Wilbur Ross asema virusi vya Corona vitawapatia ajira Wamarekani wengi

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
3,796
2,000
Katibu wa maswala ya kibiashara nchini Marekani Wilbur Ross amesema kwamba mlipuko mbaya wa virusi vya Corona nchini China unaweza kuinua uchumi wa Marekani.

Wakati wa mahojiano katika runinga bwana Ross alisema: Nadhani vitasaidia kurudisha ajira kaskazini mwa Marekani.

Kuenea kwa kasi kwa ugonjwa huo kumezua hofu kuhusu athari zake katika uchumi wa China na ukuwaji wa uchumi kwa jumla .

Matamshi hayo yamepokewa kwa hisia kali kutoka kwa wakosoaji wa utawala wa rais Trump. Akijibu swali kutoka kwa mwandishi wa runinga ya Fox kuhusu iwapo mlipuko huo ni hatari kwa uchumi wa Marekani, bwana Ross alisema: ''Sitaki kuzungumzia kuhusu mafanikio kuhusu ugonjwa huu hatari. Ukweli ni kwamba unatoa fursa kwa biashara. Hivyobasi nadhani utasaidia kuongeza ajira kaskazini mwa Marekani'', aliendelea kusema.

Baadaye wizara ya biashara iliunga mkono matamshi yake: ''Kama katibu Ross alivyoweka wazi kitu cha kwanza ni kuhakikisha kuwa virusi hivyo vinadhibitiwa na baadaye kuwasaidia waathiriwa wa ugonjwa huo. Pia ni vyema kutazama athari za kufanya biashara na taifa ambalo lina historia ya kuzuia hatari nyingi kwa watu wake na dunia nzima kwa jumla'', alisema msemaji.

Matamshi hayo yamekosolewa pakubwa , huku mbunge wa chama cha Democrat, Don Beyer akichapisha katika Twitter na kuuliza ni vipi mtu anaweza kuchukua fursa ya kibiashara katika mlipuko mkubwa.

Wanauchumi pia wameuliza maswali mengi kuhusu matamshi ya bwana Ross. Simon Baptist kutoka kitengo cha ujasusi cha Singapore aliambia BBC kwamba matamshi hayo yalimshangaza yeye binafsi.

''Kampuni hazitaweza kupata uwekezaji wa kipindi kirefu kutokana na mlipuko ambao huenda ukaathiri watu kwa kipindi cha miezi mitatu hadi sita'', alisema.

Alisema kwamba virusi hivyo huenda vikawa na athari mbaya badala ya nzuri.
''Ukweli ni kwamba Marekani itapoteza pakubwa kwa sababu licha ya kila kitu China ni soko lake kubwa, hivyobasi iwapo uchumi wa China utapunguza kasi katika ukuwaji wake utaathiri pakubwa uchumi wa Marekani vilevile''.

Virusi hivyo vipya vimetajwa kuwa janga la kiafya na shirika la afya duniani WHO huku vikiendelea kusambaa nje ya China.

Takriban watu 213 wamefariki kutokana na virusi hivyo nchini China na sasa vimesambaa hadi katika mataifa 18 mengine.

Wanauchumi wamesema kwamba virusi hivyo vya Corona vinaweza kuwa na athari kubwa katika uchumi zaidi ya virusi vya SARS vilivyozuka kati ya 2002-2003.

SARS uliambukiza watu 8000 na kusababisha vifo vya watu 700 na unakadiriwa kugharimu uchumi duniani takriban $30bn.

Virusi vya Corona vimelazimu kampuni mbalimbali duniani zikiwemo zile za teknolojia , watengenezaji magari na wauzaji kufunga kwa muda nchini China huku mamlaka ikiendeleza likizo ya kusherehekea mwaka mpya na kuweka vikwazo vya usafiri katika taifa hilo.

Chanzo: BBC Swahili
 

Jics

JF-Expert Member
Dec 16, 2016
239
500
Kumbe ni bbc
maana sijawahi ona wakiandika uxiri hata mmoja kwa trump kwa kweli.
 

Elungata

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
37,479
2,000
Huo ugonjwa utakua solved ndani ya miezi 3
Chanjo itakua tayari,tuna wiki tatu za ugonjwa,ma'am ukizi karibu 17000,
Vifo 360,
Waliopona 450
Serious case 2000
Means 14000 bado hawako kwenye hatari ya kifo ,Wana nafuu kwa ufupi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom