Wilfred Muganyizi Rwakatare ''Engaju" anasubiriwa kwa hamu Bukoba!

mpk

JF-Expert Member
Sep 26, 2012
3,115
3,862
Habari za kuachiwa kwa dhamana Mkurungenzi wa ulinzi na usalama wa Chadema na Mwenyekiti wa chama hicho mkoani Kagera Bw, W. M. Rwakatare maarufu hapa Bukoba kama "Egaju" zimeilipua Bukoba kwa furaha na sasa kila kona unayopita gumzo ni kuachiwa kwa mwanasiasa huyo aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la Bukoba mjini.

Habari hizo zimezagaa ghafla kupitia mitandao ya kijamii na redio za hapa Kagera, isipokuwa redio ya Mh Kagasheki, redio Kasibante jina amabalo uhusishwa sana na mvutano wa kisiasa kati ya Kagasheki na Rwakatare. Jina la utani la Rwakatare "Engaju" linamaanisha ng'ombe mkubwa mwenye pembe ndefu maarufu sana mkoani Kagera wakitokea Uganda, na jina la redio "Kasibante" linamaanisha kumfunga ng'ombe.

Honi za magari zimepigwa na vjana wengi walilipuka kwa makelele baada ya kusikia habari hizo toka redio Vision iliyoko mjini Bukoba. Vijana wengi wamesikika wakisema "tunataka kuvunja rekodi yetu wenyewe ya mapokezi, maana Ccm hata akija nani hawezi vunja rekodi ya mapokezi ya Dr Slaa" aliongeza "tunataka kuuonyesha ulimwengu kuwa tulisikitishwa na kesi ya kipuuzi lakini iliyomtesa kamanda wetu, tutaisimamisha Bukoba siku hiyo" alisema kijana mmoja mwendesha pikipiki.

Mama mmoja mfanyakazi wa sharika la posta mkoani hapa amasema "hata bosi anajua kwamba siku ya kumpokea Rwakatare hawezi kuniona kazini, najua hawezi kunitakisha ubaya nitamuaga siku mmoja kabla" Amesema ndiyo haki imetendeka lakini wanataka kuonyesha ulimwengu kwamba watenda haki ni wengi. "Tunataka kumuonyesha huyo Mwigulu wao kwamba tunapenda haki na kuwa tunamsubiri kwa hamu siku akija hapa tutamzomea kwa kihaya"

Nitaendelea kuwajuza kinachoendelea hapa Bk.
 
Ashukuriwe Mungu muumba wa mbingu na nchi.

Shetani kaporomoka kuelekea kuzimu.
 
Hii ni habari njema, kusikia Wanabukoba wameamka kwa kasi sana, sisi tulio mbali na nyumbani tunawapa ongera.
 
Ni haki yako, maani ni mbunge wao, aliechakachuliwa kura, well done (wasomire...wamuandalie na senene za kutosha)-utani
 
Hapa kamachumu vijana wanazunguka na pikipiki toka kamachu mjini kuelekea ndolage mala wanageuza mpaka rutenge wanadai wanashangilia na kukumbuka juhudi za Lwakatare kuwapigania tangu enzi za usafiri wa baiskeli maarufu kama asekido mpaka sasa waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda, Lwakatare kawatetea sana. Wansubiri siku ya kumpokea shujaa wao.
 
Habari za kuachiwa kwa dhamana Mkurungenzi wa ulinzi na usalama wa Chadema na Mwenyekiti wa chama hicho mkoani Kagera Bw, W. M. Rwakatare maarufu hapa Bukoba kama "Egaju" zimeilipua Bukoba kwa furaha na sasa kila kona unayopita gumzo ni kuachiwa kwa mwanasiasa huyo aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la Bukoba mjini.

Habari hizo zimezagaa ghafla kupitia mitandao ya kijamii na redio za hapa Kagera, isipokuwa redio ya Mh Kagasheki, redio Kasibante jina amabalo uhusishwa sana na mvutano wa kisiasa kati ya Kagasheki na Rwakatare. Jina la utani la Rwakatare "Engaju" linamaanisha ng'ombe mkubwa mwenye pembe ndefu maarufu sana mkoani Kagera wakitokea Uganda, na jina la redio "Kasibante" linamaanisha kumfunga ng'ombe.

Honi za magari zimepigwa na vjana wengi walilipuka kwa makelele baada ya kusikia habari hizo toka redio Vision iliyoko mjini Bukoba. Vijana wengi wamesikika wakisema "tunataka kuvunja rekodi yetu wenyewe ya mapokezi, maana Ccm hata akija nani hawezi vunja rekodi ya mapokezi ya Dr Slaa" aliongeza "tunataka kuuonyesha ulimwengu kuwa tulisikitishwa na kesi ya kipuuzi lakini iliyomtesa kamanda wetu, tutaisimamisha Bukoba siku hiyo" alisema kijana mmoja mwendesha pikipiki.

Mama mmoja mfanyakazi wa sharika la posta mkoani hapa amasema "hata bosi anajua kwamba siku ya kumpokea Rwakatare hawezi kuniona kazini, najua hawezi kunitakisha ubaya nitamuaga siku mmoja kabla" Amesema ndiyo haki imetendeka lakini wanataka kuonyesha ulimwengu kwamba watenda haki ni wengi. "Tunataka kumuonyesha huyo Mwigulu wao kwamba tunapenda haki na kuwa tunamsubiri kwa hamu siku akija hapa tutamzomea kwa kihaya"

Nitaendelea kuwajuza kinachoendelea hapa Bk.

Itakuwa bab K
 
Kwa utafiti kidogo sana nilioufanya , baada ya SHETANI , Mwingine aliyelaaniwa na watu wengi zaidi kwenye nchi hii ni MWIGULU NCHEMBA !
 
Mungu yuko daima na watenda haki,ingekuwa Lwakatare amefanya kosa asinge achiwa maana mungu wetu hadhihakiwi,
SASA WAKUBWA MWIGULU NA GENGE LAKE LA UAJI CCM WATATOKEA WAPI?
POPOTE WATZ TULIPO TUSHIRIKIANE KUITOKOMEZA CCM NI KANSA INAYOMALIZA RASLIMALI ZETU.
KARIBU KAMANDA MPIGANAJI
 
Peopleeeeeeeeeeeessssssssssssssssssss...................Paaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa Leo Nkonyagi itaniuaaaaaaaaa..............................
 
Lakini mioyo ya watu wengine ni giza sana. Yaani unmwaandalia mtu aliyeumbwa na Mungu kama wewe ufirauni wa aina hii. Mwenzetu ameteseka hivyo na kukosa familia yake. Nafikiri zamani kwenye agano la kale mtu kama huyo aliuwa pamoja na mke wake na watoto wake kwa mawe. Nchemba nakuomba nenda katubu haraka sana kabla ya hii laana haijakupata wewe na familia yako.
 
Pamoja xana kamanda tulikumic kiyaina ila kwa leo ni vizuri upumzike japo kiyaina uisalimu familia yako, lkn naamin kesho tutajua wap pa kuanzi hiz harakati za ukomboz na kwa vile ulikua celo unaweza usijue lkn ukweli ni kwamba hao magamba wamekutengenezea jina kubwa sana huku mtaani jina lililoambatana na heshima, zaman watu weng walikuwa hawakujui lkn sasa hadi watoto wadogo wanakufaham ww kama SHUJAA...,!
 
Back
Top Bottom