Will Kikwete make this speech?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
There is this speech that I've been dreaming recently that H.E Kikwete would give one of these days to the nation. a speech that will spark a flame and light a fire in the minds of Tanzanians... It is the speech that our dear friend "Curtis" would very well write (I bet he knows what need to be in that speech)... A speech that will not be given while sitting down or in a market arena... a speech that will stand to the level of such speeches like "Gettysburg Address", JF Kennedy Inaugural Speech, "I have a dream" or "declaration of Arusha" speech... the speech I'm thinking about will be titled like.."Tanzania, Rise my Nation", "We too have a dream", "My Country - A way Forward" etc... Oh.. I wish I could make that speech... for I know.. we just need a little spark to fire the nation...!! Oh.. my dear friends..

The problems however, is that.. he never stay at home.....
 
Endelea kuota JK anataka kusema yale madogo walala hoi wanapenda kusikia kama Serikali yake ama yeye anawageukia vibaka watafute kazi baada ya kula sahani moja na ujambazi hiyo yako endelea kuisubiri
 
Siyo hotuba zenye maneno matupu zinazohamasisha wote, bali zile zinatolewa kwa uthabiti wa moyo na ushawishi wa mawazo. Ilikuwa hotuba ya Gettysburg address ndiyo ilibadilisha wimbi la vita vya wenyewe kule Marekani, ilikuwa ni hotuba ya "Nina Njozi" iliyobadilisha kwa kiwango kikubwa mahusiano kati ya watu weusi na weupe, ilikuwa ni hotuba ya "Nia Tunayo" iliyowahamasisha watanzania kumng'oa yule nduli.. maneno yana nguvu ya kuwasha moto ndani ya mioyo ya watu na kuwafanya wajitahidi zaidi na kudhamiria makuu. Hotuba ya JFK "Usiulize nchi yako itakufanyia nini, bali jiulize wewe utaifanyia nini nchi yako" hadi leo inakumbukwa kwa kuwahamasisha Wamarekani hadi kwenda mwezini!! Hotuba ya Mandela wakati akisimama kizimbani kujitetea na kusema kuwa wazo la kupinga ubaguzi wa rangi "ni wazo ambalo lafaa kuishi kwalo, na ni wazo ambalo niko tayari kutoa maisha yangu kwake" ilimuinua toka mpigania haki wa kawaida na kumuweka kwenye anga za pekee!

Ndugu zangu niaminini JK akija na hotuba ya dhati, iliyojaa maneno ya kujaza watu imani kwao binafsi na yenye kuchochea jitihada, na kuwapa njozi inayofikika nawahakikisha moto utakaowaka Tanzania hautakuwa na mfano katika bara la Afrika. We just need a spark.. to light the fire...!
 
Je, hotuba hii niliyoitamani wakatu ule ndiyo iliyotolewa kwenye Mkutano Mkuu... ??
 
Mwanakijiji,
Jibu analo FD mtazama pande zote, ila hala hala asiwe na kengeza likamfanya aone zaidi upande mmoja.
 
Kukubalika Kwa Speech Pia Kunategemeana Na Status Ya Jamii Husika Kwa Wakati Huo Na Pia Inategemeana Na Ni Kivipi Jamii Hiyo Inamchukulia Kiongozi Huyo Kwa Wakati Huo!kama Wananchi Wana Imani Na Kiongozi Huyo Basi Historia Huandikwa Kwani Wananchi wako likely kucooperate,kuwa Motivated Na Kuiridhia Hotuba Ama Ujumbe Huo.sijapata Nafasi Ya Kufanya Tathmini Ya Status Ya Rais Kikwete Kwa Wakati Huu Anaotaka Kutoa Hotuba Hiyo!Ila based on current news wananchi hivi Sasa Wana Mixed Feelings Kwamba Wawe Na Imani Nae Ama La!Akisha kuikata Kiu Ya Maswali Nyeti Ambayo Ni Current Kabla Hajatoa Hotuba Hiyo Then Possibility Kwamba Anaweza Kutoa Historic Speech Inawezezekana!
 
