Wilfred Lwakatare: Mrejesho kutoka mahabusu Segerea

pole kwa yaliyokukuta kamanda makala yako inavutia kusoma umetumia weledi mkubwa katika kuandika
 
Inahuzunisha sana kwa kweli hasa hilo la watu kupewa kesi zisizo zao. Nani wa kuwasaidia watu hawa? Kumbuka leo ni kwa mwingine lakini kesho waweza kuwa ni wewe!! Pole Lwakatale kwa yaliyokufika.

Ndugu yangu Lwakatale,pole sana.Hakika Mungu ajua walio wake.Tanzania yetu ilipofika ni ya hatari na yakutisha.Vijana wameanza kujutia kuzaliwa Tanzania.Wakati ajira za vinana zinamezwa na MAFISADI kwa kutuibia rasirimali zetu,kuuza viwanda na kuvifunga,Serikali inayojiita SIKIVU inayowajali watanzania iko busy kutengeneza CD feki kuwabambikizia kesi watu,kuwasotesha rumande vijana wanaotafuta ajira kwa staili zao,hata akina dada poa hawafanyi yale kwa kujitakia.

Makala ya ndugu Lwakatale yanauma sana,sijui aidbu MACCM na MWIGULU ambaye yuko tayari kutoa ushahidi Duniani,Mbinguni wa ugaidi wa Lwakatale atauficha wapi.Siku zimehesabika za hawa watu,wataikimbia nchi kama siyo kujipiga kitanzi.Makamanda msichoke,songa mbele bila kurudi nyuma.Wengine hatuna vipaji vya kusimama majukwaani maana liziki yetu ya kila siku itaisha siku hiyo(sheria za kazi),lakini tuko pamoja nanyi.

Dr Slaa na Kamanda Mbowe, Msilale,hakikisha elimu mliyoitoa pale Morogoro na kwingineko inawafikia kule vijijini Tandahimba,Kigoma,kule Ngara,Muruvyagira,Mugikomelo na Bushubi.2014 siyo mbali uchaguzi wa mitaa,tuwakamate vizuri kwa kuwa na viongozi kila kijiji na kila shina,kwa kufanya hivyo 2015 hata KIKWETE na wenzake wataikimbia nchi.

NAKUPUA POLE SANA WEWE NA FAMILIA YAKO NA CHADEMA,maana wamezima nguvu ya M4C uma ukahama,jipangeni,sisi tuko nyuma yenu.DAIMA ANZENI NA MUNGU,NENDA NA MUNGU NA MALIZA NA MUNGU,waacheni MACCM watakufa kifo cha mende mda si mrefu.
 
Cunning? NO. I insist experience can never be imitated, it is personal and factual. To be cunning you are concealing the truth for a purpose like the other side is doing. Our government is cunning? YES because they say what they do not do, and do what they do not say.
Yes, ninakubaliana na wewe kwa upande mmoja. Uzoefu unapatikana kwa kutenda na Lwakatare ameyaona kwa macho yake na kuyatenda baadhi ya mambo aliyoyaelezea katika article yake, lakini pia ninapatwa na kigugumizi kununua yote aliyoyasema kama ni kweli kwa sababu ya nature ya swala zima na muhusika ambaye ndiye mleta article.

Binadamu siyo maraika na serikali nayo inaongozwa na binadamu kwa maana hii, hatuwezi kutegemea Lwakatare anaweza kusema ni kweli alifanya kitendo kilichompelekea kupata uzoefu jela wa mambo aliyotuelezea na pia hatuwezi kusema serikali ni wasafi kwa sababu kuna mambo imefanya yanayotuonyesha kuwa tatizo ndani yake.

Kwa mazingira ya Tanzania kijamii, inakuwa ni vigumu sana kuupata ukweli matokeo yake wananchi wanaishi kwa kutegemea INSTINCT zao ambazo mara nyingi zinakuwa WRONG.
 
Pole sana Bwana Lwakatale! Mungu alikupeleka gerezani ili ujifunze jinsi watu wanavyoish huko ktk vyombo vya usalama na mbinu nyangine za kueneza ukomboz hata kwa walio kizuizini ninaamini utashinda kesi inayokukabili Mungu yu nawe. Endelea kukipigania chama na sis Ma-volunteer tusiopenda kuchukua kadi za chama lkn tunaendelea kukieneza chama kwa nguvu zote tupo na tutaendeleza harakati bila malipo wala kuchoka na pengine sisi ma-volunteer tupo wengi zaidi ya wanachama wa Chadema! na tutazid kukipigania kwa nguvu ikiwemo kutoa elimu ya uraia,kujiandikisha kupiga kura na kupiga kura kwenyewe!
Bwana Lwakatale,endelea kukipigania chama. Mungu akubaliki sana!
 
