Wilbroad Slaa – Hii Ndiyo Fact Check Sahihi na ya Wazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wilbroad Slaa – Hii Ndiyo Fact Check Sahihi na ya Wazi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Abunuwasi, Oct 29, 2012.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. A

  Abunuwasi New Member

  #1
  Oct 29, 2012
  Joined: Oct 29, 2012
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wilbroad Slaa – Hii Ndiyo Fact Check Sahihi na ya Wazi

  WAHENGA waliamini kuwa tabia na hulka ya binadamu haibadiliki hata akiwa na umri mkubwa kiasi gani. Chukulia mfano wa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Wilbroad Slaa. Huyu kwa umri wake, kwa asili yake ya kupitia mifumo ya dini ya Kikristo madhehebu ya Kikatoliki, asingekuwa mtu wa kutunga, kusema na kuwaaminisha watu ukweli. Huyo ni mtu ambaye alikuwa padre, kiongozi mkubwa wa kiroho. Usingemtegemea kabisa kutunga na kuwaambia watu uongo. Kwa hakika, tabia yake hiiya kutunga na kusema uongo inazua maswali kuhusu mfumo mzima wa kulea watoto katika Seminari na kufundisha mapadre katika Kanisa hili.

  Mtu kama Slaa – mzushi, mwongo, mnafiki asiyeheshimu watu anaweza vipi kufikia hatua ya kuwa padre; baya zaidi aliweza vipi kupanda ndani ya mfumo huo hadi kufikia kuwa Katibu wa Baraza la Maaskofu (TEC). Nasema haheshimu watu kwa sababu mtu anayetaka watu wamchangue awaongoze, hawezi tena kushiriki katika tabia ya kuwadanganya na kuwafanya wapumbavu. Lakini Bwana Salaa hili halimnyimi usingizi. Majuzi, Ijumaa, kule Sikonge, Tabora amezua na kutunga jipya. Amedai kuwa Julai 2, mwaka huu, 2012, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete alisafiri kwenda Hong Kong kumwokoa mtoto wake wa kiume, Ridhiwani Kikwete ambaye anadaiwa kuwa alikuwa amekamatwa na mihadarati siku moja kabla, yaani Julai Mosi.

  Huu ni uongo wa dhahiri kwa sababu ratiba ya Mhe. Rais Kikwete katika siku hizo anazozitaja Slaa iko wazi.
  Julai Mosi, akitumia Ndege ya Rais, alisafiri kwenda Rwanda ambako alihudhuria Sherehe za Miaka 50 ya nchi hiyo na akalala mjini Kigali. Julai 2 alisafiri kwenda Bujumbura kuhudhuria Sherehe za Miaka 50 ya Burundi. Alirejea Dar es Salaam Julai 3 na Julai 4 alikutana na ujumbe wa Kampuni ya IBM na Mjumbe Maalum kutoka Zimbabwe. Julai 5, alikwenda Dodoma ambako aliendesha Kikao cha Baraza la Mawaziri na kurejea Dar es Salaam siku hiyo hiyo. Sasa alikwenda Hong Kong lini? Ama alikuwa Burundi na Hong Kong siku hiyo hiyo? Slaa anadai pia kuwa alipowasili Hong Kong, Mheshimiwa Rais Kikwete alipokelewa na Balozi wa Tanzania nchini China, Mheshimiwa Philip Marmo ambaye alimpeleka kwenye mkutano na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China Mheshimiwa Hu Jintao. Huu ni uongo mwingine wa dhahiri na ambayo sijui unamsaidia nini Slaa. Slaa anasema uongo kuhusu Balozi Marmo kwa sababu ratiba ya Mheshimiwa Marmo kwa siku sita za mwezi Julai nayo iko wazi na siyo kificho.

