Wilbroad Mutafungwa Mkuu Mpya Wa Kikosi Cha Usalama Barabarani Tanzania

Habari Zilizotufikia Hivi Punde, IGP Simon SIRO Amefanya mabadiliko ya Mkuu wa Trafik Na Kumteua Wilbroad Mutafungwa kuwa Mkuu Mpya wa kikosi cha usalama barabarani.
Fortunatus Muslim anaenda kuwa RPC Mkoa wa Morogoro.
Ni jambo jema!
 
Tujiandae kwa faini zisizo na mashiko maana sasaivi hata ya kubrashia viatu hawataki, ni kukuchorea mkeka tuu kwa kwenda mbele hata huna kondom kwenye gari.
 
Hii imekaaje wajuvi wa mambo? Ilitokea kwa Mpinga na sasa kwa Muslim,yaani utoke Tanzania nzima uende mkoani.Hii mbona ni kama demotion? Wajuvi wa vyeo vya polisi tudadavulieni
Hapo wamebadilishiwa majukumu tu wala hakuna aliyepanda wala kushuka cheo, ila kwa hela za kiwi Muslim kala shavu zaidi, hakuna sehemu yenye umateumate pale polisi Kama uRPC ukiondoa IGP
 
Habari Zilizotufikia Hivi Punde, IGP Simon SIRRO Amefanya mabadiliko ya Mkuu wa Trafik Na Kumteua Wilbroad Mutafungwa kuwa Mkuu Mpya wa kikosi cha usalama barabarani.

Fortunatus Muslim anaenda kuwa RPC Mkoa wa Morogoro.

Kangi Lugola alikuwa na ubunifu ulioleta mwelekeo chanya na kupunguza manyanyaso na hata zile za kubrashia viatu. Katika hayo haya hapa yalirejeshwa kinyemela baada ya Kangi kutumbuliwa:

1. Matumizi ya simu binafsi kwenye kurushiana majini.

2. Gari moja kutopigwa faini zaidi ya moja ubovu ukinyumbulishwa kama makosa tofauti.

3. Aliweka namba yake ya simu wazi kwa ajili ya kupokea malalamiko ya waliokuwa wakionewa na kuyatolea ufumbuzi.

4. Nk, nk.

Kamanda Mutafungwa tembelea kwenye mazuri ya Kangi utatoboa.
 
Back
Top Bottom