Wiliam Mhando what are you doing?

MVUMBUZI

JF-Expert Member
Jan 8, 2011
5,182
2,304
Mkurugenzi wa TANESCO Mr. William Mhando imebidi nikuulize hili swali " WHAT ARE YOU DOING?" wakati Arusha imegeuka DARK CITY for almost 14 hours every day for more than a week now.
Nakuuliza what are doing kwa sababu Meneja wa TANESCO Mkoa wa Arusha na team yake hawataki kutujibu kwa nini asilimia 90 ya mkoa wa Arusha hasa mjini na maeneo ya pembezoni umeme unakatika kwa almost 14 hours kila siku?

Ninakuuliza what are you doing badala ya kuwawajibisha wazembe kutoka Customer care wanapokuwa na majibu ya mizaha na utumbo wanapopigiwa simu kuulizwa tatizo la umeme Arusha linatokana na nini na litaisha lini?

Ninakuuliza "what are you doing" wakati tatizo la mgao Arusha lina kuwa kubwa badala ya kupungua.
Ninakuuliza tena what are you doing wakati tayari wakazi wa Arusha wameshaanza kulihusisha tatizo la umeme Arusha na visasi vya kisiasa huku wewe ukibaki kimya.

Tunahitaji majibu kwa sababu hapa hali ni mbaya mno kila kona hakuna umeme hasa nyakati za usiku kuanzia saa 12 jioni hadi saa 2 asubuhi. Hali hii imetengeneza mazingira mazuri kwa wezi waliokuwa wamepungua kwa muda mrefu kuanza rasmi shughuli zao.
 
yuko bize anajenga shule yake pale muheza ili akistaafu awe na chanzo cha mapato
 
Ana mikakati....

Time is running out mgonjwa mahututi unamwacha kwenye meza ya upasuaji unatoka nje kuhudhuria vikao are you sure utamkuta bado hai mkuu. Naomba aache shughuli zote aka u- attend mji wa Arusha na vitongoji vyake uko mahututi ki-umeme unapumulia oxygen.
 
Yuko kwenye mchakato! Kweli Arusha kuna matatizo ya umeme. Yaani unakatika hadi kero kuna siku umenikatikia nikiwa kwenye lift pale Silver palm.
 
yuko bize anajenga shule yake pale muheza ili akistaafu awe na chanzo cha mapato

Kilio tu na malalamiko ya watu waliokosa ajira na kipato kwa miradi yao kukosa umeme itasababisha hiyo shule iporomoke.
 
Mkurugenzi wa TANESCO Mr. William Mhando imebidi nikuulize hili swali " WHAT ARE YOU DOING?" wakati Arusha imegeuka DARK CITY for almost 14 hours every day for more than a week now.
Nakuuliza what are doing kwa sababu Meneja wa TANESCO Mkoa wa Arusha na team yake hawataki kutujibu kwa nini asilimia 90 ya mkoa wa Arusha hasa mjini na maeneo ya pembezoni umeme unakatika kwa almost 14 hours kila siku?

Ninakuuliza what are you doing badala ya kuwawajibisha wazembe kutoka Customer care wanapokuwa na majibu ya mizaha na utumbo wanapopigiwa simu kuulizwa tatizo la umeme Arusha linatokana na nini na litaisha lini?

Ninakuuliza "what are you doing" wakati tatizo la mgao Arusha lina kuwa kubwa badala ya kupungua.
Ninakuuliza tena what are you doing wakati tayari wakazi wa Arusha wameshaanza kulihusisha tatizo la umeme Arusha na visasi vya kisiasa huku wewe ukibaki kimya.

Tunahitaji majibu kwa sababu hapa hali ni mbaya mno kila kona hakuna umeme hasa nyakati za usiku kuanzia saa 12 jioni hadi saa 2 asubuhi. Hali hii imetengeneza mazingira mazuri kwa wezi waliokuwa wamepungua kwa muda mrefu kuanza rasmi shughuli zao.

Khaaa Mkuu na wewe maswali yako magumu!! Ngoja tuyapeleke kwa Badra Masoud huenda akakujibu. Unataka kumtoa mtu roho?
 
i think Mhando needs to take action ili iwe mfano kwa baadhi ya watendaji wake... in dar kinondoni north watu wa customer care wanajitahidi sana... They are really responding to calls
 
Usizungumzie ya Arusha

Hapa Dar Kuna Mgao INGAWA hawasemi Kama Mgao Unaendelea

Mnyamala, Knyama, Sinza Kila cku Lazima wakate Umeme for 8 hrz

Mgao Upo wa Kimya kimya Tanesco Hawataki kusema
 
Mhando hana la kusema, alimdanganya Ngeleja kwamba tatizo la umeme TZ litaisha na kuwa historia, Ngeleja naye akaujulisha umma wa waTZ kwa kujiamini; baada ya hapo tatizo limezidi kuwa kubwa zaidi hatimaye ameamua kukaa kimya.

Hata hivyo kwa maswali yako mkuu inabidi ajibu tu!
 
Kwa kweli hii nchi imefika mahali inaonekana kana kwamba tunacheza michezo ya kuigiza tu... hivi huko duniani wanaweza kuamini wakisikia kuwa mji muhimu kama Arusha unakosa umeme kwa saaa 14 kwa siku!
 
Khaaa Mkuu na wewe maswali yako magumu!! Ngoja tuyapeleke kwa Badra Masoud huenda akakujibu. Unataka kumtoa mtu roho?

Mkuu dhana ya uwajibikaji inapokuwa siyo tena utamaduni wetu inabidi tutumie mbinu yoyote ku-draw attention ya hawa wakubwa ili wajue kuna watu wa na suffer simply kwa sababu wao au baadhi ya team member kama MENEJA WA TANESCO ARUSHA hawaja play role zao.
 
i think Mhando needs to take action ili iwe mfano kwa baadhi ya watendaji wake... in dar kinondoni north watu wa customer care wanajitahidi sana... They are really responding to calls

Hawa ni adamant na vichwa vyao vimejaa utani na mizaha na hakuna mwenye jibu la kwa nini hali ni mbaya namna hii ya umeme. Hapa ikifika saa 12 jioni tunategemea umeme kukatika na tutausikia tena kesho saa 2 .asubuhi bila kuambiwa why. Customer Care hapa TANESCO Arusha hawana majibu na wakati mwingine wanasema umeme hatujui tatizo ni nini?
 
Mkuu dhana ya uwajibikaji inapokuwa siyo tena utamaduni wetu inabidi tutumie mbinu yoyote ku-draw attention ya hawa wakubwa ili wajue kuna watu wa na suffer simply kwa sababu wao au baadhi ya team member kama MENEJA WA TANESCO ARUSHA hawaja play role zao.

Huenda huko Arusha kuna tatizo katika uongozi wa TANESCO Mkoa. Kusema kweli kwa sasa TANESCO wanajitahidi kuhusu huduma kwa wateja si kama zamani. Mimi mwenyewe niliwahi kuharibikiwa na mita umeme ukazimika nilipiga simu wakaja fasta wakabadilisha mita wakaweka luku nikaendelea na mgao.

Washitaki tu kwa kutumia Clients' Charter yao. Kama huna nende ofisini kwao ichukue kisha uwashitaki hapohapo.
 
William Mhando, William Ngeleja wote hawana majibu...tuko kwenye mkakati, mchakato, blah blah....

Afadhali na Idrisa
 
Wabunge mtakaosoma thread hii please please mtusaidie kuliongelea kwani ni jambo la dharura na linahitaji majibu ya haraka
 
Back
Top Bottom