  Kwanza, Ubalozi wa Tanzania katika China hauko Hong Kong bali uko mjini Beijing na Mheshimiwa Marmo hajawahi hata kufika Hong Kong. Taarifa kutoka Hong Kong amekuwa anazipata kutoka kwa Balozi Mdogo wa heshima wa Tanzania Mheshimiwa Clement Chan. Hata juzi, Ijumaa, Oktoba 26, Balozi Marmo alikutana na Bwana Clement Chan. Balozi Marmo anapanga kutembelea Hong Kong kwa mara ya kwanza mwishoni mwa mwezi ujao, Novemba, 2012. Angalia ratiba ya Mheshimiwa Marmo katika wiki ya kwanza ya mwezi Julai mwaka huu:

  Julai Mosi, Balozi Mamro alikuwa ofisini Beijing. Julai 2, Balozi alihudhuria Sherehe za Siku ya Mongolia mchana na usiku alihudhuria Sherehe za Siku ya Djibouti kwenye Hoteli ya Lengedane mjini Beijing. Siku nzima ya Julai 3 alishiriki katika warsha ya Kampuni ya China Chemicals Techonologies Group ambayo inataka kufungua viwanda cha madawa na mbolea nchini Tanzania. Asubuhi ya Julai 4, Balozi Marmo alikutana na ujumbe wa Kampuni ya Sichaun Honda Group inayowekeza katika miradi ya Mchuchuma na Liganga na jioni ya siku hiyo alikutana na ujumbe wa Kampuni ya Mawasiliano ya ZTE. Julai 5, Balozi alihudhuria Sherehe za Siku ya Venezuala Day na Julai 6 alijiunga na Mabalozi wa Nchi za Jumuia ya Afrika Mashariki katika mkutano wa Forum on Trade na Cooperation na jioni alihudhuria Sherehe za Rwanda Day. Sasa, Balozi Marmo alikwenda lini Hong Kong kumpokea Mheshimiwa Rais kama siyo uongo?

  Katika siku zinazotajwa, Bwana Ridhiwan alikuwa Dar es salaam muda wote. Kwa hakika, Ridhiwan hajapata kufika Hong Kong ama China katika maisha yake yote. Nchi pekee inayokaribia China ambayo amewahi kuitembelea ni Dubai kwa sababu hata India hajapata kufika. Ratiba hizi za Mhe. Rais na Mheshimiwa Marmo na ukweli kuwa Ridhiwan hajapata hata kufika China ama Hong Kong ni ushahidi usiopingika kuwa Mzee Slaa kwa mara nyingine ametunga, yeye amekuwa bingwa wa goofing. Huyu ni mtu anayezeeka vibaya. Tunaamini kuwa ameanza kuchanganyikiwa pengine kwa kuzidiwa na jukumu ya kulea mtoto-mjukuu na kumtunza mchumba Bi Josephine ambaye wanaishi kama vimanda kwa sababu huyo mama bado anayo ndoa halali. Pole sana Mzee Slaa kama Josephine na mwanae amekushinda mrudishie mwenye mali yake.
   
 2. don12

  don12 JF-Expert Member

  #2
  Oct 29, 2012
  Joined: Oct 11, 2012
  Messages: 653
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  hakusema ridhiwani ni mdogo wake na ww mzushi,
   
 3. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #3
  Oct 29, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,743
  Likes Received: 832
  Trophy Points: 280
  vipi ni yule muuza madawa Rizone amekutuma kuja kutukana au ni wewe mwenyewe Rizone,lilikutach lile heheheee??utashangaa sana una degree lakini unauza madawa ya kulevya,unaonaje ukitumia elimu uliyogharamiwa na hela za walala hoi kuwa mbunifu na mchapa kazi,kwani nani alikudanganya baba yako akiwa Rais ni lazima uwe tajiri??hizo mali zitawatokea matakon,i siku isiyojulikana
   
 4. Kiona

  Kiona JF-Expert Member

  #4
  Oct 29, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 933
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Samwel Six amekupa madebe mangapi ya mahindi mpaka uje uandike pumba hapa? Au umepokea sukari kutoka kwa dogo mwenye malori ya mafuta?

  Kuna wale watu ukienda bar wanakuja wanakaa meza yako wanaanza kukusifia na kukupamba mambo kibao ilimradi tu uwaagizie bia. Sishangai
   
 5. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #5
  Oct 29, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,364
  Likes Received: 2,034
  Trophy Points: 280
  Hujui unachokiandika! Alichokiongea Dr. Slaa ni sahihi japo vyombo vya habari vinaficha ukweli wa mambo!
   