....a very touching piece by Lwakatare.....hongera sana mkuu na pole kwa yote....Nafurahi kuona unaimba concept ya change...real change begins with people....endelea kuimarisha hii concept mkuu.....watanzania wanahitaji sana hii aina ya change......
 
safi sana, makala nzuri mno.

kama ni kusafishwa basi Shekhe Ponda kwa mara ya kwanza leo amesafishwa vilivyo, nimeanza kurudisha imani kwa mbaali juu ya shekhe Ponda, bado natafakari.

Ndugu rudisha imani kwa Ponda, Kesi zote zile kwa kuwa anajitahidi kurudisha mali ya Wakfu kwa waislamu baada ya BAKWATA na Kigogo mmoja na Mfadhili mkubwa wa CCM kuuziana kiwanja hicho kitu ambacho hakikushirikisha waumini ambao ndio wenye mali, Pia hata sheria zetu za nchi zinasema mali za wakfu haziuzwi ila Watawala wetu walikipatia kiwanja hicho matumizi mazuri zaidi ya wale wenyemali. Hivyo mzee wa watu anapewa kashkash kwa kuzuia madili ya wakubwa wanaowafanyia waumini akiwepo mwenyewe.
Ndani ya Tanzania utasikia mengi sana, Hizi bado ni Trela tu "Subiri siku CCM ikiondoka madarakani usikie vimbwanga vyake" Tuombe uhai tu.
 
pole ndugu lwakatare, kuna somo nimepata hapa tusiichukie tanzania coz Tanzania ni mama tulichukie hili balaa kansa ccm amablo linaomaliza Tanzania na kisha kutuchonganisha wenyewe, nimevutiwa na ule mfano wa nyumba za uswazi wanishi watu hamsini fulu kuazimana vyombo kutumana sokono kukaribishana chalula bila kuulizana ati huyu kuku kachinja nana au wewe dini gani, EeeMungu ilaani na uitokomeze ccm na viongozo wake ili Tanzania ibaki salama. Amen.
 
Kamanda pole sana, najaribu kufikiri juu ya siku 92 uko ndani siyo mchezo lakini ndiyo safari na gharama ya ukombozi wa MTANZANIA. Mtiririko wa makala yako si wa kawaida, unavuta hisia ya mtu, nimesoma neno kwa neno, sentensi kwa sentensi nimeishia kutokwa na machozi mwishoni. MUNGU NI MKUBWA NA ALUTA CONTINUA.
 
Lakini Kamanda hebu na wewe funguka vizuri hasa kwenye Point ya msingi, ilikuwaje ukanasika kiasi kile? Au kwa muda wako baada ya akili kutulia jaribu ku-play hako ka-cd kisha u-comment (YOU TUBE- CHADEMA HAPA LWAKATALE ALIKUWA ANAMAANISHA NINI?).
 
Hakika hii makala inahuzunisha sana but haya ndiyo maovu ya ccm.
Tutawang'oa kwa nguvu zote hawa ccm.
 
Makala inavutia kuisoma.Umeandika kwa hisia sana,huku ukitafuta kuonewa huruma.Vipi kuhusu mshirika wako mloshitakiwa pamoja,Ludo kijana wa nyumbani?Ina maana hamjaonana kabisa huko selo?Nilitegemea ungemzungumzia kidogo kwenye hii taarifa yako.
 
This is a milestone, thus CCM is all but dead

More importantly Killing itself!
 
leo nimemsoma Lwakatare... kuna mengi tusiyoyajua na kama alivyoiweka vyema, TUNA NADHARIA NYINGI SANA!!

Wilfred nashukuru kukusoma kinamna hii, halafu pia nimependa sana serikali ilivyokosea na kuwaweka nyie "magaidi wawili" pamoja, imefungua avenue hatari sana kwake kwani mmetupa taswira nyingine kabisa na reality mpya

Kweli ukimpiga chura teke, basi ujue unamfupishia safari... i see positives out of the whole saga
 
Makala inavutia kuisoma.Umeandika kwa hisia sana,huku ukitafuta kuonewa huruma.Vipi kuhusu mshirika wako mloshitakiwa pamoja,Ludo kijana wa nyumbani?Ina maana hamjaonana kabisa huko selo?Nilitegemea ungemzungumzia kidogo kwenye hii taarifa yako.
Jamaa si mjinga kama unavyofikiri, hajamgusi Ludo wala kesi yake

kwi kwi kwi... hebu kuza kuza basi hiyo IQ
 
Mungu akutetee na kusimamia haki yako.WANAJAMVI kwa hii makala kuna mengi ya kujifunza na moja ni ILI.Aliyetoka JKT MWIGULU hajajifunza bado domo chafu kwa mitusi.Aliyetoka Mahabusu LWAKATARE ameongeza ufahamu na uwelewa kuhusu mambo yanavyokwenda.
 
Back
Top Bottom