Morogoro. Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Kebwe Stephen amesema baadhi ya maeneo katika halmashauri za wilaya za Gairo, Kilosa, Mvomero, Morogoro Vijijini na Manispaa yameripotiwa kukabiliwa na ukame.
Dk Kebwe amesema ukame huo umesababisha viashiria vya upungufu wa chakula kuonekana kuanzia Januari hadi Machi.
Hata hivyo, Dk Kebwe amesema kwa sasa hakuna halmashauri iliyoripoti uwapo wa njaa kulingana na tathmini ya kina ya hali ya chakula na lishe inayoendelea kimkoa.
“Kwa sasa nimewaagiza wakuu wa wilaya kuhakikisha wanawaelekeza wananchi kuweka akiba ya chakula na kuacha tabia ya kukiuza kile walichovuna,” amesema.
Chanzo: Mwananchi