 6. M

  Magesi JF-Expert Member

  #6
  Oct 29, 2012
  Joined: Jul 10, 2012
  Messages: 2,590
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wewe ni msemaj wa ikulu ama ni nani mkuu ili tukijibu vizuri
   
 7. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #7
  Oct 29, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,493
  Likes Received: 1,833
  Trophy Points: 280
  Du!
  Hapa sitii neno,watu wazima kuchorana nooma!
   
 8. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #8
  Oct 29, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,909
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 145
  mbona nguvu ya kukanusha imekuwa kubwa hivi?
   
 9. M

  Mndokanyi JF-Expert Member

  #9
  Oct 29, 2012
  Joined: Sep 6, 2012
  Messages: 630
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ukweli unauma
   
 10. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #10
  Oct 29, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,909
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 145
  kanusha kuhusu yale masaa na namba za gari zilizotajwa.hata EPA slaa alisema uongo!
   
 11. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #11
  Oct 29, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,054
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Dr Slaa kasema ukweli. Ridhiwan alikamatwa na madawa ya kulevya China. Nusura anyongwe ila JKilaza akaenda mbio mbio kumwokoa. Soon nitakuja na ushahidi kamili wa hili.
   
 12. BHULULU

  BHULULU JF-Expert Member

  #12
  Oct 29, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 4,894
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Kanusheni tu ila iko siku kila kitu kitakuwa wazi nakumbuka huu usemi wa Slaa "......Ikulu ni weupe kama karatasi..."Hivyo hakuna litakalojificha.
   
 13. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #13
  Oct 29, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,275
  Likes Received: 353
  Trophy Points: 180
  Mbona hili suala liko wazi linaitajinkulitetea kweli?
   
 14. U

  Ukana Shilungo JF-Expert Member

  #14
  Oct 29, 2012
  Joined: Apr 17, 2012
  Messages: 813
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45

  raise issue,huna adabu umekosa malezi,huwezi kumtukana mtu WA heshima,kama uwongo fungueni mashtaka,halafu we si msemaji wa rIZONE.MODS NAMCHANA JAMAA NIKO TAYARI KWA BANN ,KWA MARA NYINGINE,HUYU JAMAA ANATUMIA MAVI BADALA YA UBONGO,HE CAN NOT UNDERSTAND BEYOND THE VISIBLE MEANING.
   
 15. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #15
  Oct 29, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,364
  Likes Received: 2,034
  Trophy Points: 280
  Huyu ni wa POLICCM tu - anatembea na kitu chenye ncha kali!
   
 16. MR. ABLE

  MR. ABLE JF-Expert Member

  #16
  Oct 29, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 1,479
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 133
  Abunuwasi

  Join Date : 29th October 2012

  Posts : 1
  Rep Power : 0
  Likes Received: 0

  Likes Given: 0

  Umeingia kwa hasira bila hata kubisha hodi!!!!!!!

  Basi mama basiiii.... futa mapovu mdomoni, punguza hasira usiendelee kulia..
   
 17. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #17
  Oct 29, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,836
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 0
  Anza kujitambulisha kwenye jukwaa la utambulisho
   
 18. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #18
  Oct 29, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,909
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 145
  huu ni ujumbe wa mwana JF ulioletwa hapa jamvini mida ya saa saba mchana 13;31 julai mosi.

  lakini si tumeambiwa mambo yote yalitendeka usiku??
   
 19. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #19
  Oct 29, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,666
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Karibu JF RIZ1 Posts : 3 Join Date : 29th October 2012 Rep Power : 0 Likes Received 0 Likes Given 0
   
 20. A

  Asa79 JF-Expert Member

  #20
  Oct 29, 2012
  Joined: Jul 19, 2012
  Messages: 591
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mbona unatoka povu hivyo? mkamate dr.slaa uone..........we kweli b.w.e.g.e yaani unadhani km rais alisafiri kwenda hong kong kumuokoa mtoto wake wkt hana ratiba ya kiserikali atakuambia alienda?.....mbona alijitengenezea kampuni feki yeye kwa kushirikiana na rostam na lowasa ile richmond lkn kakaa kimya mpaka lowasa alipoona anahukumiwa peke yake ndipo akamtaja na kikwete..........we mtu wa hivyo kabisa yaani ulitaka kikwete aseme jamani nilikuwa kumuokoa mtoto wangu ...........
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...