Wilaya ya Kongwa: Tabibu ahukumiwa kwenda jela miaka sita kisa rushwa 100,000/-

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
2,054
2,000
Mahakama ya Wilaya ya Kongwa, imemhukumu Ofisa Tabibu wa wilaya hiyo, Martine Ndahani, kifungo cha miaka sita jela baada ya kupatikana na hatia ya kumshawishi mwananchi ampe rushwa ya Sh. 100,000 ili mgonjwa wake aongezwe damu.Hukumu hiyo ilitolewa jana na Hakimu Mfawidhi wa Wilaya hiyo, Kisasila Malangwa, ambaye alisema adhabu hiyo imetolewa baada ya kusikiliza mashahidi tisa waliojitokeza kwenye kesi hiyo.

Alisema kwa upande wa mtuhumiwa ulikuwa na mashahidi watatu waliojitokeza kutoa ushahidi ambao mahakama haikuridhika nao.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Malangwa alisema baada ya kusikiliza ushahidi huo, mahakama inamhukumu kifungo cha kwenda jela miaka sita au kulipa faini ya Sh. 500,000 kwa kila kosa alilosomewa.

Hakimu huyo alisema mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo kinyume cha kifungu namba 15 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya Mwaka 2007.

Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(Takukuru), Dodoma, Sosthenes Kibwengo, alisema baada ya Takukuru kufanya uchunguzi, walimkamata na kumfungulia mashtaka ambayo hukumu imetolewa.

Alisema kesi hiyo ilikuwa chini ya Mwendesha Mashtaka wa Taasisi hiyo, Moshi Kaaya, huku akiwataka wananchi kuendelea kutoa taarifa za viashiria vya rushwa.

Katika hatua nyingine, Mahakama ya Wilaya ya Kondoa imemhukumu kutumikia kifungo cha miaka minne Jeremia Magawa, aliyekuwa msimamizi wa miradi ya Kampuni ya FM Engineering, iliyokuwa inasambaza umeme katika Kijiji cha Kiteo wilayani Kondoa, kwa kuchukua Sh. 120,000 kwa wananchi wawili ili kuwawekea nguzo karibu na nyumba zao.

Hukumu hiyo ilitolewa na Hakimu wa Mahakama hiyo, Mateso Masao, baada ya mahakama kumtia hatiani kwa kosa la kuomba rushwa.

NIPASHE
 

secret file

JF-Expert Member
Sep 10, 2019
2,529
2,000
Hv hakuna adhabu zenye economic value.....
manake kwa 120000 kumfunga mtu naona in a long run serekali itapata hasara kubwa....
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom