambapo licha ya kuhamisha hamisha wafanyakazi lundo waliokuwa wazoefu hapo NSSF na kuwapeleka Serikali Kuu, Halimashauri n.k alihakikisha anabeba viongozi aliokuwa nao PPF na kuhamia nao wote NSSF...” Really?

Mkurugenzi wa NSSF aliwezaje kuhamisha wafanyakazi kutoka NSSF kwenda Serikali Kuu na halmashauri? Wafanyakazi wa NSSF nao wako chini ya Civil Service?
Watu wa majungu wanajikanyaga kanyaga tu.
Sijui mamlaka hayo aliyatoa wapi bwana Erio?!!
Anapelekaje watu sehemu ambayo hana mamlaka nayo ya kufanya uhamisho au ajira?
 
Watu wa majungu wanajikanyaga kanyaga tu.
Sijui mamlaka hayo aliyatoa wapi bwana Erio?!!
Anapelekaje watu sehemu ambayo hana mamlaka nayo ya kufanya uhamisho au ajira?
Ndyo ukweli wenyewe, Erio hata huko ppf alinyanyasa sana watu waliokua wanampinga kwa uungu mtu na wizi wake
 
Pitia ushahidi ulowekwa hapo juu
Namaanisha Erio alitoa wapi mamlaka ya kuhamishia watu Halmashauri?
Alikuwa na mamlaka ya kuajiri watu toka PSPF hiyo ipo wazi na dhahiri.
Ukiona hivyo ujue kuna mwenye mamlaka hayo makibwa kuliko Erio aliyefanya hivyo.
 
Ndyo ukweli wenyewe, Erio hata huko ppf alinyanyasa sana watu waliokua wanampinga kwa uungu mtu na wizi wake
Alipelekaje watu Halmashauri wakati ajira za Halmshauri hazikuwa chini ya mamlaka yake?
 
Namaanisha Erio alitoa wapi mamlaka ya kuhamishia watu Halmashauri?
Alikuwa na mamlaka ya kuajiri watu toka PSPF hiyo ipo wazi na dhahiri.
Ukiona hivyo ujue kuna mwenye mamlaka hayo makibwa kuliko Erio aliyefanya hivyo.
Ka initiate Erio
 
Back
Top Bottom