Red Giant
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 15,658
- 20,889
Bahati nzuri miaka ya juzi kati nimevutiwa kusomasoma kuhusu China hivyo nilipata mawili matatu. Hiki kitabu kimoja kilikuwa kinazungumzia mapinduzi ya AI, AI ndiko dunia inakoelekea. Unapozungumzia mapinduzi ya nne ya viwanda unazungumzia AI. Atakaye tawala AI ataishika dunia. Kwenye hii sekta US ndiyo alikuwa pioneer lakini China amecatch up na kuna uwezekano mkubwa wa kumpita US. Ili AI ifanye kazi inahitaji mabilioni ya data wanasema China kwa idadi yake ya watu na sheria zake kuhusu usiri wa data hiki ni kitu rahisi sana kwake. Kwa hiyo AI ya china ndiyo iko kwenye mazingira bora ya kustawi.
Hiki kitabu kingine (China disruptors)kinazungumzia makampuni ya China. Makampuni binafsi ndiyo huendesha uchumi wa nchi zilizoendelea. Ukiulizwa leo kati ya China na Marekani ni wapi makampuni yanapata ushindani mkubwa wa kibiashara kutoka makampuni mengine ya ndani unaweza sema US. Haiko hivyo, China kwa kila kampuni moja linalosimama kuna makampuni maelfu kadhaa yanakuwa yamekufa. China hakuna copyrights law au tuseme hazisimamiwi kihiivyo, sasa ukigundua kitu leo kesho mwenzako ameiga. Mara kakampuni kameanzishwa kameiga. Makampuni yamebuni mbinu mbalimbali, app kama we chat imebidi iwe app ya kila kitu ili kusurvive. Hizi biashara za mitandaoni, Makampuni ya China yanawekeza mtandaoni na yanajenga store(duka), yanafanya kila mbinu. Ni mazingira magumu sana kusurvive. Hilo linamaanisha nini? Linamaanisha kampuni inayoweza survive China ikitoka huku duniani hakuna wa kusimama nayo. Pia Kampuni zao zina njaa balaa, zinanunua kampuni za Marekani kama zina kichaa vile. Kitu kingine ni quality ya bidhaa, wamejifunza sana kwenye hii sekta.
Military, kwanza wanasema China hana tabia ya ubeberu(emperialism) hivyo hana haja ya kuweka mabase ya mbali na kushika sehemu za mbali. Changamoto kubwa ya kijeshi kwa China ni South China Sea na Taiwan. Hii south China Sea anagombania na mataifa mengi sana lakini wanasema kwa jinsi nchi hizi na hata Taiwan yenyewe zinavyoitegemea China kwa uchumi wao hakuna atakayethubutu kupigana au kuleta fyokofyoko japo wananunua mandege, manyambizi na kubluff. China anahakikisha wanamtegemea zaidi kiuchumi(Sun tzu anasema kumpiga adui bila kupigana ndiyo hekima kuu)
China imeendelea mpaka hapo kwa sababu ya kubadili sera zake na kuruhusu zaidi sekta binafsi kuingia kwenye uchumi. Lakini mageuzi hayo hayatoshi bado na kila siku yanafanyika ili kufanya shughuli fulani za kiuchumi zifanyike. Waandishi wanasema China bado inahitaji kufanya mapinduzi makubwa zaidi ili izidi kusonga mbele vinginevyo maajabu ya kiuchumi iliyoyapata miaka ya karibuni hayataweza kusogea mbele tena. Isipofanya mabadiliko makubwa kwenye sera zake na namna inavyoendesha mambo isahau kuipita US.
Mi nimeona nizungumzie upande wa China, ila mambo ya kuifanya Marekani ishinde au ishindwe siyaelewi vizuri, imekuwa nchi isiyotabirika, si ajabu ikatumia advantage yake(jeshi).