Wilaya za Kahama, Bukombe zatajwa kuwa vinara wa uhalifu

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
Wilaya za Kahama na Bukombe mkoani Shinyanga ndizo wilaya vinara wa matukio mballimbali ya uhalifu yakiwemo matukio ya ujambazi na unyang’anyi wa kutumia silaha.
Kamanda wa Polisi mkoani Shinyanga, Diwani Athumani, amethibitisha kuwa wilaya hizo ndizo zenye changamoto nyingi kwa jeshi la polisi na ulinzi shirikishi ambapo matukio mengi ya uhalifu na mauaji ya vikongwe kuendelea kuripotiwa wilayani humo.
Kamanda huyo alitoa taarifa hizo kufuatia kuongoza katika matukio mbalimbali hasa ya ujambazi na mauaji ya vikongwe kwa mwaka jana.
Athumani aliwambia waandishi wa habari kuwa moja ya sababu kubwa ya kuwepo kwa hali hiyo ni kwa wilaya hizo kuwa na mwingiliano mkubwa wa wageni wa ndani na nje ya mkoa wa Shinyanga, mikoa jirani na nchi jirani.
Aidha, alisema wilaya hizo zimekuwa na maeneo yenye shughuli za uchimbaji mkubwa na mdogo wa madini ya dhahabu na almasi.
Kadhalika, wilaya hizo zina mwingiliano mkubwa kutokana na kuwepo kwa barabara kuu ya lami kutoka Isaka hadi nchi jirani za Rwanda, Jamhuri ya Kimedokrasi ya Kongo (DRC), Burundi na Uganda pamoja na kambi za wakimbizi zilizo kuwa katika mikoa jirani ya Kagera na Kigoma.
Alisema kutokana na hali hiyo, matukio ya mauaji ya vikongwe na watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) yamekuwa ukijitokeza ndani ya maeneo hayo na maeneo mengine kama Bariadi, Shinyanga, Maswa na Meatu yakihusika kwa asilimia kidogo.
Kuhusu hatua zinazotarajiwa kuchukuliwa na jeshi hilo kupamabana na hali hiyo, alisema kuanzia 2011 polisi wamejipanga kuhakikisha hali ya amani na utulivua inarejea katika maeneo yote yenye uhalifu.
“Jeshi la polisi tumejipanga kwa mwaka 2011 kwa kuhakikisha kuwa uhalifu unapungua au kuondoka na kutoweka kabisa, ninachosema hao majambazi watafute shughuli nyingine ya kufanya,” alisema Diwani.
Alifafanua kuwa polisi kwa kutumia ulinzi shirikishi, watashirikiana na wananchi kwa kupata taarifa zinazohusu uhalifu na kwamba hazitavujishwa.
Aidha, alisema kuwa watahakikisha wanawatumia sungusungu kuimarisha ulinzi katika wilaya hizo na kwamba vikundi vya sungusungu vinapatiwa elimu na mbinu za ulinzi na usalama.
CHANZO: NIPASHE
 
Back
Top Bottom