Habari za kuachiwa kwa dhamana Mkurungenzi wa ulinzi na usalama wa Chadema na Mwenyekiti wa chama hicho mkoani Kagera Bw, W. M. Rwakatare maarufu hapa Bukoba kama "Egaju" zimeilipua Bukoba kwa furaha na sasa kila kona unayopita gumzo ni kuachiwa kwa mwanasiasa huyo aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la Bukoba mjini.
Habari hizo zimezagaa ghafla kupitia mitandao ya kijamii na redio za hapa Kagera, isipokuwa redio ya Mh Kagasheki, redio Kasibante jina amabalo uhusishwa sana na mvutano wa kisiasa kati ya Kagasheki na Rwakatare. Jina la utani la Rwakatare "Engaju" linamaanisha ng'ombe mkubwa mwenye pembe ndefu maarufu sana mkoani Kagera wakitokea Uganda, na jina la redio "Kasibante" linamaanisha kumfunga ng'ombe.
Honi za magari zimepigwa na vjana wengi walilipuka kwa makelele baada ya kusikia habari hizo toka redio Vision iliyoko mjini Bukoba. Vijana wengi wamesikika wakisema "tunataka kuvunja rekodi yetu wenyewe ya mapokezi, maana Ccm hata akija nani hawezi vunja rekodi ya mapokezi ya Dr Slaa" aliongeza "tunataka kuuonyesha ulimwengu kuwa tulisikitishwa na kesi ya kipuuzi lakini iliyomtesa kamanda wetu, tutaisimamisha Bukoba siku hiyo" alisema kijana mmoja mwendesha pikipiki.
Mama mmoja mfanyakazi wa sharika la posta mkoani hapa amasema "hata bosi anajua kwamba siku ya kumpokea Rwakatare hawezi kuniona kazini, najua hawezi kunitakisha ubaya nitamuaga siku mmoja kabla" Amesema ndiyo haki imetendeka lakini wanataka kuonyesha ulimwengu kwamba watenda haki ni wengi. "Tunataka kumuonyesha huyo Mwigulu wao kwamba tunapenda haki na kuwa tunamsubiri kwa hamu siku akija hapa tutamzomea kwa kihaya"
Nitaendelea kuwajuza kinachoendelea hapa Bk.