Wilaya ya HAI yakabiliwa na upungufu mkubwa wa vituo vya afya

Kinuju

JF-Expert Member
Mar 20, 2021
2,390
5,310
Hai. Halmashauri ya Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, inakabiliwa na upungufu wa vituo 10 vya afya, hali inayosababisha usumbufu mkubwa kwa wananchi pindi wanapohitaji huduma za matibabu.

Hayo yamebainishwa jana alhamisi Machi 17, 2022 na Mganga Mkuu wa Wilaya ya Hai, Dk Irine Haule wakati akitoa taarifa ya mradi wa ujenzi wa kituo kipya cha afya na nyumba ya watumishi katika kijiji cha Chekimaji kata ya Masama Rundugai, kwa kamati ya siasa ya CCM ilipotembelea na kukagua mradi huo.

Dk Irine amesema mahitaji ya vituo vya afya katika Wilaya hiyo ni vituo 17 lakini vilivyopo ni saba ambapo vya serikali ni 6 na hivyo kufanya kuwepo kwa upungufu wa vituo kwa asilimia 58.8 na kwamba vilivyopo bado havijakidhi kutojana na kukosekana kwa huduma za dharura za upasuaji.

"Wilaya ya Hai bado ina upungufu wa vituo vya Afya kwa asilimia 58.8, kwani kwa sasa vipo vituo saba kati ya 17 vinavyohitajika katika kila kata ambavyo havijakidhi viwango kwa kuwa katika vituo hivyo Sita vinavyomilikiwa na serikali, hakuna hata kituo kimoja kinachotoa huduma za dharura za upasuaji kwa sasa," amesema.

Ameongeza, "Hivyo kuleta hitaji kubwa sana la ujenzi Wa kituo cha afya hasa katika ukanda wa tambarare wa wilaya ambapo katika kata zote nne zilizopo katika ukanda huu hakukuwa na hata kituo kimoja cha afya na kituo hiki ambacho kinatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi huu, kitakuwa msaada mkubwa kwa wakazi wa ukanda huu."

Amesema mradi wa ujenzi wa kituo hicho umeunganisha miradi miwili ambapo ni ujenzi wa kituo cha afya kwa fedha za tozo ya simu na ujenzi wa nyumba za watumishi kwa fedha za Uviko -19 na kwamba miradi yote itagharimu Sh340 Milioni.

"Halmashauri ilipokea fedha za tozo za simu toka serikali kuu kiasi cha Sh250 milioni kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya Chekimaji, pia ilipokea kiasi cha Sh90 milioni ambazo ni fedha za uviko-19 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya watumishi,” amesema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Patrick Boisafi amezitaka Halmashauri za wilaya mkoani humo kuhakikisha maeneo yote ya taasisi za umma, yanakuwa na matumizi bora ya ardhi na hati miliki za ardhi ili kudhibiti uvamizi na migogoro katika maeneo hayo.

Wakati kamati hiyo ikiwa katika mradi wa kituo cha afya Chekimaji Longoi, Mwenyekiti Boisafi amehoji kama eneo hilo lina hati miliki ambapo alijibiwa halina na ndipo alipozitaka Halmaahauri kuhakikisha maeneo ya taasisi za umma yanawekewa mipaka na kuwa na hati miliki.

"Serikali tayari ilishatoa naelekezo kwamba maeneo yake yawe na hati miliki, sasa ni vyema agizo hili likatekelezwa, wekeni utaratibu hati ya maeneo yote ikiwemo hili la kituo cha afya ipatikane ili kulinda maeneo haya yasivamiwe na watu,” amesema.

Diwani wa kata ya Masama Rundugai, Simbano Waziri amesema kukamilika kwa hicho kutakuwa msaada mkubwa kwa wananchi wa kata hiyo, ambao wamekuwa wakusaka huduma umbali wa zaidi ya kilometa tano.

"Hii zahanati ni muhimu sana katika kata hii, kwani itawezesha wananchi kupata huduma za afya kwa karibu na zinazokidhi, tunaishukuru sana serikali kwa hatua hii" amesema.
 
Sera ya CCM ya kuwa na zahanati kila kijiji na vituo vya afya kila kata ni sera mbaya kwa Tanzania.
 
Back
Top Bottom