Uncle Rukus
JF-Expert Member
- Jun 16, 2010
- 2,415
- 398
TAARIFA ambazo zimethibitishwa na katibu wa CDM mkoa wa Mwanza Willson Mshumbusi ni kuwa Mkurugenzi wa taifa wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasi na Maendeleo (Chadema) Wilfred Rwakatare amelazwa hosipitali ya rufaa ya Bugado wadi namba J-2 chumba namba J217, baada ya kuzidiwa akiwa katika uchaguzi mdogo wa Igunga. Hata hivyo hali yake imeelezwa kuwa nzuri na bado anaendelea na matibabu yake.
Inasemekana kuwa ugonjwa unaomsumbua ni Nemonia.