Wilaya ya Meatu Ikoje?

Yohana Kilimba

JF-Expert Member
Dec 25, 2012
8,105
5,629
Natokea Iramba!Ila Kikazi Nilikuwa Bukoba,Na Muda Si Mrefu Nitaenda Kuripoti Meatu Baada ya Kubadilishana na Mwalimu Wa Meatu!(Nafundisha Sekondari O-Level)!Naomba Wenyeji Mnambie:
a)Fursa za Biashara zikoje?
b)Fursa za Kilimo zikoje?
c)Nature ya Wenyeji ikoje?
d)Hali ya Usafiri ikoje?Mathalani,mimi itabidi nitoke kwetu Iramba nifike mpaka Bukundi,kisha nipate usafiri hadi Mwanhuzi!Umbali wake ukoje?
e)Upatikanaji wa Huduma za Kijamii Ukoje?
Karibuni
 
meatu nimekaa kama miez miwili..
bukundi ni kijiji kilichopo nje kabisa ya wilaya ya meatu.. huko hata network ni ya shiiida sana, mwanhuz ndo mjini, mji ni mdogo sana, na haujapanuka kibiashara, wenyeji ni wasukuma, nadhan unaelewa tabia za wasukuma, meatu suala la umeme ni tatizo ni jipu.. umeme hukatka kila mara yan haupo stable kabisaa.. usafiri pia ni shidah hasa wa kwenda huko vijijini..
 
Ticha umekubali kubadilishana sehemu za kazi bila kufanya utafiti wowote, wewe jasiri
 
Meatu zinapatikana mvua za wastani lakinu mazao kama mahindi, mpunga na pamba yanastawi.
Miundo mbinu ya usafiri si mbaya maana usafiri wa kwenda Mwanza, Shinyanga, Arusha na hata Singida kupitia Igunga unapatikana.
Biashara unaweza fanya maana mzunguko wa pesa si haba hasa wakati wa msimu wa kuuza pamba.
Wenyeji ni wakarimu usitie shaka.
 
meatu nimekaa kama miez miwili..
bukundi ni kijiji kilichopo nje kabisa ya wilaya ya meatu.. huko hata network ni ya shiiida sana, mwanhuz ndo mjini, mji ni mdogo sana, na haujapanuka kibiashara, wenyeji ni wasukuma, nadhan unaelewa tabia za wasukuma, meatu suala la umeme ni tatizo ni jipu.. umeme hukatka kila mara yan haupo stable kabisaa.. usafiri pia ni shidah hasa wa kwenda huko vijijini..
nashukuru,kumbe kuna haja ya kununua solar panel!
 
Meatu zinapatikana mvua za wastani lakinu mazao kama mahindi, mpunga na pamba yanastawi.
Miundo mbinu ya usafiri si mbaya maana usafiri wa kwenda Mwanza, Shinyanga, Arusha na hata Singida kupitia Igunga unapatikana.
Biashara unaweza fanya maana mzunguko wa pesa si haba hasa wakati wa msimu wa kuuza pamba.
Wenyeji ni wakarimu usitie shaka.
nashukuru,kwa kunifungua macho
 
Umezaliwa porini ( Iramba) unahama kazi porini (BUKOBA) na unataka kwenda porini zaidi ( Meatu) hongera mi nakupa jina we ni Mpori pori.
 
ndiyo,sikufuatilia kwani iko pua na mdomo na iramba!ukiangalia ramani utaona wilaya za Meatu na Iramba Ni Jirani!
Iramba nimekaa Mkuu na nimejua sababu ni hiyo lakini ulitakiwa udadisi kabla hufanya maamuzi, hata hivyo hakijaharibika kitu
 
Fursa nyingine ni za kitalii,kuna hifadhi huko tena imeungana na Serengeti na Ngorongoro,biashara ya chips inalipa kwa pale mwanhuzi.......mwaka jana nilikuwa huko,hakuna lami kwa njia zote zinazoingia wilaya hiyo ila njia sio mbaya ila vumbi ni shiidah!!kutoka Bk-Meatu yataka moyo,ni mkoa mpya wa Simiyu.
 
Back
Top Bottom