Mzee Mwanakijiji,
Tatizo ni kwamba hadi sasa hivi JK anajulikana kama msanii. watu wamechoka na hotuba zenye ahadi hewa. Nadhani kinachoweza kumtoa JK katika hali hii ni kuwajibika kwake hasa ktk swala la Uhujumu Uchumi. Kama alivyosema Mangula, CCM inahitaji Sokoine mwingine..
Agizo hilo halina tofauti na kusema Lowassa hafai kabisa kama waziri mkuu. Ni lugha ya jikoni kusema Tanzania haina waziri mkuu na sivyo wengi walivyotafsiri. Hilo ndio jibu pekee ktk kuwasha cheche za moto kwa Wadanganyika.... ACTION!
Yaliyokwisha semwa na wenye hekima na busara yanatosha kabisa kwetu kuyatumia ktk vitendo hatuhitaji Martin Luther ama Mandela mwingine bali mtu wa kazi - Jemadari ambaye yuko tayari kuingia msituni.
 
Mzee Mkandara, right on.. siyo hotuba tu ya maneno matamu, bali hotuba ambayo itawasha moto wa uzalendo, itachochea jitihada, na itaonesha njia ya wapi tunataka kwenda, na hotuba hiyo inafuatiwa na vitendo vinavyoendana na maneno hayo. Waswahili walisema "mkono mtupu haulambwi".. so siyo maneno tu.. bali vitendo vinavyoendana na maneno
 
Hotuba bila vitendo ni sawa na usanii.

Ndilo tatizo kubwa, yaani ukiangalia hotuba kuna hotuba nzuri sana ambazo zimewahi kutolewa. Ndio maana wakati wa hotuba umepita.. wakati wa vitendo umefika.. waache kuzungumza sana.. ile hotuba ya "Kupaa kwa Ndege ya Tanzania" ilikuwa inavutia sana...
 
Halafu kama hutoba zenyewe zinatolewa mbele ya kadamnasi ya wanafiki ambao kwao hata "pointless" ni hoja nzito,hence makofi kila baada ya sentensi,basi mtoa hotuba anaweza kuropoka chochote kile hata kama kimejitokeza kichwani kwake muda huohuo.Laiti lile vuguvugu la kuwazomea "mawaziri walikwenda kuua sumu ya wapinzani" lingeshika hatamu kwa kila hotuba (hususan zile za tutafanya a,b,c..z BADALA ya tumefanya 1,2,3...100) basi si ajabu baadhi ya mikutano ingefunguliwa bila hotuba.

Sintashangaa pindi JK atakapomaliza muda wake (iwapo hatalazimishwa kujiuzulu kabla ya muda huo) akawa na nakala 5 tu ya hotuba zake zilizojaa ahadi.Yaani zile za wakati wa kampeni zilikuwa na hoja "mkituchagua nita....",baada ya kuchaguliwa hotuba zimekuwa "tuliahidi wakati wa kampeni kuwa tuta....na napenda kuwakikishia kuwa tuta....",na mwisho wa muhula itakuwa "tupeni tena ridhaa ya uongozi ili tukamilishe mikakati ya utekelezaji wa ahadi tulizoainisha kwenye kampeni zetu..."Hakuna matamshi makubwa mithili ya Azimio la Arusha,Azimio la Musoma,etc bali porojo juu ya porojo.

Mungu ibariki Tanzania
 
There is this speech that I've been dreaming recently that H.E Kikwete would give one of these days to the nation. a speech that will spark a flame and light a fire in the minds of Tanzanians... It is the speech that our dear friend "Curtis" would very well write (I bet he knows what need to be in that speech)... A speech that will not be given while sitting down or in a market arena... a speech that will stand to the level of such speeches like "Gettysburg Address", JF Kennedy Inaugural Speech, "I have a dream" or "declaration of Arusha" speech... the speech I'm thinking about will be titled like.."Tanzania, Rise my Nation", "We too have a dream", "My Country - A way Forward" etc... Oh.. I wish I could make that speech... for I know.. we just need a little spark to fire the nation...!! Oh.. my dear friends..

The problems however, is that.. he never stay at home.....

