Will Smith(53) akiri kumruhusu rapa August Alsina(29) kutembea kimapenzi na mke wake Jada Pinket(50)

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,595
215,272
Will Smith(53) akiri kumruhusu rapa August Alsina(29) kutembea kimapenzi na mke wake Jada Pinket(50)

Ikumbukwe mwaka jana mjadala uliibuka baada ya rapa huyo kusema alishakuwa kwenye uhusiano na Jada baada ya kupewa ruhusa na mumewe, wengi walimponda Jada kuwa hakuwa mwaminifu kwenye ndoa yake, Jada alikataa Ila baadaye akakubali

Sasa Will Smith katika mahojiano mapya na GQ jarida maarufu la lifestyle za wanaume, amekiri kuwa ingawa yeye na Jada walifunga ndoa mwaka 1997 na ndoa yao ipo hadi sasa lakini walikubaliana kuwa na ndoa ya mahusiano ya wazi ili Kila mmoja kumruhusu mwenzie kwenda kuwa na mahusiano ya muda mfupi anapovutiwa na mtu mwingine huku wao wakiendelea kuwa wanandoa na kutimiziana majukumu yao na kuheshimiana Kama kawaida

Will Smith amesema baada ya kufunga ndoa walianza kubanana kwenye ndoa Kama walivyo wanandoa wengi kutopeana Uhuru wa kucheouka, lakini baada ya muda yaliwashinda, Will amesema Jada alikuwa na ndugu waliokuwa kwenye mahusiano ya wazi hivyo akawa anaona tangu akiwa mdogo na yeye Will alikulia katika mazingira tofauti na Jada hivyo kila mmoja akawa hayupo kamili kwa ajili ya ndoa waliyofunga ndio wakapeana Uhuru huo

Will amesema ameshakuwa kwenye mahusiano na wanawake wengine na Jada ameshakuwa na wanaume wengine lakini kikubwa kati yao ni kuaminiana, kuchepuka kwa umakini na hadi sasa upendo baina yao na kusapotiana katika mambo mengi havijawahi kabadilika

Will amesema yeye na Jada hawaamini kuwa ndoa ni kunyimana uhuru wa kufanya kinachokupa furaha lakini hamshauri mtu yeyote afuate njia yake

Wanandoa hao wamejaaliwa watoto wawili ingawa Will Smith anaye mtoto mwingine mkubwa aliyempata kabla ya kufunga ndoa na Jada
h(53) akiri kumruhusu rapa August Alsina(29) kutembea kimapenzi na mke wake Jada Pinket(50)

Ikumbukwe mwaka jana mjadala uliibuka baada ya rapa huyo kusema alishakuwa kwenye uhusiano na Jada baada ya kupewa ruhusa na mumewe, wengi walimponda Jada kuwa hakuwa mwaminifu kwenye ndoa yake, Jada alikataa Ila baadaye akakubali

Sasa Will Smith katika mahojiano mapya na GQ jarida maarufu la lifestyle za wanaume, amekiri kuwa ingawa yeye na Jada walifunga ndoa mwaka 1997 na ndoa yao ipo hadi sasa lakini walikubaliana kuwa na ndoa ya mahusiano ya wazi ili Kila mmoja kumruhusu mwenzie kwenda kuwa na mahusiano ya muda mfupi anapovutiwa na mtu mwingine huku wao wakiendelea kuwa wanandoa na kutimiziana majukumu yao na kuheshimiana Kama kawaida

Will Smith amesema baada ya kufunga ndoa walianza kubanana kwenye ndoa Kama walivyo wanandoa wengi kutopeana Uhuru wa kucheouka, lakini baada ya muda yaliwashinda, Will amesema Jada alikuwa na ndugu waliokuwa kwenye mahusiano ya wazi hivyo akawa anaona tangu akiwa mdogo na yeye Will alikulia katika mazingira tofauti na Jada hivyo kila mmoja akawa hayupo kamili kwa ajili ya ndoa waliyofunga ndio wakapeana Uhuru huo

Will amesema ameshakuwa kwenye mahusiano na wanawake wengine na Jada ameshakuwa na wanaume wengine lakini kikubwa kati yao ni kuaminiana, kuchepuka kwa umakini na hadi sasa upendo baina yao na kusapotiana katika mambo mengi havijawahi kabadilika

Will amesema yeye na Jada hawaamini kuwa ndoa ni kunyimana uhuru wa kufanya kinachokupa furaha lakini hamshauri mtu yeyote afuate njia yake

Wanandoa hao wamejaaliwa watoto wawili ingawa Will Smith anaye mtoto mwingine mkubwa aliyempata kabla ya kufunga ndoa na Jada.

1632866292237.png
 
Alafu ikisha kuja ili ugundue nini kwa mfano yaani?
Hio aina ya ndoa huko ni kama hii hii tu.. michepuko ipo tena kwa ndoa nyingi sana na ni kitu cha kawaida. Mume na mke wote wanachepuka haswaa. Na matokeo yake ni kuumizana kila siki mmoja akigundua au akihisi, na kufanya penzi za siri na kuleteana maradhi au kufujisha mali ovyo.
 
Mmh wewe ulishasikia mume anamruhusu mchepuko kumla mkewe huku Afrika?
 
Hamruhusu kabisaa .. lakini wanawake wanachepuka anyway kisirisiri na mwisho wa siku ndoa zinavunjika na watoto ndio wanaumia. Bora hata waMarekani wakiona ndoa haiendi, wanafanya kama hivyo Will Smith na mkewe wamefanya ili kila mmoja wao awe na furaha, na ndoa isivunjike na watoto waendelee kulelewa na wazazi wote vizuri.
 
Open relationship mbona hata Bongo ipo sana tu...

Ni zile utasikia "wewe fanya mambo yako, nami usiniingilie kwenye mambo yangu", na kweli, kinachoendelea hapo kila mmoja na lwake!!

Sio kwamba wanaishi nyumba tofauti, hell no... sema ndoa "imeshavunjika" beyond repair!!

Back in the days nilishakuwa na demu mmoja, siku ananiambia wazazi wake wapo kwenye ndoa ya camera, sikuamini kwa sababu, nje ungeweza kudhani wapo pamoja kumbe ndani kila mmoja anaishi upande wake!!

Na hii hutokea sana kwenye ndoa za influential figures kama vile wanasiasa na wafanyabiashara ili waendelee kuudanganya umma kwamba wapo pamoja, na piahutokea kwa ndoa za Kikristo ambazo mkishajipiga kitanzi, panatakiwa pawepo na sababu za msingi hasa za kukitanzua!!
 
Back
Top Bottom