Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,005
- 9,872
Wilaya ya Handeni imejipanga kuhamasisha jamii kuondokana na imani za kishirikina, badala yake ijikite kwenye shughuli za maendeleo kwenye ngazi za kaya na vijiji.
Wakati yakielezwa hayo wilaya hiyo inatajwa kuwa na jumla ya waganga wa jadi 6,600.
Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Toba Nguvila alibainisha hayo baada ya kushtushwa na idadi hiyo na baadhi ya vijiji vyake, kikiwamo cha Kwamsisi kuwa na sifa iliyoenea ndani na nje ya nchi kwa kubobea kwa uchawi. Nguvila kwa sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Muleba.
“Mahala popote nchini, mtu akitishia kwamba nitaenda Kwamsisi basi ataogopwa. Hatupaswi kuiendekeza sifa hii kwa sababu uchawi hauleti maendeleo,” alisema Nguvila na kuwataka kuondokana na sifa hiyo na wawe na sifa ya maendeleo.
Nguvila alitoa kauli hiyo alipozungumza na wakazi wa Kata ya Kwamsisi, baada ya kupokea mradi wa maji wa Kijiji cha Mkaramo uliojengwa kwa Sh143.3 milioni na Shirika la World Vision, akitaka waondokane na sifa ya waganga wengi na wachawi.
Nguvila alisema Wilaya ya Handeni ina fursa nyingi katika sekta ya Kilimo, mazingira, mifugo na madini ambazo zimekuwa zikiwafaidisha wageni na kuwaacha wenyeji katika lindi la umaskini, akisema hali hiyo lazima ibadilike.
Baadhi ya wakazi wa Kijiji cha Kwamsisi waliozungumza na Mwananchi walisema imani ya kishirikina imetawala eneo lao na husababisha baadhi yao kushindwa kujenga nyumba za kisasa kwa kuhofia kulogwa na wanaojihusisha na uchawi.