Maneno matupu hayavunji mfupa. Watanzania tumechoka na maneno matamu ambayo hayatupeleki kokote miaka nenda miaka rudi tumeshasikia hotuba nzuri sana lakini ikija kwenye vitendo ni ZEROOOO!. Watanzania tunataka hotuba ya kuwakikishia kwamba Tanzania hakuna mtu yeyote aliye juu ya sheria kama amefanya madudu basi sheria itaachwa ifanye vitu vyake, kama mtu amekula rushwa, ni fisadi, ametumia wadhifa wake kujilimbikizia mali basi sheria itafanya kazi yake. Kama mikataba iliyosaini haina maslahi kwa Watanzania basi ifanyiwe mabadiliko makubwa tena kwa haraka, hakuna sababu yoyote ya kusubiri miezi sita au zaidi kufanyia marekebisho mikataba hewa.

Hotuba hiyo ifuatiwe na vitendo vya ukweli kabisa ili kurudisha credibility ya Kikwete kwa Wananchi vinginevyo si tu ataondoa uwezekano wa yeye kuwa mgombea wa CCM 2010 bali pia kuiweka hatarini CCM kuwa minority party.
 
Mzee Mwanakijiji,
Hotuba ya JK alipoingia madarakani ingekuwa moja ya hotuba zinazotakiwa kuhifadhiwa. Nina hakika hawezi toa hotuba kama ile tena. Lakini kama ulivyosema mkono mtupu haulambwi, that is our President..
Unajua hata tapeli mara ya kwanza huingia kwa vishindo lakini akisha shtukiwa inabidi abadilishe mbinu zake.. JK hakutegemea kabisa kuwa Tanzania ya Nyerere, Mwinyi, Mkapa sio hii tena. Vijana mnayafanya mavituz kiasi kwamba labda anakuhitaji wewe kuziandaa hizo Hotuba zikifuatiwa na vitendo.
Trust me kama kweli kuna uchunguzi unafanyika kuhusu wizi wa BOT na hawa wahujumu cuhumi basi ni kazi ndogo sana kwa ke. Awaruhusu waandishi wa habari kuandika kila hatua ya uchunguzi huu kutokana na taarifa zinazotolewa na taasisi husika. Iwe kama vile Watergate ama kesi ya OJ.. itamsaidia sana wananchi wanapofahamu kuwa swala hili kweli linafuatiliwa na hakika ushahidi mwingine utazidi kumiminika dhidi ya wahusika.
tena basi kama ni mimi ningeomba wananchi wenye taarifa zozote ama document zozote ziunazohusiana na hujuma wazitume ktk taasisi fulani inayoongozwa na Sokoine mpya ambayo itazipitia kwanza kabla ya kuzitumia kama ushahidi dhidi ya watuhumiwa. Identity ya mtu itahifadhiwa ama kulindwa na ofisi yake mwenyewe.
Nina hakika jina lake litajikosha lenyewe maadam
 
kwa JK sidhani kama anaweza kuja na speech ya namna hiyo.
kila mmmoja na style yake ya hotuba na yake yeye ni style ya "kishkaji", hotuba kama majadiliano ya mzaha, na sio kama mamlaka.

na kabla ya kutoa hotuba ya aina hiyo kwanza na abadilishe baraza la mawaziri, kisha hata akitoa hutuba ya style gani, inaweza kuamsha "sparks" kwa wananchi.

kwa hali ya sasa, ni vigumu kupata respond nzuri kwa wananchi hata kama atatoa hutuba aliyoshushiwa kwa nyuzi kutoka mbinguni
 
Niko tayari kusaidia kuandika hotuba ya namna hiyo provided, vitendo vitaifuatia... tena bure najitolea..!
 
Niko tayari kusaidia kuandika hotuba ya namna hiyo provided, vitendo vitaifuatia... tena bure najitolea..!

Hongera kwa kuoffer support. Ila nathani Salva anaiweza hiyo kazi, lakini huo si mtizamo wa mkuu kwa sasa.kwa ile hutuba ya jana nathani ingefaa kutolewa pale Saigoni. Mkuu mpaka anasema hallo hallo!I am speecheless.
 
yaani mnakaa hapa kudiscuss eti lini rais atatoa speech ya aina fulani (memorable speech) heheheeeee, nyie kweli mmeshiba maendeleo !

am out of this thread bana !
 
Ndugu zangu niaminini JK akija na hotuba ya dhati, iliyojaa maneno ya kujaza watu imani kwao binafsi na yenye kuchochea jitihada, na kuwapa njozi inayofikika nawahakikisha moto utakaowaka Tanzania hautakuwa na mfano katika bara la Afrika. We just need a spark.. to light the fire...!

Mzee Mwanakijiji, heshima yako Mkuu!

Rais Kikwete ameshika nyazifa mbalimbali kwa kipindi kirefu sana katika maisha yake. Hata hivyo, wakati wa kampeni za uchaguzi za 2005, kuanzia yeye binafsi, na kwa wale wanaomfahamu, hakuna aliyekuwa tayari kuueleza umma wa watanzania kwa kinagaubaga sifa za ubora wa Kikwete na kazi alizozifanya katika nyazifa alizoshika ambazo zingeambatana na mifano hai. Badala yake, vyombo vya habari vya nje na ndani ya nchi vilimmwagia sifa kemkem zisizo na mahusiano yoyote na masuala ya ubora wa kuongoza nchi.

Alikwepeshwa chujio la jamii kama maswali ya moja kwa moja na waandishi wa habari, kusahiliwa au midahalo na wagombea wenzake. Ziliibuliwa sifa za ajabu kana kwamba Kikwete alikuwa amezaliwa upya na si yule aliyekuwa Waziri wetu kwa miaka mingi. Ungedhani alikuwa na mengi ya kutueleza kutokana na nyazifa alizoshika Serikalini. Ghafla, Kikwete akaanza kuvutia watu, umbo na sura yake nzuri vikapakwa rangi mpya, akaanza kuvuma, akapagaisha watu, akatumwa na Mungu, akawa mcheshi na mpenda watu, akaanza kuwa mtu wa watu n.k. Kura za maoni kutoka kwa Tido (BBC) na zile za IPP media zikasindikiza hizi sifa mpya za Kikwete. Sifa zake za kweli za utendaji kazi ambazo zilikuwa na mahusiano na uongozi hazikutajwa, Matokeo yake, Kikwete akajulikana zaidi miongoni mwa watanzania kwa sifa zake zisizo na mahusiano na uongozi wa nchi.

Hakuna mtanzania ambaye alikuwa hajuhi kuwa kambi ya Kikwete ilitumia fedha nyingi mno wakati wa kampeni. Hakuna ambaye alikuwa hajuhi kwamba utajiri wa Lowasa na baadhi ya viongozi ndani ya kambi ya Kikwete ulihitaji kupitishwa kwenye darubini kabla ya kiongozi yeyote kupewa dhamana ya kuongoza. Hata hivyo, katika hotuba yake ya kufungua Bunge pale Dodoma, Rais Kikwete alisema kuwa viongozi ambao utajiri wao unaleta wasiwasi miongoni mwa watanzania na wameupata pindi walipoteuliwa kushika nyazifa mbalimbali wangetoka kapa katika safu ya uongozi wake. Wakati anatamka hayo maneno alikwisha mteua Lowasa kuwa kiranja Mkuu wa kusimamia maneno yaliyoko kwenye hotuba zake. Hotuba yake ilionekana kuchukizwa na matumizi makubwa ya fedha katika uchaguzi. Hata hivyo, watu aliokuwa akiwahutubia na wakimshangilia, walijua kuwa pengine hakuna mgombea Urais katika historia ya nchi yetu aliyetumia fedha nyingi kama aliyekuwa anawahutubia kwa wakati huo.

Pamoja na kutambua matendo yote haya, kuna watu walituambia kuwa ile hotuba ilikuwa ni ya kuleta matumaini kwa watanzania (you got to be kidding me). Katika masuala ya majukwaa ya kisiasa kuna mahusiano ya moja kwa moja kati ya matendo ya mtu na hotuba anazozitoa. Mara nyingi, matendo na juhudi za viongozi hutangulia hotuba zao na hapo ndipo historia huwa inaandikwa. Karibu hotuba zote ulizoziorodhesha Mzee Mwanakijiji zilitanguliwa na matendo.

Kumbuka Martin kabla ya hotuba yake ya "nina njozi" alikwisha anzisha libeneke na weusi wenzake akina Mzee X huko mitaani na alilipia gharama zake. Alikwisha pokea mkong'oto na kibano cha nguvu katika matembezi ya mara kwa mara kwa juhudi zake za kutaka kuwaunganisha wazungu na weusi. Matembezi yake yalijumuisha wazungu pamoja na weusi wakiwa wameshikana mikono. Katika kilele cha ile hotuba, waliokuwepo walioanisha maneno ya mtoa hotuba (Martin) na matendo yake kabla ya hotuba. Walitambua kwa dhati kuwa hiyo ilikuwa dhati ya moyo wake ndio maana walijawa na imani juu ya hotuba yake. Kwa wamarekani (weusi na wazungu) sio rahisi kutenganisha ile hotuba na matendo ya Martin kabla ya hapo.

Mzee Madiba aliendesha libeneke mpaka kikaeleweka kabla hajakamatwa. Alikwenda nje ya nchi kupata mafunzo ya kijeshi. Aliporudi, alianzisha jeshi na kufanya uharibifu kwa kutegesha mabomu ya kulipua njia kuu za uchumi wa wazungu. Alikataa katakata kukimbia nchi kama walivyofanya akina Oliva na Mbeki. Matendo ya Mzee Madiba kabla ya ile hotuba ya " ikibidi nimejiandaa kufa kwa hilo" na hotuba yenyewe haviwezi kutenganishwa. "Baada ya maneno yale, kulitokea ukimya wa muda mrefu ndani ya Mahakama na giza nene likatanda", alisimulia mke wa marehemu Sisulu. Waliokuwepo walioanisha matendo ya Mzee Madiba kabla ya hapo na yale aliyokuwa akiyaongea pale. Walijua kuwa ile ilikuwa dhati ya moyo wake na wakawa na imani na aliyokuwa akiyasema.

Kumbuka Mzee Iddi alitushambulia mwaka 1972 kwa kile alichodai kuwa anashambulia majeshi ya msituni ya Obote. Nyerere alijiandaa na ile vita iliyoanza 1978 kwa muda mrefu sana. Hatukupata mkopo wala msaada wa maana katika vita ya Uganda. Tuliigharamia wenyewe. Hoja yangu sio kama tulipashwa kupigana vita au hapana. Ninachotaka kusema ni kuwa Nyerere alijiandaa muda mrefu kumuondoa Amin. Hata kabla ya hapo Nyerere alitambulika bayana kwa maamuzi yake ya kuamuru majeshi yetu kwenda kupigana Msumbiji na kakisiwa fulani huko Afrika. Mikakati ya kumuondoa Mzee Smith huko Zimbabwe, mapigano Angola, na vikwazo vya uchumi Afrika kusini. Hivyo basi, alipowaita wazee wa Dar na kuwaeleza "nia tunayo na nguvu tunazo" wazee walisisimka kwasababu walioanisha matendo yake ya nyuma tokea harakati za kumg'oa mkoloni mpaka siku alipokuwa anawahutubia. Waliamini kuwa ile ilikuwa dhati ya moyo wake na wakawa na imani na aliyokuwa akiyasema.

Sikatai kwamba Kikwete anaweza kutoa hotuba yenye maneno ya kujaza watu imani, lakini kutokana na mantiki niliyoielezea juu, nina shaka kama watu watajawa na imani baada ya kuyasikia hayo maneno kutoka katika hiyo hotuba ya kufikirika. Binafsi natabiri kuwa utakuwepo mwendelezo wa hotuba kutoka kwa Kikwete zinazofanana na matendo yake kabla ya hizo hotuba. Matendo yake ya jinsi alivyoingia madarakani na matendo yake ya jinsi anavyoendesha nchi yote yako wazi na yanajulikana. Binafsi sioni haja ya kuumiza kichwa kwa kujaribu kufikiria hotuba inayotofautiana na yale yanayoonekana. Binafsi naamini kuwa hizo hotuba ndio dhati ya moyo wake ingawa sina imani na anayoyaongea.
 
Back
Top Bottom